Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Kuna suala hua linaniumiza kichwa nikiwa najiuliza kila wakati juu ya viongozi kuwa wakweli ktk kutaja mali walizonazo.serikali imekua ikilifumbia macho jambo hili huku uchumi ukididimia pasi na sababu za wazi.

Viongozi wamekua na tabia ya kujilimbikizia mali wao na familia zao bila kujali hali duni ya wananchi masikini ktk kuwezeshwa.

Wamekua waongo pindi waombapo kura huku wakitoa ahadi hewa pasi nakujali athari zitakazojitokeza.matokeo yake mnaaambiwa serikali haina pesa,tuna madeni mengi ya nchi za nje,mara hivi mara vile.

Ukienda kununua shamba utaambiawa eneo lote hili la hekari 300 ni la kigogo fulani, mtu anaamua tu kuzuia ardhi kubwa bila kuwafikiria wananchi wake wanyonge.muda ukiisha wa uongozi anaanza tena kampeni za ulaghai ilimuradi kuharibu fikra za wanachi.

Suala hili lazima liangaliwe kwa kina, viongozi lazima watoe habarai sahihi juu ya mali wazimilikizo na sio blablah wanatukatisha tamaa.
 
Last edited by a moderator:
Swala la viongozi na kutaja mali zao lina lengo gani hasa?.. maanake sio viongozi wataje mali zao wakati hakuna malengo hasaya zoezi zima zaidi ya kujua nani ana kitu gani!

Nadhani Huyo Mkapa pamoja na kutaja majumba yake yote je, aliyajenga wakati gani na hizi mali zote alizojilimbikiza zilikuwepo ktk malipo yake ya kodi kwa mwaka unaohusika?

Maana unaweza kumkuta mtu kasema ana nyumba mbili lakini nyumba hizo zina thamani zaidi ya dollar laki tatu na mwingine nyumba kumi lakini hazifiki hata laki moja! Kinachohesabika kiuchumi na hasa kodi zake ni thamani ya hizo mali. Laa sivyo tuwe na malengo mengine kabisa kama vile kupitia mizani ya mishahara yao na upatikanaji wa mali hizo, jambo ambalo sidhani kama linaweza tokea kwani hakuna sheria wala tume inayoshughulikia Rushwa ama utajiri wa wizi kwa miaka ya nyuma. Tumeanza kuzuia sasa hivi kwenda mbele... huko nyuma aliyekwisha chuma kachuma...ndio sera mpya. Hapa haki iko wapi?

Mimi nadhani kuna haja ya ofisi ya ushuru kama sio hiyo tume ya kuzuia rushwa wao wafuatilie zaidi kodi za hao viongozi kama walivyofanya kwa wafanyabiashara wakati wa Mkapa.
 
NDugu zangu hilo ni zoezi la wakomunisti,tukiana kumcambua kila mtu basi huo ndio utakuwa mwanzo wa mfarakano kwa taifa letu changa.Kumbukeni zoezihilo lilianznzishwa na Sokoine na lilileta matatizo makubwa sana nchini,hizo ni politicsza kukomoana na fitna tupu.kumbukeni serikali yetu inasheria na ni vyema tungefuatilia sheria ,kama kinogozi kavunja sheria kujipatia mali basi sheria itumike mara moja hao wako wengi sana ,watu kama aliyekuwa waziri muu Mr Sumaye ni miongoni mwa wavunjaji wa shria na wamejilimbikizia mali kwa taratibu chafu sana na zinaeleweka na kila mtu hapa.Naomba tuzingatie sheria kabla ya kutoa ushauri mwingine.

peace!!!!!
 
Willo,
Zoezi kama hili sio Ukomunist hata kidogo isipokuwa kuwepo na malengo ya kuendesha zoezi kama hili ndio muhimu. Sheria husimama pale wanasheria wana sauti kusimamisha mashtaka.. TZ hakuna sheria isipokuwa ile ya kesi za jinai, vibaka, wabinjukaji na wale wa ofisini ambao hesabu hazikubaliani.

Maelezo yako yote yame -base kwenye nchi za magharibi ambako wao system yao tayari hairuhusu kabisa vitendo kama hivi na wala kingozi wa serikali hawezi kuwa mfanyabiashara kwa wakati mmoja... lini ataweza kulitumikia taifa?..Sisi tumeshindwa kabisa kutofautisha kati ya kiongozi ndani ya chama na yule wa serikali. Kiongozi wa ngazi ya juu CCM anayo sauti kubwa kuliko kiongozi yeyote nje...hata kama mtu huyo akistaafu kazi serikalini bado chama kitamlinda kwa hali na mali.

Kwa hiyo zoezi lolote lile huendeshwa pale sheria iliposhindwa na huyo Sumaye asingeweza kujilimbikiza mali zote hizo kama sheria imesimama na imechukua mkondo wake. Ni kweli zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa na sababu kubwa ni kwamba hakuna sheria zaidi ya sheria hizo kuwa vitabuni ndani ya makabati.

Zoezi la Sokoine - fagio la chuma halikuwa na matatizo kwa raia ila haohao viongozi ambao walikuwa above the law. Je, kuna mbinu gani zaidi kuhakikisha viongozi hawana sauti zaidi ya sheria hasa ktk nchi ambayo imefuata sera ya Chukua Chako Mapema....
 
Habari za Kitaifa Habari nyingine zaidi!
Wabunge wachenga kutangaza mali zao
Joyce Macha
HabariLeo; Friday,January 12, 2007 @00:08

WABUNGE 96, hadi jana walikuwa hawajawasilisha fomu zinazowataka kuainisha mali na madeni yao, katika Ofisi za Bunge na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imefahamika. Kama sheria itachukua mkondo wake, wabunge hao wako hatarini kupoteza wadhifa huo kwa kushindwa kutekeleza masharti hayo.

Akizungumza na HabariLeo Dar es Salaam, Katibu wa Bunge, Damiani Foka alisema hadi jana wabunge 224 kati ya 320 ndiyo waliokuwa wamekwisha kurejesha fomu katika ofisi hizo. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ilikuwa ni Jumapili ya Desemba 31, mwaka jana.

Foka alieleza kuwa kama kifungu cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kikichukua mkondo wake wabunge hao watapoteza nafasi zao za kuendelea kuwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Katiba ya nchi, ibara ya 70 na 71 zinaelezea masharti yanayowabana wabunge watakaposhindwa kurudisha fomu kwa muda uliopangwa. “Ibara ya 70 ya Katiba hiyo hiyo inamtaka kila kiongozi wa umma wa ngazi yoyote kujaza fomu hizo kuainisha mali na madeni aliyonayo na kuzirudisha sehemu husika, iwe hapa Bunge, kwa Spika au Tume.

“Lakini pia ibara ya 71 inasema kama kiongozi yeyote atashindwa kurudisha fomu hizo kwa wakati uliopangwa basi kiongozi huyo atakuwa amejivua wadhifa huo mwenyewe,” alisema Foka. Foka alieleza pia kuwa Sheria inaruhusu watu kuendelea kurudisha fomu hata kama muda unaotakiwa umepita ila ni lazima waambatanishe maelezo ya kwa nini walichelewa kuzirejesha.

“Unajua hatuwezi kusema sheria ichukue mkondo wake moja kwa moja maana unaweza kukuta kiongozi mwingine ni mgonjwa au amesafiri nje ya nchi kikazi ndiyo mana tunawapa nafasi ya kutoa maelezo,” alisema Foka.

Foka alisema hajapokea taarifa yoyote ya udhuru wa ugonjwa au safari kutoka kwa Mbunge yeyote hivi karibuni. Alisema kuwa utaratibu unaofuata sasa ni kuangalia viwango vya mshahara na marupurupu ya kila kiongozi wa umma na kulinganisha na mali anazozimiliki.

“Tunachukua hatua hii ya kuoanisha mali na mshahara wa kila kiongozi tuweze kufahamu uhalali wa umiliki wa hizo mali kwa kila kiongozi ili kubaini kama wanajihusisha na vitendo vya rushwa. “Ndiyo maana kila kiongozi anatakiwa kutaja bila kudanganya kila mali anayomiliki hata kama ni baiskeli na kama anaendesha biashara yoyote kwa kuchukua mkopo benki basi anatakiwa kuzitaja hizo benki ili tume ifuatilie na kujua uhalali,” alieleza Foka.

Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kama mtu hajarudisha fomu kwa muda uliopagwa sheria ipo na itachukua mkondo wake.

“Mimi sina la kusema maana hiyo sheria inanibana hata mimi nisiporudisha. Bahati nzuri nimesharudisha kwa hiyo Tume ya Maadili ndiyo inayoshughulikia hii sheria kwa hiyo huu ndiyo muda wake wa kuifanyia kazi sheria hiyo.




SASA TUONE YATAKAYOTOKEA
 
Hao ni lazima wawe ni CCM maana kama ni wapinzani tungalisikia Kamati inaundwa wajieleze ama habari za wao kuwa wamejifuta . Fomu tu inachukua muda gani ? Naamini na Lowasa hajarudisha maana duh!!!
 
Wanasiasa wetu 4,000 waamua KUKIUKA KATIBA ya JMT kwa kukwepa kutaja mali zao
Joyce Macha
HabariLeo; Friday,January 26, 2007 @00:06


VIONGOZI wengi nchini hawajarejesha fomu zinazotaja mali na madeni yao, kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imefahamika.

Katibu Kiongozi wa Siasa, katika tume hiyo, Fredrick Mandara, amesema kati ya viongozi 6,241 nchini wanaotakiwa kurejesha fomu zao ni 2,493 waliofanya hivyo katika muda uliopangwa na serikali. Viongozi 3,748 ndiyo wanasuasua kurudisha fomu hizo na hadi sasa hawajatoa taarifa au sababu za kushindwa kiziwasilisha, alisema.

Mandara aliwataja viongozi wa umma wanaohusishwa na sheria hiyo kuwa ni Mawaziri na Manaibu wake,Wabunge, Makatibu Wakuu, Madiwani,Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri za Miji, Manispaa, Wilaya, Majaji na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma.

Viongozi hao wanatakiwa kujaza na kurejesha fomu hizo kila mwaka na kwa mwaka jana mwisho wa kurejesha fomu hizo ilikuwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, Mandara aliiambia HabariLeo kuwa mgongano wa Katiba na Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma unatoa mwanya kwa viongozi wa Serikali kugomea kutaja mali na madeni yao. Alisema Sheria ya Tume ya Maadili, kifungu cha 15 (a) cha Sheria Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya Mwaka 1995 inasema kama kiongozi yeyote wa umma atashindwa kurudisha fomu bila sababu za msingi kwa muda uliopangwa atahesabiwa kwa kosa la kukiuka maadili.

Lakini Mandara alisema sheria hiyo haikutungwa kwa nia ya kuwaadhibu viongozi wa umma bali kuhakikisha viongozi hao wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kiwango cha juu ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali . Alisema kuwa adhabu za ukiukwaji wa maadili zilizoainishwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 zitachukuliwa iwapo kiongozi amechunguzwa na kuthibitika kuwa amekiuka maadili.

Wakati Sheria ya Tume hiyo inakana kuwapo kwa adhabu, kiongozi anaposhindwa kurudisha fomu, Katiba ya nchi ibara za 70 na 71 zinaelezea masharti yanayowabana viongozi wanakaposhindwa kurudisha fomu kwa muda uliopangwa.

Ibara ya 70 ya Katiba hiyo inamtaka “kila kiongozi wa umma wa ngazi yoyote kujaza fomu hizi ili kuainisha mali na madeni aliyonayo na kuzirudisha sehemu husika, iwe hapa Bunge, kwa Spika au Tume kwa wakati.” Nayo ibara ya 71 inasema, “kama kiongozi yeyote atashindwa kurudisha fomu hizi kwa wakati uliopangwa basi kiongozi huyo atakuwa amejivua wadhifa huo mwenyewe.”

