Utekelezaji wa kuwa na maji ya kunawia naona lipo kisiasa

Luhungu

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
814
250
Habari wadau,

Naandika kiasi kidogo tu, kusemea kile ninacho kiona dhidi ya utekelezaji wa agizo la kunawa ama kuwa na maji ya kunawa katika maeneo yenye misongamano mfano, stendi za magari nk.

Nipo hapa Msamvu, Kituo kikuu cha magari ya mikoani. Ukweli nawapongeza wamiliki wa magari kwa angalau kujaribu kujitahidi kuwa na maji.

Ajabu na hoja yangu ni kuwa, kiasi cha maji kinavyo tolewa, naona ndiyo IMEKUWA MSINGI WA HOJA YANGU HAPA.

Kila gari naona wamenunu zile 'spray cane' na wameweka maji yaliyochanganywa na OMO. Abiria ukiingia tu unapuliziwa vijimatone kiasi mkononi na unaendelea na shughuli yako.

Kwa waliofanikiwa kuingia ndani bila kumkuta 'mpiga debe aliyepewa jukumu la kupulizia', ndiyo inakuwa imetoka.

Kwa mtizamo huu, naona, wamiliki hawa, wanachukulia issue hii ni ya kisiasa, na wameona acha nwanaharamu apite.
Hata mlango mkuu wa kuingilia kituoni, utaratibu ni huo huo.

Nadhani, hata viongozi wa stendi wamehalalisha na wanaona acha liwe. Natoa ushauri, jambo hili liangaliwe.

Kwa hadhi ya MSAMVU, hapa ni kituo ambapo ni makutano ya magari toka nchi mbalimbali, mf, Zambia, Uganda, Rwanda nk. Na kwa taarifa, nchi hizi zote zishapatwa na maambukizi kama sisi.

Nilidhani ingalikuwepo haja ya kupima hata joto la mwili la tunaoingia na kutoka, sambamba na maji ya kunyunyiziana haya.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom