Utawala wa Mwl. J.K.Nyerere V/S Uliopo sasa!

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Hebu tufikirie huu msemo.. 'MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA'...je umetimia kwa asilimia ngapi? Tukumbuke utawala wa Nyerere.. Kipindi kile kulikuwa kuna tofauti ndogo sana kati ya viongozi na wananchi! Nyerere alikuwa anaingia shambani na wananchi wanalima pamoja, wanakata kuni pamoja na kufyeka nyasi haijalishi kuwa yy ni rais, alikuwa anajichukulia kuwa yy na mwananchi wa kawaida. Kama umewah kushuhudia baadh ya video yake utaona hilo. Simaanishi viongozi wafanye hivyo, bali nawashauri viongozi wafanye mambo ambayo yatatufanya sisi tuone kuwa wao ni kama sisi na hakuna gape kubwa. Tukiangalia hivi sasa ni viongozi gani wanaweza kujichanganya na wanajamii? Matatizo ya mafuta, mgao wa umeme, shule nyingi duni za kata, matatizo ya huduma ya afya na foleni barabarini zina wakumba sana raia wa kawaida na viongozi wana kumbwa kwa kiasi kidogo. Viongozi wetu waache kuiga, marais wa nchi zilizoendelea wanafanya ziara nyingi nje ya nchi kwa sabab maalum! Sisi bado tupo ktk nchi zinazoendelea hivyo tuwajibike ndani ya nchi yetu! Sipo ktk chama chochote but sipendi utawala wa kunufaisha tabaka la juu tu! Kiukweli miaka 50 ya uhuru lakini maendeleo ni machache sana!
 
Wanajilimbikizia kama vile wakifa wataondoka navyo, kumbe unaondoka na sanda tu.
 
<font color="#ff0000"><font size="3">Wanajilimbikizia kama vile wakifa wataondoka navyo, kumbe unaondoka na sanda tu.</font></font>
<br />
<br />
ni kweli kabisa.. Mali ni yakupita tu!
 
Back
Top Bottom