Utekaji nyara wa vibinti na ubakaji ukalitikisa taifa la Ubelgiji………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utekaji nyara wa vibinti na ubakaji ukalitikisa taifa la Ubelgiji………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 24, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  2646-437.jpg
  Dutroux
  2_3_Julie_Lejeunes_victim.jpg
  Julie Lejeunes mhanga
  2_4_Melissa_Russo_victim.jpg
  Melissa Russo
  E-JULI~1.JPG
  Julie na Melissa
  wbsabine_narrowweb__200x270,1.jpg
  Sabine Dardenne
  194849-marc-dutroux-ete-condamne-juin.jpg
  Dutroux akiwa mahakamani
  2_5_Eefje_Lambreks_An_Marchal.jpg

  An Marchal na Eerfje Lambrechts
  2_6_Michel_Lelievre_headshot.jpg
  Michel Lelievre
  2_7_Bernard_Weinstein_victim.jpg
  Bernard Weinstein
  2_8_Jean-Michel_Nihoul_mugshot.jpg
  Jean Michel Nihoul

  Mnamo Agosti 9, 1996 mchana mtoto aitwae Laetitia Delhez aliyekuwa na umri wa miaka 14 wakati huo, alikuwa akitembea peke yake kurejea nyumbani akitokea kwenye bwawa la kuogelea, katika mji aliokuwa akiishi na wazazi wake wa Bertrix uliopa nchini Ubelgiji. Lakini Laetitia hakurejea nyumbani, alitoweka katika mazingira ya kutatanisha. Wazazi wa Laetitia walitoa taarifa haraka sana Polisi na pia waliomba msaada kupitia vyombo vya habari kama kuna mtu mwenye taarifa ya mahali alipo mtoto wao awajulishe au atoe taarifa kwenye kituo chochote cha Polisi kilichoko karibu.

  Miongoni mwa simu walizopigiwa, ni simu moja tu iliyopigwa na kijana wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 15 iliyofanikisha kupatikana kwa binti huyo. Kijana huyo alisema kwamba aliona gari moja jeupe likiwa jirani na bwawa la kuogelea, siku ambayo Laetitia alitoweka. Kijana huyo aliendelea kusema kwamba mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi na aliyekuwa akiangalia huku na huko kama vile mtu anayetaka kufanya uhalifu. Pia kijana huyo aliweza kuzikumbuka vizuri namba za gari lile.

  Baadae gari hilo lilikuja kufahamika kuwa ni mali ya mtu aliyefahamika kwa jina la Marc Dutroux aliyekuwa na umri wa miaka 40 wakati huo. Dutroux ambaye ni fundi umeme asiyekuwa na ajira maalum alikuwa na historia ya uhalifu, ubakaji hasa wa watoto wadogo na pia wizi wa magari na uuzaji wa dawa za kulevya.
  Baada ya Polisi kupata taarifa zile walikwenda kuvamia nyumba ya Dutroux iliyopo katika mji wa Marcinelle karibu kabisa na mpaka wa Ufaransa.

  Polisi walifanya upekuzi katika nyumba hiyo lakini hawakuona dalili za mtoto yeyote kufichwa katika nyumba hiyo. Dutroux na mkewe walipelekwa Polisi na kuwekwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa zaidi. Siku mbili baadae tangu awekwe ndani Dutroux alisalimu amri na kukubali kuwapeleka Polisi mahali alipowaficha watoto anaowateka nyara. Kwa maneno yake mwenyewe alisema, 'Nitawapeleka nilipomficha binti huyo'

  Aliapeleka Polisi katika nyumba ile ile ambayo Polisi waliifanyia upekuzi kwa saa 48 bila mafanikio. Alipofika hapo nyumbani kwake aliwapeleka Polisi hadi mahali ambapo alikuwa amejenga chumba ardhini ndani ya nyumba yake. Ndani ya chumba kile hakukutwa Laetitia peke yake bali pia alikutwa binti mwingine aliyekuwa na umri wa miaka 12 aitwae Sabine Dardenne, ambaye alitoweka nyumbani kwao katika kijiji kimoja nchini Ubelgiji kiitwacho Kain miezi mitatu ilioyopita, wakati akiendesha baiskeli nje ya nyumbani kwao.

  Mabinti wale walikutwa wakiwa na hali mbaya sana na wote walikuwa wamenajisiwa. Ndani ya chumba hicho Polisi pia walikuta mkanda wa video unaomuonesha Dutroux akiwanajisi watoto wale wawili pamoja na watoto wengine wawili ambao hawakuweza kufahamika mara moja.
  Dutroux hakuishia hapo, aliwapeleka Polisi katika nyumba yake nyingine ambapo aliwaonesha mahali alipozika miili ya watoto wawili wa kike Melissa Russona Julie Lejeune ambao nao walitoweka majumbani kwao mwaka 1995, pamoja na kuonesha makaburi hayo mawili, lakini pia alionesha kaburi la mtu mmoja aitwae Bernard Weinstein.

  Dutroux alikiri kuwateka mabinti wale wawili na kuwanajisi lakini alikanusha kuwauwa. Kwa mujibu wa maelezo yake alisema kwamba, mabinti wale walipoteza maisha kutokana na njaa wakati yeye alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi minne jela kwa kosa la wizi wa gari. Alikiri kumuachia mshirika wake Bernard Weinstein kiasi cha dola 1,500 ili awahudumie watoto wale kwa chakula wakati yeye akitumikia kifungo, lakini bwana Weinsteinaliifanya kazi ile kwa wiki sita tu kisha akatoweka na kiasi cha pesa kilichobakia.


  Wakati alipotolewa jela, Dutroux alimkuta Melissa ameshakufa na Julie alifariki saa chache baadae, akiwa mikononi mwake. Dutroux alikiri kumtesa kwa kumminya sehemu zake za siri huyo mshirika wake bwana Weinstein hadi akataja mahali alikofisha fedha zilizobakia kisha akamburuza na kumzika akiwa hai. Dutroux aliwaambia Polisi kwamba alimuua Weinstein kwa sababu alishindwa kuwahudumia kwa chakula wale mabinti wawili waliopoteza maisha. Pia aliwaelekeza Polisi mahali pengine alipozika miili ya mabinti wengine wawili, An Marchal aliyekuwa na miaka 19 na Eerfje Lambrechts aliyekuwa na miaka 17.

  Mabinti hao wawili ambao walikuwa ni marafiki walitoweka nyumbani kwao mnamo Agost 1995.
  Picha, mikanda ya video pamoja na nyaraka nyingine zilizokutwa nyumbani kwa Dutroux ziliwafanya Polisi kuamini pasi na shaka kwamba Dutroux alikuwa ni sehemu ya mtandao wa watu wanaohusika na ufanyaji ngono na mabinti wadogo na kisha kuwauza kwa watu wanaomiliki madanguro ya ukahaba barani ulaya. Katika kukusanya ushahidi Polisi waliweza kukusanya mikanda 300 ya video iliyokutwa katika nyumba anazomiliki Dutroux Mikanda hiyo ilikuwa ikimuonyesha Dutroux na mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Martin wakifanya ngono na mabinti wadogo waliowateka nyara.

  Mwendesha mashtaka wa wakati huo Michel Boulet ambaye alipewa jukumu la kuitazama mikanda hiyo kwa ajili ya kupata ushahidi alisema, ‘wote walioonekana kwenye mikanda hiyo watachukuliwa hatua za kisheria'

  Je huyu Marc Dutroux ni nani?

  Historia inaonyesha Dutroux alizaliwa Novemba 6, 1956 jijini Brusels akiwa ni wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto watano wa mzee Victor na mkewe Jeanine ambao walikuwa ni waalimu na ambao anadai walimtesa sana utotoni, hata hivyo wazazi wake walipotengana mwaka 1971 aliondoka nyumbani na kuanza kujitegemea.

  Alimuoa mke wake wa kwanza akiwa na miaka 19 na kujaaliwa kupata watoto wawili wa kiume, hata hivyo ndoa yao haikudumu, kwani mkewe alilazimika kutengana na Dutroux mwaka 1983 na hivyo kumfanya Dutroux aoe nyumba yake ndogo iliyosababisha ndoa yake kuvunjika, mwanamke huyo alijulikana kwa jina la Michelle Martin. Kwa kuwa hakuwa na ajira maalum Dutroux alikuwa na wakati mgumu kuhudumia familia yake ambayo ilikuwa na watoto watatu, lakini hata hivyo alikuwa akipata fedha za kujikimu kutoka serikalini, katika ule mpango wa kuwawezesha watu wasio na ajira na wasiojiweza (State Welfare).

  Pamoja na kupata msaada kutoka serikalini lakini pia alikuwa akijishughulisha na uuzaji wa magari ya wizi katika nchi za Poland na Slovakia, na pia kujihusisha na kuwauza mabinti wadogo kwa wamilikiwa madanguro huko Ulaya. Kutokana na biashara hiyo alimudu kumiliki nyumba saba katika jiji la Brussels nchini humo ambapo baadhi zilikuwa hazikai watu isipokuwa zile ambazo alikuwa akizitumia kuficha mabinti anaowateka nyara kabla ya kuwauza kwa wamiliki wa madanguro.
  Akieleza jinsi biashara hiyo inavyofanyika, Dutroux alisema kwamba kwa kawaida hulipa kiasi cha dola 1,600 kwa kila binti mmoja anayeletwa na mawakala wake na yeye huweauza kwa kiasi cha dola 3,200 na 4,800 kwa kila binti kwenye mtandao wa wafanya ngono na watoto (pedophiles) barani Ulaya.

  Dutroux alianza kuingia matatani mnamo mwaka 1989 baada ya kupatikana na kosa la kuwateka nyara na kuwabaka mabinti watano waliokuwa na umri kati ya miaka12 na 19, Dutroux alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela. Wakati akiendelea kutumikia kifungo, waziri wa sheria wa nchi hiyo wa wakati huo Bwana Wethelet aliagiza wafungwa wote waliohukumiwa kwa makosa ya ubakaji waachiwe huru. Ingawa Dutroux alikuwa amehukumiwa miaka 13 lakini alitumikia miaka mitatu tu akawa amenufaika na msamaha huo wa waziri wa sheria wa kuachiwa huru mnamo mwaka 1992 kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na tabia nzuri huko gerezani. Watu walipohoji kuhusu kuachiwa kwake mapema vile, waziri huyo wa Sheria alisema kwamba Dutroux alitumikia karibu nusu ya kifungo chake kwa sababu aliwekwa ndani kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kuhukumiwa.

  Aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwa sababu kuachiwa kwake kulifanywa na jopo la watu makini wanaohusika na mapendekezo ya kutoa kifungo cha nje (Parole) baada ya mfungwa kuonesha mwenendo mzuri wakati akiwa gerezani. Hata hivyo waziri huyo alisema kwamba ametoa waraka maalum kwenye mamlaka zinazohusika ili Dutroux afuatiliwe kwa karibu. Hata hivyo inasemekana hizo mamlaka zinazohusika hazikufanya kazi yao kama inavyotakiwa, kwani katika kumbukumbu yao inaonesha kwamba, mara ya mwisho kutembelea nyumbani kwa Dutroux ilikuwa ni Julai 1996 na kutoa ripoti kwamba hakuna jambo lisilo la kawaida lililoonekana nyumbani kwa Dutroux. Lakini ukweli ni kwamba wakati Dutroux na mkewe Michelle pamoja na watoto wao watatu wamejenga muonekano kwa watu kwamba, ni familia inayopendana au inayojali watoto, chini ya chumba walichokijenga ardhini, kulikuwa na watoto wengine waliokuwa wakiteswa na kunajisiwa na Dutroux mwenyewe.

  Kilio cha wananchi..............

