Utekelezaji wa MCC unaendelea vema, Muhongo aendeleza ubora wake usio na shaka

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
916
Marekani kuendelea kutekeleza miradi ya MCC

96.jpg
Makamu
wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa Marekani Mark Childress

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini.

Kikao hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA).

Katika kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya rushwa, huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika uendelezaji wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.

Chanzo:fullshangwe
 
Hawa watu wa MCC nao wanafiki sana, wanasema mingine kwenye vyombo vya habari, ila kwenye vificho wanafanya tofauti. Pumbavu sana!!
 
Hizi ni propaganda tuu. Muhongo alivyo muongo ametunga tu huo uongo. Picha hiyo ya lini?
Kwani MCC kutekelza miradi ina maana Muhongo ndio amefanya iwe hivyo? MCC imesainiwa mwaka 2007 wakati wa George W Bush. Muhongo wakati huo alikuwa kwenye miamba yake huko ......
Wacheni pumba nyie huyu ataendelea kuwa mwizi tuuu awajibishwe
 
Pole sana Mkuu. Usisikilize propaganda za akina Tumbili

Hapana mkuu, maana hata MWIZI kajiuzuru baada ya kuona spidi ya TUMBILI ni supersonic. Otherwise, I think we have to go one extra mile in investigating the issue. Imejaa siasa nyingi kuliko kawaida, na sijui shida ni nini. Na shida ni kwasababu ya CAG kutosema exactly kiasi gani ni cha umma na kipi ni cha MAJIZI.
 
Kwani unajueje kama hapo wanazungumzia MCC? Ama unajua hiyo picha ilipigwa mwaka gani?
 
salamu kwake kafulila ....kiko waapii sasaaa ulichokuwa unajidai nacho????...Mimi nilisema toka mwanzo Kafulila na wenzake ni waongo wakubwa watu humu jamvini wakaniraukia sasa leo tunaona wenyewe....
Marekani kuendelea kutekeleza miradi ya MCC

96.jpg
Makamu
wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa Marekani Mark Childress

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini.

Kikao hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA).

Katika kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya rushwa, huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika uendelezaji wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.

Chanzo:fullshangwe
 
Hizi ni propaganda tuu. Muhongo alivyo muongo ametunga tu huo uongo. Picha hiyo ya lini?
Kwani MCC kutekelza miradi ina maana Muhongo ndio amefanya iwe hivyo? MCC imesainiwa mwaka 2007 wakati wa George W Bush. Muhongo wakati huo alikuwa kwenye miamba yake huko ......
Wacheni pumba nyie huyu ataendelea kuwa mwizi tuuu awajibishwe

hiki kikao kilifanyika novemba 12, 2014. tembelea hapa upate full story MICHUZI BLOG: WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC
 
salamu kwake kafulila ....kiko waapii sasaaa ulichokuwa unajidai nacho????...Mimi nilisema toka mwanzo Kafulila na wenzake ni waongo wakubwa watu humu jamvini wakaniraukia sasa leo tunaona wenyewe....

hii ilikuwa kabla ya bunge kujadiili escrow
 
hiki kikao kilifanyika novemba 12, 2014. tembelea hapa upate full story MICHUZI BLOG: WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC

kama ni hivyo bado taarifa iliyositisha misaada hiyo ni Valid kwani tamko lilitolewa baada ya kikao hicho cha mwezi novemba.

Escrow yatikisa mpaka Marekani

headline_bullet.jpg
Yasitisha mkataba wa miradi kibao ikisubiri uamuzi wa Rais Kikwete
headline_bullet.jpg
Kauli ya Kafulila yatimia
Jakaya-Kikwete--December12-2014.jpg

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo, Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.

Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.

Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

“Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilikutana katika mkutano wa kila mwaka wa kuchagua nchi zitazopatiwa fedha na MCC, katika mkutano huo Bodi ilielezea hofu na masikitiko yake kuhusu hali ya rushwa nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na yale yaliyojitokeza hivi karibuni katika suala linalohusu kampuni ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taaarifa hiyo, ingawa bodi hiyo ilipiga kura ya kuiruhusu Tanzania iendelee na maandalizi kwa ajili ya mkataba wa pili wa miradi ya MCC, imehimiza Serikali ya Tanzania kuchukua hatua thabiti na mahsusi za kukabiliana na rushwa ili bodi hiyo iweze kuidhinisha mkataba huo.

Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Naye Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress, alisema kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni muhimu sana kwa mkataba mpya kati ya MCC na Tanzania katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini Tanzania.

“Tumetiwa moyo na tamko lililotolewa na Ikulu hapo tarehe 9, Desemba kwamba hivi karibuni itashughulikia maazimio ya bunge kuhusu IPTL. Tunatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu suala hili hasa kutokana na uzito wake katika masuala muhimu kadhaa ya maendeleo,” ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, Bodi iligusia makubaliano kadhaa yaliyofanyika na serikali ya Tanzania iliahidi kufanya mageuzi ya kisera, kimuundo na kitaasisi ili kuongeza ufanisi na uwazi katika taasisi zake pia na katika sekta ya nishati.

“Tunafurahi kwamba mchakato wa majadiliano ya maandalizi ya mkataba wa pili utaendelea kwa miezi kadhaa ijayo. Tunapenda kusisitiza kuwa ni lazima ahadi hizi zitekelezwe kabla Marekani haijafanya maamuzi ya mwisho kuhusu mkataba wowote mpya na Tanzania,” alisema.

Tanzania ilikuwa mojawapo kati ya nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.

Kama mkataba huu utapistishwa utakuwa ni mkataba wa pili wa MCC kwa Tanzania. Kati ya mwaka 2008 na 2013 MCC ilitekeleza mkataba wa uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 698 uliowezesha utekelezaji wa miradi ya maji, barabara na nishati ya umeme nchini kote.

Chini ya mkataba huo, mtandao wa nyaya za umeme wenye zaidi ya kilomita 3,000 ulijengwa, jumla ya kilomita 450 za barabara pia zilijengwa, hali kadhalika, mitambo mikubwa miwili ya usafishaji maji na njia ya kurukia ndege katika kiwanja kimoja cha ndege ilijengwa.

Shirika la Changamoto za Milenia ni taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea. Shughuli za MCC zinajengwa katika msingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umasikini.

Novemba mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati nchini.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Balozi Childress.

Makubaliano yalitiwa saini na Makamu wa Rais wa MCC anayeshughulikia Mikataba na Uendeshaji wake, Kamran Khan, na Waziri wa Fedha wa Tanzania, Saada Mkuya Salum.

Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alikazia akisema makubaliano hayo yalikuwa hayajasainiwa Septemba, bali kikao cha kuyapitisha kingefanyika Desemba na kushangiliwa na wabunge wa CCM.

MBATIA AKOLEZA MOTO
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amekoleza moto wa sakata Tegeta Escrow, baada ya kuwataka wananchi wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kila mmoja kudai mgao wa Sh. 609, 900 kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana na wakazi wa vijiji vya Mrimbo-Uuwo, Matala, Kondiki, Mwika Lole, Maring’a, Msae-Kinyambuo na Kondeni vilivyopo Kata ya Mwika Kusini na Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi, Mbatia aliwaambia wananchi hao kwamba hawapaswi kuendelea kuumia kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara na shule za kata kwa sababu wanao uwezo wa kutumia fedha zilizochotwa katika akaunti hiyo kuchangia maendeleo.

“Si mliona baadhi ya wabunge wa CCM wakiwatetea watuhumiwa wa wizi wa fedha za Escrow, ni hivi; wakija Vunjo kuwaomba muwapigie kura wagombea wao katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kesho kutwa, kila mtu adai kwanza hela yake shilingi 609, 000 ndo muwapigie kura…wako vigogo wanaotafuta njia za kujinasua na kashfa hii wakitafuta vijisababu eti zilikuwa za shule na wengine wametafuta watetezi wakati waliwatusi Watanzania wenzao,” alisema Mbatia.

"Katibu Mkuu Kiongozi (Balozi Sefue) anasema Rais atafanya uamuzi kuhusu maazimio ya Bunge baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha na muda mfupi baadae Ikulu hiyo hiyo, inasema Rais Kikwete atafanya uamuzi wiki ijayo, sasa tuamini kauli ipi hapa…Bunge la Januari mwaka ujao, litakuwa chungu kwa serikali kama kashfa hii itafukiwa fukiwa na kuwaacha baadhi ya watuhimiwa wakiwakejeli watanzania,” alisema Mbatia.CHANZO: NIPASHE

MH hawa watu wanatufanya sie wenda wazim hivyo waache wafanye yao kwani hum kuna walokwisha andaliwa kusafisha majina ya watu
 
Kesho utasikia Prof akiitwa dalali eti kwa vile amekutana na wadau wa wizara ya nishati na madini ofisini kwake

Pole sana Mkuu. Usisikilize propaganda za akina Tumbili

Kweli mkuu anachokifanya muhongo ni sahihi kabisa.

Hata kusoma hujui?

salamu kwake kafulila ....kiko waapii sasaaa ulichokuwa unajidai nacho????...Mimi nilisema toka mwanzo Kafulila na wenzake ni waongo wakubwa watu humu jamvini wakaniraukia sasa leo tunaona wenyewe....

Naomba mniambie hicho kikao kilikaa lini tofauti na hivyo taarifa hii hapa chini ndio inayoaminika zaidi kuliko hiyo ya kwenu

Escrow yatikisa mpaka Marekani

headline_bullet.jpg
Yasitisha mkataba wa miradi kibao ikisubiri uamuzi wa Rais Kikwete
headline_bullet.jpg
Kauli ya Kafulila yatimia
Jakaya-Kikwete--December12-2014.jpg

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo, Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.

Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.

Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

"Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilikutana katika mkutano wa kila mwaka wa kuchagua nchi zitazopatiwa fedha na MCC, katika mkutano huo Bodi ilielezea hofu na masikitiko yake kuhusu hali ya rushwa nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na yale yaliyojitokeza hivi karibuni katika suala linalohusu kampuni ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)," ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taaarifa hiyo, ingawa bodi hiyo ilipiga kura ya kuiruhusu Tanzania iendelee na maandalizi kwa ajili ya mkataba wa pili wa miradi ya MCC, imehimiza Serikali ya Tanzania kuchukua hatua thabiti na mahsusi za kukabiliana na rushwa ili bodi hiyo iweze kuidhinisha mkataba huo.

Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Naye Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress, alisema kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni muhimu sana kwa mkataba mpya kati ya MCC na Tanzania katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini Tanzania.

"Tumetiwa moyo na tamko lililotolewa na Ikulu hapo tarehe 9, Desemba kwamba hivi karibuni itashughulikia maazimio ya bunge kuhusu IPTL. Tunatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu suala hili hasa kutokana na uzito wake katika masuala muhimu kadhaa ya maendeleo," ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, Bodi iligusia makubaliano kadhaa yaliyofanyika na serikali ya Tanzania iliahidi kufanya mageuzi ya kisera, kimuundo na kitaasisi ili kuongeza ufanisi na uwazi katika taasisi zake pia na katika sekta ya nishati.

"Tunafurahi kwamba mchakato wa majadiliano ya maandalizi ya mkataba wa pili utaendelea kwa miezi kadhaa ijayo. Tunapenda kusisitiza kuwa ni lazima ahadi hizi zitekelezwe kabla Marekani haijafanya maamuzi ya mwisho kuhusu mkataba wowote mpya na Tanzania," alisema.

Tanzania ilikuwa mojawapo kati ya nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.

Kama mkataba huu utapistishwa utakuwa ni mkataba wa pili wa MCC kwa Tanzania. Kati ya mwaka 2008 na 2013 MCC ilitekeleza mkataba wa uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 698 uliowezesha utekelezaji wa miradi ya maji, barabara na nishati ya umeme nchini kote.

Chini ya mkataba huo, mtandao wa nyaya za umeme wenye zaidi ya kilomita 3,000 ulijengwa, jumla ya kilomita 450 za barabara pia zilijengwa, hali kadhalika, mitambo mikubwa miwili ya usafishaji maji na njia ya kurukia ndege katika kiwanja kimoja cha ndege ilijengwa.

Shirika la Changamoto za Milenia ni taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea. Shughuli za MCC zinajengwa katika msingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umasikini.

Novemba mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati nchini.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Balozi Childress.

Makubaliano yalitiwa saini na Makamu wa Rais wa MCC anayeshughulikia Mikataba na Uendeshaji wake, Kamran Khan, na Waziri wa Fedha wa Tanzania, Saada Mkuya Salum.

Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alikazia akisema makubaliano hayo yalikuwa hayajasainiwa Septemba, bali kikao cha kuyapitisha kingefanyika Desemba na kushangiliwa na wabunge wa CCM.

MBATIA AKOLEZA MOTO
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amekoleza moto wa sakata Tegeta Escrow, baada ya kuwataka wananchi wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kila mmoja kudai mgao wa Sh. 609, 900 kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana na wakazi wa vijiji vya Mrimbo-Uuwo, Matala, Kondiki, Mwika Lole, Maring'a, Msae-Kinyambuo na Kondeni vilivyopo Kata ya Mwika Kusini na Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi, Mbatia aliwaambia wananchi hao kwamba hawapaswi kuendelea kuumia kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara na shule za kata kwa sababu wanao uwezo wa kutumia fedha zilizochotwa katika akaunti hiyo kuchangia maendeleo.

"Si mliona baadhi ya wabunge wa CCM wakiwatetea watuhumiwa wa wizi wa fedha za Escrow, ni hivi; wakija Vunjo kuwaomba muwapigie kura wagombea wao katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kesho kutwa, kila mtu adai kwanza hela yake shilingi 609, 000 ndo muwapigie kura…wako vigogo wanaotafuta njia za kujinasua na kashfa hii wakitafuta vijisababu eti zilikuwa za shule na wengine wametafuta watetezi wakati waliwatusi Watanzania wenzao," alisema Mbatia.

"Katibu Mkuu Kiongozi (Balozi Sefue) anasema Rais atafanya uamuzi kuhusu maazimio ya Bunge baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha na muda mfupi baadae Ikulu hiyo hiyo, inasema Rais Kikwete atafanya uamuzi wiki ijayo, sasa tuamini kauli ipi hapa…Bunge la Januari mwaka ujao, litakuwa chungu kwa serikali kama kashfa hii itafukiwa fukiwa na kuwaacha baadhi ya watuhimiwa wakiwakejeli watanzania," alisema Mbatia.CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom