milion 50 kila kijijiiiiiiiiNdoto za vyama vya upinzani kuchukua dola mwaka 2020 huenda zikawa zimeyeyuka baada ya Chama Cha Mapinduzi CCM kuthibitisha ubora wake kwa kuendelea kutekeleza sera zake kwa vitendo katika maeneo na nyanja tofauti tofauti nchini, duru zinaeleza.
Ni ukweli kwamba Chama Cha Mapinduzi kimeamua kuifanya kazi za Watanzania kwa weledi wa hali ya juu kwani sote ni mashuhuda wa namna miradi mbali mbali yenye tija na manufaa kwa wananchi wanayonge inavyoendelea kutekelezwa kwa kasi ya kipanga.
Wakati wapinzani wakiendelea kupiga porojo CCM yenyewe imeendelea kupiga kazi za kuwaletea maendeleo na kushughulika na kero zao pasipo kuchoka.Wapinzani waelewe kwamba Watanzania wamechoka siasa uchwara za maneno matupu Watanzania wanataka vitendo tu.
CCM ina sera safi na mipango inayotekelezeka, nani aliyetegemea leo hii kuboreshwa kwa huduma za jamii kuanzia elimu,afya,maji, umeme barabara ,uchukuzi na nyinginezo kwa kasi kubwan ni wazi kuwa wananchi wamefaidika vilivyo na uwepo wa CCM madarakani.
CCM Mpya imekua kinara wa mapambano ya kulinda raslimali za nchi ili ziweze kuwanufaisha Watanzania. Sasa hivi mathalani utoroshwaji wa madini umedhibitiwa kwa kujengwa kwa ukuta wa Mererani kunakochimbwa madini adhimu yasiyopatikana kokote Duniani na kufunguliwa kwa masoko ya madini katika mikoa yenye shughuli za uchimbaji wa madini ya aina tofautitofauti .Watanzania walitaka kuona namna mapato yatokanayo na raslimali za Taifa yakifanya kazi.Kwa namna Serikali ya awamu ya Tano inavyokeleza Sera za CCM hususani katika kuwaletea Wananchi maendeleo ni ushahidi usio na chembe ya mashaka kwamba mapato hayo yanafanya kazi ya kuwatumikia Wananchi kwa uaminifu mkubwa.
Itakapofika mwaka 2020 CCM watakua na sababu lukuki za kuwaambia Watanzania kwa nini wakichague chama hicho tena wakati upande wa pili wapinzani hawatokua na sababu yoyote ya kuwaambia Watanzania kwa nini wasiichague tena CCM. Kutokana na hali hiyo ni wazi kwamba watapata kipigo kikali na watakiona cha mtema kuni.
Sera safi za CCM ni kikwazo kwa wapinzani ambao badala ya kupambana na CCM kama taasisi wao wameelekeza mashambulizi yao kwa mtu binfasi (Individual attacks), hili ni kosa la kiufundi na litawagharaimu kwa sababu CCM imeendelea kujiimarisha na kuvuna mamilioni ya wapiga kura kila siku.
Tukutane 2020 ambapo CCM itarudishwa madarakani kutokana na sera zake safi huku upinzani ukizikwa rasmi kutokana na porojo zao zisizo na maana yoyote.
Augustino Chiwinga
0756 810804 / 0559438889.