  Kumbukumbu zinaonesha kwamba mwaka 1993 mshirika mmoja wa Dutroux aliwadokeza Polisi kwamba Dutroux alimwahidi kumpa dola kati ya 3,000 and 5,000 kama akiteka nyara mabinti wadogo na kumpelekea, lakini taarifa hiyo ilipuuzwa. Mwaka 1995 mama yake mwenyewe na Dutroux aliwaandikia Polisi akiwaeleza wasiwasi wake kwamba huenda Mwanae huyo anaficha watoto wa kike anaowateka nyara katika miongoni mwa nyumba zake ambazo hajazipangisha, lakini taarifa hiyo pia ilipuuzwa.Baadae mwaka huo huo wa 1995 yule mshirika wa kwanza kutoa taarifa Polisi aliwaeleza tena Polisi kwamba Dutroux amejenga chumba cha ardhini kwa ajili ya kuwahifadhi mabinti anaowateka nyara kwa ajili ya kuwauza katika nchi za ulaya.

  Safari hii Polisi walitembelea nyumba ya Dutroux ambapo ndipo Melissa na Julie walikuwa wamefichwa, wakati wakiendelea kuwahoji Dutroux na mkewe, Polisi walisikia sauti ya mtoto akilia, lakini mkewe Dutroux, Michelle aliwaeleza Polisi kuwa anayelia ni mwanae ambaye alitoka shule mchana ule akiwa na mafua.
  Hali ya wasiwasi ilizidi kuwa mbaya baada ya wanachi kuchoshwa na jinsi Polisi walivyokuwa wakifanya uchunguzi wa kesi hiyo taratibu mno. Hali hiyo ilisababisha kuzuka minong'ono kwamba, kuna rushwa imetembea ili kumlinda Dutroux, ilisemekana kwamba maafisa wa ngazi za juu wamepkea rushwa ili kuwalinda watuhumiwa ambao ni vigogo wa mtandao huo ambao wengi wapo serikalini wakijihusisha na mtandao wa biashara ya madanguro.

  Wasiwasi ulizidi kuongezeka baada ya Jaji aliyekuwa asikilize kesi hiyo Jean Marc Connerotte kuondolewa kuisikiliza kesi hiyo kwa kile kilichoelezwa kukosa uadilifu, kwani inasemekana Bwana Connerotte alihudhuria chakula cha usiku cha hisani kwa jili ya kukusanya fedha zitakazosaidia familia za wazazi waliopoteza watoto wao au ambao watoto wao waliathirika na vitendo vya Dutroux. Cornnette ambaye alijulikana pia kwa jina la "Little Judge," aliaminika sana kwa kazi yake nzuri aliyoifanya bila kuchoka ya kukusanya ushahidi wa kutosha dhidi ya Dutroux na mtandao wake.

  Connerotte alitaka kuhakikisha anakomesha vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo. Kosa alilofanya Jaji Connerotte ni kukubali mwaliko wa chakula hicho cha hisani ambapo wazazi wa watoto wawili waliotekwa na Dutroux walihudhuria, inaelezwa kwamba haikuwa sahihi kwa Connerotte kuhudhuria chakula hicho cha hisani, lakini hiyo haikuwa ni sababu kwake kuondolewa kusikiliza kesi hiyo. Kitendo cha kuondolewa katika kusikiliza kesi hiyo kulimfanya Jaji Connerotte kuwa shujaa nchini humo.


  Katika hali ya kushangaza ka-nchi haka kadogo ka Ubelgiji kaliingia katika mtikisiko mkubwa, kuanzia Brussels, Antwerp, Ghent na miji mingine midogo midogo nchini humo wafanyakazi walitupa zana zao na kuingia mitaani kupinga jambo hilo. Usafiri wa Treni, pamoja na mabasi yote yalisimamisha huduma, ofisi za serikali nazo zilifungwa. Serikali ya Ubelgiji ilitikiswa na haraka sana Waziri mkuu wa wakati huo Jean Luc Dehaene alitangaza kwamba alikuwa achukue hatua kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika taasisi za kisheria nchini humo, pia aliwahakikishia wananchi kwamba atafanya uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa namna gani shauri hilo la Dutroux lilikuwa limeshughulikiwa.

  Kabla uchunguzi huo haujawekwa hadharani kashfa nyingine ikaibuka makao makuu ya Polisi wilaya ya Charlorei. Mnamo Septemba 10, 1996 askari wa upelelezi walivamia makao makuu hayo na kuwakamata maafisa wa Polisi wapatao 11 miongoni mwa akiwepo Mkuu wa Upelelezi wa wakati huo Georges Zicot. Zicot alishtakiwa kwa kosa la kushirikiana na Dutroux katika wizi wa magari na pia kushiriki katika mtandao wa wahusika wa kufanya mapenzi na mabinti wadogo (Pedophiles)Nchi ya Ujerumani ilikiri kumdokeza Zicot na maafisa wengine kwamba kuna magari mengi ya wizi yamekuwa yakiingizwa nchini humo mengi yakiwa BMW, Porsches na magari mengine ya kifahari lakini taarifa hizo hazikufanyiwa kazi.

  La kuvunda halina ubani............!

  Kama hilo halikutosha, baada ya kamatakamata iliyotokea makao makuu ya polisi ya Charlorei yakaibuka mengine. Kesi iliyopuuzwa siku nyingi ya mauaji ya mwanasiasa machachari na mwanachama maarufu wa chama cha French-Speaking Socialist na naibu waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Andre Cools ilianza kuzungumziwa. Andre Cools aliuawa mwaka 1991, na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kushitakiwa kwa mauaji hayo. Kwa takriban miaka mitano hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa ili kuharakisha upepelezi wa kesi hiyo ya mauaji unakamilika na washitakiwa kufikishwa mahakamani.

  Hata hivyo kulizuka minong'ono kwamba mauaji ya Cools yalitokana na kuibuliwa kwa kashfa za rushwa zilizoikumba serikali hiyo ya Ubelgiji kwenye miaka ya 1980 ambapo inaelezwa kwamba maafisa wengi wa serikali walipokea rushwa kutoka kwa Agusta mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza helikopta nchini Italia. Hata hivyo Agusta amekuwa akikanusha madai hayo mara kwa mara pale yanapoaibuka. Lakini kati ya mwaka 1994 -1995 kashfa hiyo ilipelekea mawaziri wanne wa serikali ya Ubelgiji kujiuzulu akiwemo Katibu mkuu wa Ubelgiji wa NATO Willy Claes, ambaye alipoteza sifa ya kushika nafasi hiyo kutokana na kashfa ya rushwa.

  Mnamo Septemba 12, 1997 wakati taifa hilo liliendelea kupambana na jinamizi la kesi ya Dutroux Polisi katika mji wa Liege hatimaye wakatangaza kukamatwa kwa Alan Van Der Biest pamoja na watu wengine watano akiwemo Polisi mmoja, na wote walifunguliwa mashtaka ya kuhusika na mauaji ya Andre Cools. Van Der Biest waziri wa zamani wa nchi hiyo na mtu maarufu na mwandishi wa vitabu, aliwahi kunukuliwa huko nyuma akikiri kwamba ndiye aliyekodisha walenga shabaha wawili kutoka eneo la Sicilian nchini Italia ili kuja kumuua Cools.

  Van Der Biest aliamuru mauaaji ya Cool ili kuficha kashfa za rushwa zilizokikumba chama cha Socialist kilichokuwa kikitawala nchini humo. Inaaminika kwamba Cools alikuwa afichue kashfa hiyo kama alivyonukuliwa na watu wake wa karibu kabla ya kuuawa kwake, ambapo alikaririwa akisema, "nitaweka kila kitu hadharani na hakika taifa litatikisika, na wote waliohusika na kashfa hiyo nitahakikisha wanashtakiwa"

  Maadui wengi..............!

  Kwa kitendo chake cha kutaka kukomesha vitendo vya rushwa vilivyoikumba serikali ya nchi hiyo, kulimjengea Cools maadui wengi ukilinganisha na marafiki. Wakati wa mazishi ya Cools Mwanae wa kiume aitwae Marcel alinukuliwa akisema, "ni jambo la kuhuzunisha kwamba miongoni mwa waombolezaji waliozunguka kaburi la baba yangu, wapo ambao watalala usingizi mwororo baada ya kifo cha baba yangu." Hata hivyo Marcel alikuwa anaamini kwamba Van Der Biest alihusika na kifo cha baba yake kwa njia moja ama nyingine. "Jambo la kushangaza ni kwamba alishindwa hata kuniangalia machoni wakati wa mazishi ya baba yangu." Alisema Marcel.


  Upelelezi wa mauaji ya Cools ulikuwa ukifanywa taratibu mno na Polisi hawakuichukulia kama ni kesi yenye uzito, hata hivyo baada ya mauaji ya Cools, Polisi walipokea taarifa kutoka kwa mtu asiyejulikana alimtaja Van Der Biest na watu wengine kwamba ndio waliokuwa nyuma ya mauaji ya Cools. Taarifa hizo hazikupewa umuhimu wowote na Polisi.
  Mwendesha mashtaka katika kesi ya mauaji ya Cools na ile ya Dutroux, alidai kwamba kesi hizo hazina uhusiano wowote, lakini ukweli ni kwamba kesi hizo zilikuwa na uhusiano wa dhahiri.

  Kwani kesi hizo zilikuwa na uhusiano na rushwa zilizowahusisha wanasiasa na mtandao wa wahalifu katika eneo linalozungumzwa Kifaransa la Kusini-Mashariki mwa Ubelgiji.
  Baada ukweli wa kesi hiyo ya Cools kujulikana wananchi wa taifa hilo walionesha kutoridhishwa kwao na mwenendo wa Polisi na taasisi ya Sheria nchini humo, ambapo walizituhumu taasisi hizo waziwazi kwamba zimebobea kwa rushwa. Mtu wa kwanza kukumbwa na dhahama ya malalamiko hayo alikuwa ni kiongozi wa upelelezi wa kesi ya Cools, kwani mara baada ya Van Der Biest kukamatwa na kushitakiwa, alijiuzulu.

  Mnamo mwaka 2002 wakati upelelezi wa kesi hiyo ukiendelea Van Der Biest alijiua na mnamo mwaka 2003 shauri hilo lilianza kusikilizwa na watuhumiwa katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa Dereva wa Van Der Biest na mtu wake wa karibu Richard Taxquet na mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Giusseppe "Pino" Di Mauro pamoja na watu wengine walisimama kizimbani kujibu mashtaka ya mauaji ya Andre Cools. Mnamo mwaka 2004, shauri hilo lilisha kusikilizwa na Taxquet na Di Mauro walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

  Ukweli wa kesi ya Dutroux wajulikana........


  Mara baada ya taarifa ya kurasa 300 ya ripoti ya upelelezi wa kesi ya Dutroux kuwekwa hadharani hapo mnamo April 15, 1997. Taarifa hiyo iliweka wazi kwamba kulikuwa na uzembe wa mawasiliano kati ya vitengo vilivyohusika na upelelezi wa kesi hiyo, ambapo hawakuonesha kuipa umuhimu wowote. Taarifa hiyo iliweka hadharani uzembe mwingi wa Polisi katika kushughulikia kesi hiyo ambayo ilivuta hisia za watu wengi sio Ubelgiji pekee hata Nchi za Ulaya na dunia kwa ujumla.
  Kesi hiyo ya Dutroux ambayo ilikuwa ikipigwa kalenda mara kwa mara, ilidaiwa kucheleweshwa kutokana na kusubiri wataalamu wa vipimo wamalize kupima aina za nywele zipatazo 6,000 zilizokusanywa kutoka katika vyumba vya chini ya ardhi vya Dutroux.

  Ni jambo la kushangaza kwamba kesi hiyo ilicheleweshwa kwa takriban miaka 7, kabla ya kufikishwa mahakamani, lakini ikawa imepangwa kusikilizwa rasmi mnamo Marchi 1, 2004. Na pamoja na Dutroux, pia waliunganishwa washitakiwa wengine ambao ni mkewe Dutroux Michelle Martin, aliyekuwa na miaka 45 wakati huo, mfanyabishara Jean-Michel Nihoul miaka 63, na Michel Lelievre.
  Kesi hiyo ilisikilizwa kwa miezi mitatu mfululizo, ambapo waliitwa mashahidi zaidi ya 500.

  Mnamo June 22, 2004, Dutroux alihukumiwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa parole, mkewe Michelle Martin alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, Michel Lelievre alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela, na Michel Nihoul alihukumiwa miaka 5 Jela.


  Kesi hii ilibeba umaarufu mkubwa nchini Ubelgiji kiasi cha zaidi ya robo ya wananchi wa nchi hiyo wenye jina la ubini la "Dutroux" kuomba kisheria kubadili jina hilo eti ili kuepuka mikosi, hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1996 na 1998.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Watakaoona simulizi hii ni ndefu, naomba mniwie radhi, nimejitahidi sana kui-summarize, lakini labda kutokana na uwezo wangu mdogo katika kufanya summary nikaishia hapo.................LOL

  Ni nzuri kuisoma na inaelimisha, lakini pia inahuzunisha.
  Nawatakia siku njema na weekend njema.


   
 3. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu! imenibidi nisinzie, maana ni ndefu sana, inahuzunisha na kusikitisha, ila huyu mke wa Dutroux, nae alilizia mmewe kuwabaka hawa mabinti, au inakuwaje?
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  So sad......
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Poa Kaka,

  Usijali kabisa... Ni story yenye mafunzo muhimu kwa wazazi!

  Babu DC
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,371
  Likes Received: 19,606
  Trophy Points: 280
  usiwe una sumarize sisi wengine tunazisoma hivyo hhivyo mwanzo mwisho
   
 7. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Dah, inasikitisha sana... Yaani kuna watu wara roho za ajabu kweli.
  Halafu mkuu, ningekushauri uache kuwa unawaomba radhi wavivu wa kusoma! Mimi naona ukiomba radhi inakuwa kama umekichakachua kisa chenyewe! Kama mtu hana muda, au ni mvivu wa kusoma kumuomba radhi haimsaidii vyovyote, sanasana tunazidi kulea uzembe... Mbona watu wanatumia masaa kibao baa? Wengine mabuku ya hadithi za Shigongo wanayamaliza bila kujiuliza... Inasikitisha hapa tunapojenga mazoea ya kulea uzembe/uvivu wa kusoma kwa kisingizio cha 'habari hii ni ndefu'.
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapana ndugu,

  Kuna watu tunapenda kusoma tena kuliko unavyodhani ila mara nyingi tunabanwa na majukumu...

  Siyo wote wanashindwa kusoma kwa sababu ya uvivu!!


  Babu DC!!
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Du! Ukatili wa hali ya juu dhidi ya wahanga wote..halafu mtandao wake Dutroux ulisukwa vizuri. Kuhusishwa kwa polisi&rushwa kwenye huo mtandao kulichelewa upelelezi wa haraka sana.
  Asante Gustavo for sharing!..FurahiDay njema mkuu!
   
 10. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  unaomba radhi ya nini wakati uzi mtamu hivi.maskini cjui tutaashwa kufanyiwa ukatili huu lini?
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi bwana wewe hta ukiweka Kitabu kizima tutasoma tu
  Bado naendelea
   
 12. mwantui

  mwantui JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,249
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  inasikitisha asante mkuu...
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hebu nilale ntaisoma yote nikiamka.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni habari ya kuhuzinisha/kusikitisha sana. lakini uzuri kwa hawa wenzetu ni kuwa kila kwenye tatizo la aina hii, watafukua kila kitu katika kutafuta suluhisho. Huku kwetu, mhalifu ni mhalifu na akikamatwa anapelekwa mahakamani na akihukumiwa anapelekwa gerezani ambako hakuna hata mfumo wa kurekebisha tabia unaoleweka.
  kwa wenzetu ni tofauti. Inapotokea hali kama hii, ni lazima wataangalia chanzo cha tatizo ni nini. Mhalifu atachunguzwa kuona ni nini kilisababisha afanye alivyofanya. kwa kuchunguza hivyo, wanafikia mahali wanaweza kupanga sera za malezi ambazo zinahakkikisha kuwa zinapunguza kuzalisha watu wenye tabia kama hizo
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Babu, heshima sana! Kwenye post yangu nimetaja 'wanaokosa muda na wavivu'. Natambua siyo wote ni wavivu, lkn anayependa kusoma na akabanwa na majukumu hatahitaji kuombwa radhi! Labda tuwe tunawapa 'pole' tu watu wa hivyo... Babu hujawahi kuona watu wanaponda baadhi ya mabandiko humu kwa sababu tu ni 'marefu?'.
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hichi kisa kinasikitisha kweli, hasa ambapo maisha ya wasichana ambao walikuwa na haki ya kuishi. Lakini pia kisa kina mafunzo mengi kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mtiririko wa kisa unaonekana kama mnyororo, sababu moja imeungana na nyengine kiasi ambacho zote zinahusiana:
  - Utekaji nyara
  - Ubakaji
  - Unyanyasaji na ufanyaji ngono na watoto
  - Biashara ya madawa ya kulevya
  - Wizi wa magari.
  - Uzembe wa wanasiasa (Waziri wa sheria aliyetoa msamaha kwa wabakaji)
  - Uzembe wa polisi
  - Nguvu za genge la wahalifu (Mafia)
  - Uoga wa watu wa chini (polisi) kufatilia uhalifu kwa woga wa kupoteza kazi au kuuliwa

  - Kulindana kwa viongozi - wawe wanasiasa au watendaji.
  - .....................
  - .....................
  - ..................... na mengine mengi
  .

  Yote haya ni mfululizo wa matendo na mnyororo wa matukio ambao hapa tunaona ukweli katika ule msemo "Ukishangaa ya Mussa, utaona ya Firauna". Ikiwa nchi kama Ubelgiji, "nchi ya dunia ya kwanza" yanatendeka hayo, usishangae kuona kuwa nchi kama Tanzania "ya dunia ya mwisho", matukio kama haya ndio "mkate wetu wa kila siku".

  Je, hakuna "Little Judges" Tanzania (polisi, majaji, watendaji wengine) wenye/waliokuwa na uchu wa kuona haki inatendeka lakini akina "Van Der Biest" wanatenda watakalo wakilindwa na sheria na vyombo vya dola, kiasi cha kuwaziba midomo kwa kuwaua, kuwafukuza kazi, kuwahamisha vijijini mikoani ambako huishia huko na daima majina yao hayajulikani tena?

  Ni imani yangu, siku moja na Watanzania "tuwacha majembe, mapauro, spana, kalamu ofisini, usukani wa daladala, rundo za nguo kwa wamachinga hata wezi wadogo wadogo watastaafu kwa muda, ili sote tuungane tutoke mitaani tudai kwa moyo na sauti moja kusema:
  Hatutaki (viongozi) wauza madawa ya kulevya!
  Hatutaki Unyanyasaji wa watoto na wanawake!
  Hatutaki mikataba feki!
  Hatutaki uchakachuaji wa matokeo ya kura
  Hatutaki kutishwa, kuzibwa midomo na kuuliwa tukiwa katika harakati za kudai na kutetea haki zetu!
  ................................
  ................................
  ................................
  SASA BASI TUMECHOKA!
  HATUTAKI! HATUTAKI! HATUTAKI!
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Du, hii inasikitisha sana!
  Sasa naona mimovie mingi ya ngono ambapo vibont vidogo vinashiriki, huenda wametekwa na kulazimishwa kupigwa mipicha hiyo.

  Sijui wadada wa kibongo wanaoiga kila kitu kifanywacho na wazungu, wanajua kuwa wengine ni slaves na si ihari yao!
   
 18. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuna mijiwatu ina roho za ajabu sana humu duniani... Ni bora ukutane na nyati kuliko mijitu kama Dutroux... lol... Asante kaka.. Sisi wenye mabinti inatutia wazima kesi kama hizi...
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana aisee..
   
 20. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
Loading...