Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Taarifa za Habari Leo Usiku zilihanaikizwa na mgomo wa Wafanyakazi wa Kiwanda cha Viatu Bora ambao kufuatia ziara ya Waziri wa Kazi na Ajira Kiwandani hapo aliagiza wafanyakazi wote wasio na Mikataba wapewe Mikataba ndani ya siku 14.
Wafanyakazi hao wamegoma baada ya siku hizo kupita huku kukiwa hakuna dalili ya utekelezwaji wa agizo hilo huku meneja wa Mauzo akijinasibu kwamba wako katika hatua za mwisho kutekelea ilihali siku zilishapita
Sanjari na hilo, kumegubikwa na sintofahamu ya kuanza kwa mradi wa mabasi ya kasi ambao Waziri mwenye dhamana aliagiza uanze ifikapo Januari 10 na leo ni J anuari 13.
Huenda yapo maagizo mengi mengine lakini kwangu nayaona ni maagizo yaliyoongozwa na mihemuko, sifa na kujionesha zaidi badala ya kuzingatia uhalisia. Wakati haya yaliyokishatolewa hayajatekelezwa, mawaziri wanaendelea kutoa maagizo mengine, hali inayonifanya niamni kwamba huenda hata yale ya awali wameyasahau huku wakiwaacha watu kuwa wahanga kwani wafanyakazi hao waliogoma utasikia wametimuliwa badala ya kupewa hiyo mikataba.
Ningewaomba mawaziri wetu watulie na kuwa na mikakati madhubuti ya kushughulikia kero mbalimbali nchini badala ya hii ya zimamoto.