Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Baadhi ya vyuo vikuu vya umma nchini Afghanistan vimenguliwa tena kwa mara ya kwanza tangu kundi la Taliban lilipochokua madarakani mwezi Agosti.
Utawala wa Taliban umetangaza kuwa wanafunzi wa kike wataruhusiwa kuhudhuria masomo. Lakini endapo tu watatenganishwa na wanafunzi wa kiume na mtaala utafuata kanuni za Kiislamu. Nchi mbalimbali duniani zilishinikiza Taliban kuruhusu elimu kwa watoto wa kike, kama sharti la kupewa misaada ya kiutu.
Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifuatilia kwa karibu endapo utawala huo mpya ungeanzisha sheria kali kama ilivyokuwa wakati wa utawala wake katika miaka ya 90. Sheria hizo ziliwazuia wasichana kupata elimu na wanawake kufanya kazi.
Chini ya utawala wa Taliban, wanafunzi wa kiume watahudhuria masomo asubuhi na wa kike mchana ili kuendana na mfumo wa kutenganisha jinsia.