Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Unaweza ukasema labda ni miujiza maana hii sio kawaida kwa serikali nyingi za Kiafrika. Maana pale bunge la bajeti linapoanza kukaa serikali nyingi huwa zimeishiwa pesa na nyingi huwa zimesimamisha shughuli za kimaendeleo ili kusubiri mwaka mpya wa fedha uanze.
Lakini kwa John Pombe Magufuli hili ni habari nyingine. Tayari alikuwa ameshajenga hospitali za wilaya 67 na zimeshakamilika. Sasa tayari ameshatoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospital zingine 31 za wilaya ili zianze kujengwa. Moja ya wilaya zilizonufaika na mgao huo wa pesa ni wilaya ya Misungwi na Sengerema.
Kwa wapinzani hii ni dhahiri kuwa CCM na serikali yake chini ya JPM wamejipanga kuwatumikia wananchi. Na mnatakiwa mkubali kuwa rushwa na ubadhilifu vimedhibitiwa ndio maana serikali inakuwa na pesa za kutekeleza miradi hata kama tunaelekea ukingoni mwa mwaka wa fedha.
Na kwa mantiki hii, nawasihi wapinzani muache maigizo ya kutangaza nia ya kugombea urais. Ubunge na udiwani jaribuni japokuwa ni kijani tu ndio wengi watarudi.