Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma

MKJJ,
Wanasemaje hao wanene kuhusu "viongozi wasipotangaza mali zao wakati wanatoka madarakani?" Sheria inasemaje? Tume imewafuatilia kwa mfano, viongozi waliokuwa katika awamu iliyopita, kina BM na FS,na wengine?
 
JK aonyeshe jinsi anayoilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala hili.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta azungumza na KLH News kuhusu baadhi ya viongozi hususan Wabunge ambao wanatakiwa kurudisha fomu za kutangaza mali na madeni yao kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Mhe. Sitta anaeleza ni wabunge wangapi mpaka sasa wameshafanya hivyo na nini kifanyike kwa wale viongozi wasiofanya hivyo.
 
Wakati umefika kuweka mali za viongozi wetu walizo kuwa nazo kabla ya kuingia madarakani na wakati wakutoka madarakani kutoa uwiano wa mali na muda aliyokuwa madarakani, ilituweze kupunguza mianya ya 10% na rushwa iliyo enea kila mahali nchini,

katika topic hii unaandika mali unazo HISI kuwa ni za kiongozi fulani na baadaye kufanyiwa kazi kama unahisi andika mali hizi nina hisi hazina uwakika ili tujue na kuzitafutia ushaidi, na wamiliki halali.

sehemu hii itasaidia serikali kwa wale ambao walidanganya idadi ya mali walizo nazo.

taja aina ya mali au biashara unazo fikiri ni za kiongozi usika ,kama unahisi wewe andika na unote kwamba nina hisi .sisi tutazifanyia kazi.

komesha rushwa za 10% na nyingine za 30% na kwenda juu
 
kweli nimeamini wanaJF wanauchungu na mali zao na pesa zao za kodi kweli muda umefika kuwaanika viongozi wetu hawakujua kama kuna kitu kama hichi utandawazi na tukiwaandika tu basi wengine wata kufa na stroke hili nina waambia nikweli na mtasikia wakati wakila rushwa na kupeleka watoto wao ulaya na wakiugua wanatibiwa nje sasa itawatokea puani.

wanaJF msilale kwahili ili waje hapa kujibu tuhuma zao za rushwa mimi nina sema andikeni sana tu kila kitu mpaka vilivyo andakwa majina ya watu wengine , huu utakuwa msaada mkubwa sana kwa srikali hii ya JK,

WALETENI TUJUE WANATUNYANYASA SANA HUKO MITAANI NA MAJUMBA NA MAGARI KUMBE NI DAMU ZA WALALAHOI WAVUJA JASHO.
 
Mhh sidhani kama hili litawezekana...maana karibu kila mali itakayotajwa humu itakuwa na neno NAHISI...kama huna nakala/copy ya hati miliki ya mali iliyo mashakani yenye jina la mtuhumiwa/kiongozi then utakuwa UNAHISI. Kitu ambacho sidhani kama watu humu na wengine huko nje watakichukulia kwa umakini. Itapelekea kuombana ushahidi kupita kiasi...!!

Huo ndio wasiwasi wangu lakini kwa mtazamo wa juu juu hili wazo limetulia.
 
Yebo yebo

ondoa shaka, jamboforum inahazina ya vichwa, wewe kama unahisi mwaga data watu watafuatilia na ukeli utabainika.

wanabodi inatubidi twende mbali kidogo, tusiangalie mali zisizoamishika tu, tuangalie pia pesa zinazowekezwa kwenye elimu ya watoto wao, mimi hainiingi akilini kabisa kwa mfanyakazi wa serilkali au taasisi ya serikali kusomesha zaidi ya watoto watu nje ya nchi, pesa hizi zatoka wapi?

Ninahakika jamboforum itaandika historia ya nchi hii ....
 
ili kazi hii iwe na mafanikio napendekeza uchuguzi huu ufanyike kwa mafungu, tuangalie zile sehemu zilizoumiza sana uchumi wetu, alafu wale wahusika wote wa karibu tuwamulike.

mfano
1. wahusika wa mkataba wa IPTL
2. wahusika wa mikataba ya madini
3. wakuu wa polisi
4. mawaziri .............

majina ya watu hawa yatajwe hapa mmoja paada ya mmoja, kisha wanabodi wamwage data
 
Mh! nasita kuhusu mali za ku-HISI.

If we are honest with ourselves we will admit that wa-TZ kwa kuzusha hawajambo. Ukimuuliza mtu kitu hiki ni cha nani hatakawia kukwambia ni cha fulani simply kwasababu alimuona hapo, au aliambiwa.

Kama tunataka kufanya mambo kiutu-uzima please tusiandike kitu ambacho hata circumstancial evidence yake ni doubtful. Kama una taarifa fulani jaribu kupima ukweli/uwezekano/mazingira yake; piga picha ukiweza, leta hapa JF kama kuna mwenye taarifa tofauti aitoe.

Cha msingi tusikurupuke maana kuna hata mitaa imepewa majina ya viongozi fulani kwa kuhisiwa wana nyumba huko wakati ukweli ni kuwa hawana hata kiwanja hapo.

Sitetei wabadhirifu ila naona hatari ya ku-act on pure speculations and rumours, of which wabongo wengi wamebobea.
 
Mh! nasita kuhusu mali za ku-HISI.

If we are honest with ourselves we will admit that wa-TZ kwa kuzusha hawajambo. Ukimuuliza mtu kitu hiki ni cha nani hatakawia kukwambia ni cha fulani simply kwasababu alimuona hapo, au aliambiwa.

