Utekelezaji wa Mapendekezo Yaliyotolewa Katika Baadhi ya Kaguzi za Ufanisi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mwaka 2019/20, CAG alifanya ukaguzi wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa
katika ripoti tano zilizotolewa Aprili 2016 ambazo ni;

i. Usimamizi wa utoaji leseni na mikataba ya utafutaji na uendelezaji gesi asilia.

ii. Ufuatiliaji wa utekelezaji na uzingatiaji wa Sera, Sheria na Kanuni kwenye shughuli za utafutaji wa petroli Tanzania.

iii. Utekelezaji wa matakwa ya maudhui ya ndani na uthibitisho wa gharama za uwekezaji katika mikataba ya uchangiaji wa gharama za uzalishaji.

iv. Usimamizi wa taarifa za kijiografia na kijiolojia katika sekta ya mafuta na gesi asilia Tanzania.

v. Usimamizi wa uendelezaji rasilimaliwatu katika sekta ya mafuta na gesi asilia.

Ripoti hizo zilikuwa na jumla ya mapendekezo 63 yaliyotakiwa kutekelezwa na taasisi 4 zinazosimamia utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Kati ya mapendekezo 63, ni mapendekezo 9 sawa na asilimia 14 ndiyo yaliyotekelezwa kikamilifu, mapendekezo 38 sawa na asilimia 60 yako kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji, mapendekezo 13 sawa na asilimia 24 hayajatekelezwa kabisa na pendekezo 1 sawa na asilimia 2 limepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom