Utawala wa sheria ni upi ikiwa muumini wa kusimamia utawala huo ana vunja sheria?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Naomba wakuu mjaribu kunijuza nami angalau nipate maana halisi ya utawala wa sheria,serikali imekuwa kila siku ikijinasibu serikali sikivu yenye kufuata utawala bora lakini ndani ya serikali hiyo hiyo kumekithiri uvunjaji wa makusudi wa sheria za nchi.Mambo mengi tu yametendeka pasi na kutia shaka kuhusu uvunjwaji wa sheria unao fanya na serikali yetu kupitia wizara na taasisi zake.

Lengo hasa la mada hii ni kutaka kupata tafsiri sahihi juu ya uatawala wa sheria.Aliyoyafanya mh waziri Pro Muhongo na katibu mkuu wake kutekeleza mipango ya kununua mafuta kwa bei nafuu na kuokoa takribani bilion 3 ni kizuri lakini je sheria ya manunuzi inasemaje!?

Unapozungumzia utawala bora una maanisha nini.Unapo tumia power of appoint kuteuwa wale wale ambao wanvunja sheria kuna ashiria nini?

Bwana mkubwa mmoja toka nchi za kaskazini mwa Afrika bwana Ibrahim Mo aliamua kuweka tuzo ili kuweza kuwanusuru viongozi wetu na nchi zao kama wakifanikiwa kuongoza na kufuata utawala wa sheria,lakini tuzo hiyo kwa kiongozi wetu inaonekana haina tija zaidi ya kubariki mali za Watanzania kudhulumiwa na walafi wachache.


Naomba niishie hapa kwani matukio ni mengi ambayo ni viashiria vya kwenda kinyume na utawala bora ambao kwangu mimi naamini utawala bora ni utawala wa sheria,naomba majibu kwenu ili tuweze kuwauuliza viongozi wetu
 
Back
Top Bottom