Kama tunataka kufanya mambo kiutu-uzima please tusiandike kitu ambacho hata circumstancial evidence yake ni doubtful. Kama una taarifa fulani jaribu kupima ukweli/uwezekano/mazingira yake; piga picha ukiweza, leta hapa JF kama kuna mwenye taarifa tofauti aitoe.

Cha msingi tusikurupuke maana kuna hata mitaa imepewa majina ya viongozi fulani kwa kuhisiwa wana nyumba huko wakati ukweli ni kuwa hawana hata kiwanja hapo.

Sitetei wabadhirifu ila naona hatari ya ku-act on pure speculations and rumours, of which wabongo wengi wamebobea.


Mwendapole, Good point...
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi na hatutaji mali zetu pasukeni na Nchi tutaila tunavyo taka . Tutaiba kura, tuana Majeshi ,tuna usalama na tuta hakikisha tunabaki madarakani for ages to come .

Mnasemaje ?Msitake kutuumbua wananchi wakose imani zaidi na sisi maana tayari hawana imani na ndugu JK na papara zake .
 
Nafikiri pa kuanzia ni kwa BWM, hebu tuanze na zile nyumba zake Tanga na South Afrika maana hili liliongelewa sana kwenye mada zetu kwa hiyo wenye picha watubandikie hapa.
 
Kingunge Ngombale Mwiru na Huduma za parks Dar kuna unyanyasaji mkubwa .
 
Haha, Mzeeshughuli Bwana!!!

Hilo ni bonge la deal kwa Kingunge na hawezi kuongeleka. Huyu ni LULU ya sirikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Inshallah... Tutafika
 
Mimi nina waunga mkono wote waliotangulia hii topick itawaleta watanzania wote hapa jamboforums, wakiwemo viongozi, wafanyabiashara , wanafunzi shule mbalimbali na wa vyuo vikuu , iliwajuwe viongozi wao wanafanya nini

na pesa yao, wanavyoishi vizuri wakati wananchi wanakufa hata dawa hospitalini hawana , jinsi watu wanavyo lindana, nafasi za kazi zinapotangazwa kumbe mtu ameshapewa, jinsi ambavyo wananchi wanatumika kama ''condom''

Samahani kwa lugha niliyo tumia , watu wajuwe, haswa watu wa TRA,POLICE,MAHAKAMANI,WIZARA MBALIMBALI, TENDER ZA SERIKALI, WAKURUGENZI WA WILAYA, MAWAZIRI, jamani kulindana lazima tuukomeshe

Kama ulisha wai kuomba kazi mahali popote ukanyimwa kwa makusudi kwa sababu kulikuwa na mtu wao akapewa karibu hapa ndugu yangu,sema ukweli kwasababu hiyo nafasi hakuna tena, toboa lijulijake hapa ndiyo sehemu yako ya mwisho wewe kusikika mtanzania wa leo.
 
Sasa kama hawezi kuongeleka hapa tuseme kwa uwazi . Lulu kivipi mbona kidogo umenishangaza ? Ina maana bila yeye Chama kile hakipo ?
 
Sasa kama hawezi kuongeleka hapa tuseme kwa uwazi . Lulu kivipi mbona kidogo umenishangaza ? Ina maana bila yeye Chama kile hakipo ?


Na ndo lengo letu!

Ukitaka kujua mambo haya unaweza kupata wazimu! Kingunge umuhimu wake ndani ya CCM anaujua FD...

Lakini hivi unajua wife wake ndo anamiliki kampuni moja kubwa ya kuzoa taka na kusafisha jiji pia?

Na bado... Kuna wengi wanajua mengi hapa...
 
Hii kampuni inaitwaje ? Tafadhali nifungue masikio niweze kutajua haya maana duh kazi kubwa hii .
 
Kunanyumba 13 zinajengwa kwa pamoja zenye gorofa moja moja anaye zisimamia ni mfanyabiashara maharufu wa madini ya aina ya Tanzanite, anye miliki hotel moja inaitwa SINKA COURT HOTEL,jina la huyo mmasai ni BW.KANUNGA
ziko IGM HOLDINGS ESTATE

Ndiye mwenye pesa nyingi kwenye bank ya standard charter tawi la Arusha alisha wai kuzawadiwa TOYOTA LAND CRUSER PICK kwa sababu ya kutochukuwa pesa bank ni kuweka tu,

nikatika watu walio toa pesa nyingi wakati wakampeni ya CCM na EL kushinda ubunge wilaya ya MONDOLI,
ninaomba hili lifuatiliwe kwa makini.

Maana ya PIG ni Private Intelligence Group ya Tanzania

nitaieleza kwa kirefu baadaye.

nikama Ninja ya marekani AU shirika linalo shughulikia suala la RADA UK.

habari hizi zimefika mezani kwetu baada ya kujua huu mtandao Kuutumia kwa mafanikio makubwa sana tumeamua kuweka wazi kwamba tupo pamoja na nyiye na tutajitamblisha rasimu hapa JF

KAZI ZETU SIYO ZA SIRI KAMA UNAVYO ONA NCHI NYINGINE PIA TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU BADO HATUJA JIPANUA NCHINI KOTE KWA SABABU YA KIFEZA KWASASA TUNATUMIA TEKINOLOJIA HII YA HABARI NA MAWASILIANO .
kikundi cha kirai cha kuzuia ufisadi

email to: pigfile@gmail.com
 
Back
Top Bottom