Utawala wa Rais Alhaji Ali Hassani Mwinyi na maendeleo ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala wa Rais Alhaji Ali Hassani Mwinyi na maendeleo ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John W. Mlacha, Jun 24, 2012.

 1. J

  John W. Mlacha Verified User

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Mwinyi aliachiwa nchi na Nyerere, huyu mwinyi alikaa madarakani kwa miaka 10, nataka kujua kuwa aliifanyia nini Tanzania, alifanya nini kuwasaidia watu wa pwani,visiwani na watu wa kusini mwa Tanzania. Nataka mtu mwenye facts bila udini,udini si mahala pake.
   
 2. A

  Albimany JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ni Raisi alie ruhusu biashara huria Tanzania hasa Tanganyika kabla ya mwinyi mtanganyika hakuthubutu kuuza wala kununua mambo hayo yalimilikiwa na serekali tu.

  Na sema Tanganyika kwasababu Zanzibar hakukuwahi kua na Upuuzi huo na ndio maana si semi Tanzania.

  Tv, zilikua marufuku kama afghanistan ya Taliban, sabuni mchele sukari nguo hukuweza kununua hata kama unapesa lazima ununue katika maduka ya serekali kwa kiwango maalum sio mtu atakavyo.

  Watanganyika mshukuruni Rais Mwinyi.
   
 3. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hacha kudanganya bhana...soko huria halikuletwa na mwinyi ni dunia ndio ilibidi iingie kwenye mfumo huo wa soko..kwa bahati ilikuwa ni kipindi cha mwinyi hivyo hata angekuwepo nyerer bado ingekuwa hivyo...nachojua kikubwa mwinyi alimsaidia na kumjenga kisiasa JK ili aje kutawala hata alipoharibu yalifichwa na akamwacha pazuri hadi mkapa akamtumia chini ya usimamizi mzuri.....kitu ambacho na JK anajaribu kumjenge J.makamba kwa style hiyo hiyo ila sidhani kama ita work maana watu wameamka na ushahili huu wa kupangana...kikubwa lazima watanzania lazima tumshukuru mwinyio ni kuwa hakuwa na hiyana ye apate na we upate alijali wasomi kwa wasanii....mwenye uwezo alimpa nafasi bbila kujali anamjua kiviipi au ni msanii kivipia u anauchawi gani......hapo Mwinyi namkumbuka hadi leo na ninamuombea mungu amsaamehe kwa mabaya yake kwani ni binadamu hajakamilika.
   
 4. A

  Albimany JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45

  Hivyo ukisema dunia unamainisha ni tanganyika tu? mbona Zanzibar hakukua na marufuku ya uingizaji vitu?

  Kenya na nchi nyengine hatukusikia upuuzi huo. Ni Nyerere pekee ndie aliebana.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Alianzisha AZIMIO LA ZANZIBAR

  - Aliua Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kutoka kwa Chama Chake cha CCM

  - Liliua JKT

  - Liliruhusu Viongozi kumiliki Majumba ya Kifahari

  - Liliruhusu Uhuru wa DINI - Dini nyingi zilianza Nzuri na Za Uwalakini

  Mapendekezo ya Kuuza Mashirika ya Serikali yenye Hasara/YOTE YALIKUWA YANA HASARA

  ALIMLETA POPE JOHN PAUL (NYERERE HAKUWAHI KUFANYA HIVYO WAKATI WA UTAWALA WAKE)

  Alianzisha 1st Ladies kuwa Part Business Ladies, Part Motivational Speakers, Owning NGO

  Alitenganisha Rais wa Zanzibar asiwe by law Makamu wa Rais wa Tanzania (Ambayo Sasa Wanzanzibari wanataka Irudishwe)
   
 6. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zanzibar ilikuwa ndani ya Tanzania wewe...unajua kuhusu decentralization wewe????au unakurupuka tuu kujibu?unajua shinikizo la nchi za magharibi khs market oriented economy?weee usitudanganye sio wazamani sie eti mwinyi ndie aliyeruhusu ni hayo ni mabadiliko ya kiuchumi na masoko kaka pole kwa kutoelewa unadhani ulisaidiwa na mtu mmoja nae ni mwinyi..narudia tena mwinyi nitamkumbuka kwa kutoa fursa sawa kwa wote, mafnya biahsara,mfanyakazi,mkulima msanii kaka weweee wote walikuwa na equal chance provided wana struggle lkn shv ukiwa msaniii na mchawiii ndio una make up...otherwise unaumia tuu...hakuna maana kuwa mfanyakazi au mfanya biashara mdogo shv...I mean ni lazima uwe mfanya biashara mkubwa nayo hauwezi kuwa bila kuwa msanii fisadiiii kama wewe na kingine uwe mchawii ili uugopwe na utumiwe na wasanii kuwaloga kwa kukuamini.

  Nimetosha kukujibu siwezi poteza mda na wewe pengine yanakuingia sn maneno haya unajibu bila mpangilio
   
 7. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,612
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Aliongeza sana uhuru wa watu katika kutoa maoni lakini alivurunda sana kwenye uchumi. Inflation ilifikia 30%.
  Aliwafanya watanzania, kila mmoja aone anaweza kuwa Rais.
   
 8. u

  umsolopagaz Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...comrade...salute! kwanza, anatufundisha "hayati" shaaban roberts..."mbwa wa msasi mkali ni wakali kama msasi mwenyewe"...huyu (mwinyi), alikuwa ni makamu wa mwalimu...na mara baada ya kuteuliwa na mkutano mkuu wa ccm kuwa mgombea pekee wa uraisi, mwinyi akionyesha busara na hekima ambayo kwa muda mrefu hatujaishuhudia, aliwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpitisha kuwa mgombea uraisi, "na akawaomba, ktk kipindi chake cha uraisi, wasimuonee kwa kutaka kuulinganisha uongozi wake ulivyokuwa uongozi wa mwl, akiukumbusha umma kuwa mwl ni tunu ambayo watanzania tulikuwa tumetunukiwa na mungu na tusikae tukiitegemea kwa mara ya pili...("kunilinganisha mimi na mlw, ni sawa na kulinganisha mlima kilimanjaro na kichuguu")...lkn kubwa ambalo mwinyi alilifanyia ni kuleta mabadiliko ya kiuchumi, ingawa hakufanya juhudi za kutosha kuuandaa umma wa watanzania na mabadiliko hayo, na mabadiliko ya kisiasa..pia misingi ya uendelezaji wa miundombinu ya uchukuzi na mawasiliano ilianza kuwekwa ktk awamu zake..miaka kumi kwa raisi kuleta maendeleo wanayotaka wananchi ni michache, alijitahidi kufanya alichoweza, na huku kama ilivyo kwa viongozi wote akifanya makosa...
   
 9. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakuna maendeleoisha if duniani bila kuwa na basic industries. Viwanda vinavyotengeneza bidhaa inayotumika katika viwanda vingine. Hivi viwanda ndio vilianzishwa miaka ya 70 chini ushwawishi na usjauri wa Marehemu Professor Justian Rweyemamu. Kulianzishwa viwanda vya nguo na nchi zozote duniani zimeendelea kwa viwanda vya nguo.

  Sasa Mwinyi aliua viwanda hivyo kwa sera yake ruhusa. Sijui bila kulinda viwanda vya ndani unaweza kuendeleza uchumi. Maswala ya TV na Simu naona hayana tija na anayeyahesabu kuwa ni sehemu ya maendeleo huyo anafifisha fikra ya usomi na hajui dunia inaendeleaje maana haya ni amendeleo ya miaka 80 na 90 ndio maendeleo ya simu za mikonini na television yalivyoshika kasi kama ilivyo computers.

  Tunapoangalia tuangalie maendeleo katika upana wake. Tumekuwa tunadanganywa eti Mwinyi akukuta Tanzania ina kitu. Ni uongo wa mchana maana amekuta nchi inazo fixed assets kama viwanda, ardhi yenye rutuba, madini, reli, viwanja vya ndege na ndege, mabwawa ya umeme na maziwa na mito.Je, assets hizo zimesaidia maendeleo ya taifa au wachache.

  Madini ni wa kwanza kuingia mkataba, madini, kugawa mistu yetu na mbuga za wanyama na wanyama wetu, ni mwasisi wa rada na IPTL. Tuweke haya kwenye mizani ili tuone kama taifa, kama mtu mmojammoja tumefaidi nini?
   
 10. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aliamuru jeshi la Tanzania livamie wanakijiji kwa kuunda hivazi ya Mkomazi kwa ushawishi na majeshi yalichoma vijiji, yalibaka, yaliu kwa amri ya Mwinyi na sijui kama kesi hiyo haipo pahala fulani
   
 11. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alijaza madudu ikulu na kuumiza Tanzania, huku akijaza utalii Zanzibar
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Alikwenda kucheza KWASAKWASA la BONGOMAN madakitari walipogoma 1992
   
 13. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bora aliyebinafsisha akawapa makaburi akaweka hela mfukoni akasepa.Sasa hivi hata shingo hainokani imeunganikana na mabega.
   
 14. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aliwajaza Wazanzibari Bara wanakoishi asilimia 60 ya population ya Visiwa
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Alileta mageuzi ya biashara na uchumi. Alileta mafuta ya magari. Alileta dawa za meno na kandambili na viatu. Alileta mchele na sukari. Alileta neema na tabasamu kwenye nyuso za Watanzania. Alileta vyama vingi. Alileta RUKSA.

  Kwa ufupi aliwatoa wananchi kwenye lindi la umasikini na ufukara kuwarudisha duniani.

  Hivyo vyote vilikuwa hakuna wakati wa Nyerere.
   
 16. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka kidogo Mwinyi hakuwa dhaifu kama Jk, si mnakumbuka zile ishu za mabucha ya nguruwe yalipovamiwa na waislamu wanaojidai wana itikadi kali (Aliwafanya mbaya mpaka wengine wakakimbia mji) tafauti na Jk na uamsho wake.
   
 17. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Kila mwenye kisu kikali na ale nyama"

  Ndio ulikuwa msemo wa Mzee Mwinyi alipopewa mamlaka ya utawala, alifungua milango ya biashara holela, kila mwenye biashara aliingiza bidhaa zake sokoni Tanzania, kuanzia nguo, vyakula vilivyosindikwa, madawa ya binadamu, vyombo vya mawasiliano, madawa ya kulevyia n.k.

  Ndicho kipindi serikali ilishindwa kabisa kukusanya kodi, miradi mingi ya maendeleo ilisimama hadi aitishe harambee ya kuuza picha yake na saa kujaribu kunusuru miradi muhimu ya jamii iweze kuwepo, lakini matatizo yalikuwa ni makubwa kuliko uwezo wake wa kuyatatua, badala ya kujenga yeye alikuwa anachimbua, inflation ilikwenda juu, kwani waliokuwa na visu vikali waliweza kukata minofu minono ya uchumi kwa kujinafasi.

  Aliporomosha uchumi kiasi kwamba noti ya shilingi 1,000/= ilionekana ni ndogo, hadi kulazimu kuchapisha noti za shilingi 5,000/= na 10,000/= ili ziweze kubebeka kwa urahisi.
   
 18. B

  Bob G JF Bronze Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  1. Tulianza kuiona Dunia ama alitutoa matongotongo,
  2 .ilikuwa nchi ya kila kitu Ruksa,
  3.Watu binafsi walikuwa na fedha kuliko serikali,
  4.Tenda za serikali hakuna aliekuwa anazikimbilia walikuwa hawalipi,
  5. Mrema alikuwa na nguvu kuliko Rais,
  6. chimbuko la maporomoka ya maadili na uadilifu ndipo yaliposhika kasi,
  7. Kifo cha Ujamaa wa nyerere kule zanzibar (azimio la zanzibar)
  8. kuja kwa Madiba Mandela na Nyerere kumpokea mgeni mashuhuri,
  9.Noti za shs elfu 5,10, zilipozaliwa,
  10. mzunguko wa hela kutoka 4% mpaka 28% (kama alivo ukuta Kikwete toka kwa Ben 4% hadi leo 21% akimaliza utakuwa 50%) na atakae kuja 2015 atashusha hadi 3%.
  11. Mwinyi kama Mkuu wa nchi kujitoa kuwa mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam,
  12. Tanzania kuwa soko kuu la Mitumba, hakuna chuo kikuu kilichojengwa ktk utawala wake,
  13. Uvamizi wa maeneo ya wazi,
  14. Agustino Lyatonga Mrema ateuliwa kuwa Naibu Waziri mkuu (cheo niki si cha kikatiba)
  15. anashauriwa na mkewe kauli yaNyerere
  16. Malesela na Kolimba Ni wahuni Kauli ya nyerere
  17. Na mengine mengi kama GONJWA HILI LIMETUFIKA MAHALA AMBAPO SOTE TWAPAPENDA
  18. Kilikuwa ni kipindi chenye uhuru uliopindukia kama Gulamali alimwita Mama siti SHEMEJI, Ikulu si Gulio ni mahala patakatifu, Mrema kuitwa mbwa na Nyerere Hatuwezi kuruhusu nchi itawaliwe na mbwa, Kama ni Mzuri Pelekeni posa mkanywe na chai.
   
 19. B

  Bob G JF Bronze Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duh kweli mabomu Mwembechai yalipigwa mpaka msikitini mambo mengine alikuwa mkali
   
 20. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Loooo jamani !!!

  Ndiye aliyefanya mazishi rasmi ya centi 5, centi 10, centi 20, centi 50, shilingi 1, shilingi 5, shilingi 10 na shilingi 20.
   
Loading...