Mandara alisema tangu kutungwa kwa Sheria ya Maadili hakuna kiongozi yeyote wa umma aliyewahi kuadhibiwa kwa kukiuka kurudisha fomu au udanganyifu wa mali alizonazo. Hata hivyo, Mandara alisema kuwa ingawa muda wa viongozi kurudisha fomu hizo umeshapita hatua zinazofuata sasa ni kuwaandikia barua za kuwakumbusha.

Pamoja na hayo habari nyingine zinasema licha ya Katiba kuainisha adhabu, viongozi wanaruhusiwa kuendelea kurudisha fomu hata kama muda umepita ila ni lazima waziwasilishe fomu hizo zikiwa zimeambatana na maelezo ya kwa nini hawakurudisha kama ilivyotakiwa.
 
Inashangaza Bw. Mandara kulinganisha sheria ya Maadili na Katiba ya Nchi. Sheria yoyote inayotungwa inapopingana na Katiba Sheria hiyo imetanguka! Katiba inasema viongozi wasiorudisha fomu hizo kwa muda uliotakiwa "wamejivua wadhifa wao"... Hapo hakuna mjadala Katiba inasimama na sheria nyingine yoyote inatengekuka. Hiyo hatua ya kuandika barua ya kuwakumbusha iko wapi kwenye hiyo sheria na barua ngapi zinaandikwa kabla Katiba haijatiiwa!

Kwa ufupi ni kuwa viongozi ambao hawajaripoti mali zao kwa tume ya maadili kwa mujibu wa Katiba, hawastahili kurudi ofisini Jumatatu!!!! now lets some heads start rolling!!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliapishwa kuilinda katiba, sasa hawa viongozi wameshindwa kutekeleza yale yaliyo kwenye katiba inabidi rais ailinde KATIBA tena haraka sana. HEADS MUST ROLE!!!!

RAIS KUKAA KIMYA KUNA MAANISHA NINI, AMESHINDWA KAZI?
 
Inaudhi pale wale wote walioapa kuilinda Katiba wamekaa kimya.. Kama kuna mtu ana uwezo (Mtikila najua ana uwezo) aende mahakamani kufungua kesi ya Kikatiba kuwataka viongozi wote ambao hawajatii matakwa ya Katiba wasirudi kazini hadi wathibitishe kwanini wanadhani wao wanaweza kukaidi Katiba.

Kwa mara ya kwanza can we fire everybody ya hao elfu nne na waone kama nafasi zao zinajazika au la!.. Mr. President.. just this one time unless na wewe hujatangaza mali zako...!!
 
Nd. Mwanakijiji, unataka President ajifukuze kazi mwenyewe?
Sidhani kama ametangaza mali zake!
Aliyesikia atuume sikio basi!
 
yule mama wa Liberia alipoingia kazini alifukuza watumishi wote wa idara ya mapato! that was a statement.. na kuanzia hapo watu walijua hana mchezo.. Kama Rais mwenyewe hajatangaza mali zake.. then we have a bigger problem than I originally thought.
 
Yeah, Mh Rais na cabinet yake inabidi watangaze mali zao!
Ningependa kufahamu mali za Richmonduli!
Huyu jamaa inawezekana akawa amekosa sifa za kuwa mwanachama wa CCM kutokana na katiba kama nilivyosoma kwenye file ulilotupa nd. mwanakijiji
 
Brutus,
You got a point. Hatujamsikia rais akitangaza ana mali gani. Mkapa naye kaondoka bila kutuambia amekusanya mali ngapi. Let's wait and see.
 
Hii tume ya maadili nayo ni joke!
Hivi iliundwa ikusanye takwimu au ihakikishe maadili ya uongozi yanafuatwa or otherwise?
Hizi tume zisizokuwa na meno ya kung'ata zinatulostisha!
 

Hata hivyo, Mandara aliiambia HabariLeo kuwa mgongano wa Katiba na Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma unatoa mwanya kwa viongozi wa Serikali kugomea kutaja mali na madeni yao. Alisema Sheria ya Tume ya Maadili, kifungu cha 15 (a) cha Sheria Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya Mwaka 1995 inasema kama kiongozi yeyote wa umma atashindwa kurudisha fomu bila sababu za msingi kwa muda uliopangwa atahesabiwa kwa kosa la kukiuka maadili.

Lakini Mandara alisema sheria hiyo haikutungwa kwa nia ya kuwaadhibu viongozi wa umma bali kuhakikisha viongozi hao wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kiwango cha juu ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali . Alisema kuwa adhabu za ukiukwaji wa maadili zilizoainishwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 zitachukuliwa iwapo kiongozi amechunguzwa na kuthibitika kuwa amekiuka maadili.

Wakati Sheria ya Tume hiyo inakana kuwapo kwa adhabu, kiongozi anaposhindwa kurudisha fomu, Katiba ya nchi ibara za 70 na 71 zinaelezea masharti yanayowabana viongozi wanakaposhindwa kurudisha fomu kwa muda uliopangwa.

Ibara ya 70 ya Katiba hiyo inamtaka “kila kiongozi wa umma wa ngazi yoyote kujaza fomu hizi ili kuainisha mali na madeni aliyonayo na kuzirudisha sehemu husika, iwe hapa Bunge, kwa Spika au Tume kwa wakati.” Nayo ibara ya 71 inasema, “kama kiongozi yeyote atashindwa kurudisha fomu hizi kwa wakati uliopangwa basi kiongozi huyo atakuwa amejivua wadhifa huo mwenyewe.”

Mandara alisema tangu kutungwa kwa Sheria ya Maadili hakuna kiongozi yeyote wa umma aliyewahi kuadhibiwa kwa kukiuka kurudisha fomu au udanganyifu wa mali alizonazo. Hata hivyo, Mandara alisema kuwa ingawa muda wa viongozi kurudisha fomu hizo umeshapita hatua zinazofuata sasa ni kuwaandikia barua za kuwakumbusha.

Hivi huyu Mandara ni Mwanasheria? Kati ya Katiba na hiyo sheria iliyotungwa ni kipi kinapaswa kutiiwa.

Ibara 64:5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi:
(5) Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.
(Msisitizo wangu)

Sheria ya maadili ya viongozi kifungu cha 15 (a) cha Sheria Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya Mwaka 1995 ambapo haitoi adhabu kwa kiongozi ambaye hataki kutangaza mali yake au amepitisha muda kutangaza mali zake, kinapingana kwa sehemu na moja kwa moja na kifungu cha katiba cha 70 kinachoweka ulazima kwa viongozi kutangaza mali zao na kifungu cha Ibara 71:1(g) kinachoelezea kuwa mtu atapoteza nafasi yake ya Ubunge endapo
atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
Zaidi ya yote, Kwa mujibu wa Katiba ya JMT, sheria ya Maadili itakapotungwa "itafafanua adhabu inazoweza kutolewa kwa kuvunja misingi ya maadili;" Hivyo kwa sheria hiyo kutokuanisha adhabu basi inapingana na kifungu cha Katiba cha 132:5(d)

sasa, wabunge wote ambao hawajatangaza mali zao hawatakiwi Bungeni wiki ijayo. Kama kuna wapinzani hapa wachangamkie kufungua kesi ya Kikatiba!!
 
This could be one of the best questions to be asked to JK.

Watakaokuwepo mkutanoni hiyo february, take note ya hivyo vifungu alivyoweka Mwanakijiji.
 
Kulikoni, kama wanataka kuharibu sherehe za CCM ni kwenda Mahakamani na kuhakikisha kuwa wabunge wote ambao hawajatangaza mali zao hawaruhusiwi kuingia bungeni kwani wamepoteza sifa za kuwa Wabunge. Spika atakiwe kutangaza kuwa viti hivyo viko wazi na kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo kianze.

This is a slam dunk... CCM wamezoea kufanya mambo kwa kujipendelea lakini hapa waswahili wanasema "Papa mkaange kwa mafuta yake".. Katiba wameandika wao, na sheria ya maadili wametunga wao.. sasa itumike kuwakaangia!!!
 
Mwanakijiji,

Hivi hii haiwezi kwenda bungeni kama hoja binafsi?

Kama sisiemu hawawezi kuipeleka .. si ndio nafasi hii kwa wabunge wa CUF, Chadema etc? (well, assuming wao wamerudisha fomu!)
 
Back
Top Bottom