Utawala wa namna hii huwa 'nauchukia' na 'naudharau' mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,877
Umeshasema kuwa mwisho wa Wamachinga kuwa maeneo wasiyotakiwa ni tarehe 18 Oktoba, 2021 kwanini tena msogeze Siku mpaka tarehe 30 au 31 Oktoba, 2021?

GENTAMYCINE nachukia Watu (hasa Watawala) wasio na 'Misimamo' na wanakuwa 'Kigeugeu' katika ama Matamko au Mwamuzi yao.

Kama mnadhani hii 'Huruma' yenu ya 'Kinafiki' dhidi ya Wamachinga kwa Kuwaongezea Siku zaidi za Kuhama imewapa 'Credits' za Kisiasa na Kiutawala bali nawataarifu kuwa sasa ndiyo imewafanya 'Mdharaulike' na muonekane Wapuuzi na Waswahili.

Serikali makini haipendwi wala haisifiwi na Wananchi kwa kuwaonea Huruma Kinafiki bali ni kwa kuwa na Msimamo huku ikisimamia taratibu, nidhamu na Misingi iliyopo au iliyowekwa.

Nina uhakika Serikali juzi ile ile (ya Ukomo wao waliouweka) wangeamua 'Kubomoa' na Kuwaondoa Wamachinga maeneo wasiyotakiwa ingeheshimika, ingeogopeka na isingeoneka ni Lege Lege (Ndembe Ndembe) na iliyojaa 'Undumilakuwili' mwingi.

Upuuzi huu huwezi Kuukuta kwa Mataifa yaliyo 'Serious' kama ya Israel, Korea Kaskazini, Rwanda, Urusi, Cuba na China. Serikali haitakiwi izoeleke hovyo na Wananchi bali isimamie Kanuni na Miongozo iliyopo Kikatiba au Kisheria.

Subirini GENTAMYCINE ndoto yangu ya kuja kuwa Rais wa Tanzania itimie mbona mtanitambua na mtanyooka Wenyewe. Sitokuwa na Huruma Wala Upendeleo kwa Watu, Ndugu zangu na Marafiki bali nitafuata Katiba na Utaratibu wa Kiutawala / Kiuongozi.

Mkidharauliwa mnatusema tunatumika.
 
Hata stendi ya mabasi magufuli mbezi mle ndani waliongezewa siku 10 ili kuwapa muda zaidi wa kujenga na kuhamisha biashara zao..zilipoisha siku 10 wote waliondoka bila fujo wala ghasia. Kuongeza siku 12 haifanyi serikali Kwamba ni dhaifu Bali kuwapa muda zaidi wakujenga vibanda vyao sehemu mpya wanazoenda.
 
I just thought that, kama hio serikali imedhamiria hasaa 100% kukoma umachinga basi watuoneshe kweli yani hata kama it would take them long.

Sina shaka kwa strain hio kutok kwa serikali, automatically sisi machinga tutatengeneza/tutapata Fursa mpya kama ambavyo tuliona umachinga ni fursa. HATUTAKUFA, kama ni mduarani tukaingie, kama ni kwenye majaruba barida tuu.
 
Ulitaka siku zilipoisha waanze kuwaondoa kwa nguvu upate uhasi wa kuongea tena wameongeza siku napo unachukia wew ni mtu wa Aina gani.
 
Kiongozi una moyooo, yaani umehangaika kuijibu hiyo thread kweli?
Kwa Kuniogopa naona umeamua uje na ID yako nyingine ili Kunikabili ukidhani huwa siwajui 'Haters' wangu.

Na nitawateseni mno Wapumbavu kama Wewe hapa Jamvini mpaka mpasuke na Mfe.
 
Back
Top Bottom