Utawala wa JK umezikuza mno nyufa hizi za utaifa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala wa JK umezikuza mno nyufa hizi za utaifa...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 14, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Nyufa hizo ni nne za kitaifa zilizoongeza migawanyiko mikubwa ni:-

  a) Umasikini na tofauti za kimapato zimepamba moto na kunenepesha matabaka ya kiuchumi ndani ya jamii yetu.


  b) Udini umeshamiri kupitia ajira za ngazi za juu serikalini zenye upendeleo kwa dhehebu moja, Ilani ya CCM ya 2005 ilidhubutu kukusudia kuanzisha mahakama za kadhi ndani ya serikali isiyo na dini na jitihada za kujiunga na washirika wa nchi za kiislamu duniani wa OIC. Hili kuliko yote limeleta mgawanyiko mkubwa kati ya matabaka ya kidini hususani wakristo na waislamu. Wakristu wengi hivi sasa wanamwona JK siyo Raisi wao na anapendelea dini yake na hii ni moja ya sababu yao ya kutompigia kura

  c) Ujinga hususani shule za duni za wanyonge za kata na kutokuwa na jitihada za makusudi za kuimarisha elimu ya watu wazima. Kwa taarifa yetu tu, hakuna kiongozi yoyote ndani ya serikali ya JK ambaye watoto wake wanasoma kwenye shule za kata.

  d) Kuporomoka kimaadili hususani serikalini na kusababisha kashfa nzito za ufisadi kulighubika taifa. Kashfa hizo zimeligawa taifa katika makundi ya watawala wadhalimu na watawaliwa wanyonge.

  TUNAHITAJI RAISI AJAYE AWE ANAZITAMBUA CHANGAMOTO HIZO KUTOKA NDANI YA MOYO WAKE NA MATENDO YAKE.....CHAGUA DR. SLAA.....CHAGUA CHADEMA......................................
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  katika kujenga utaifa ni vyema tukatumia busara katika kupresent mambo yaliyo miyoni mwetu. Hiyo kauli yako ni hatari sana mimi ndio mara ya kwanza kuisoma ikiandikwa wazi wazi namna hiyo. Hivyo inaweza kujenga negative consequences kwa wasio wakristo. Aidha pia inaweza kuwachochea wakristo kumdharau rais wao. I wish you have the guts to withdraw it.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Rutashubanyuma.

  Mkuu ukijaribu kumchambua Kikwete utagundua ni aina ya kiongozi asiyetabirika au kwa maneno rahisi kidogo ni kiongiozi mwenye sifa za kinyonga.Unaweza kushangaa sana aliwezaje kupenya hadi kushika madaraka makubwa bila viongozi wa chama chake kujua hana uwezo wa kuongoza achilia mbali ugonjwa unaomwandama kila mara.

  Alipoingia madarakani aliwapa matarajio makubwa watanzania wengi kwamba ni kiongozi waliekuwa wakimtarajia kutatua matatizo makubwa yaliyokuwa yakilisumbua taifa rejea hotuba yake ufunguzi wa bunge mwaka 2005.Aliunda tume ya jaji Kipenga kuchunguza mauaji ya wachimbaji na wauza madini kule Morogoro tukashangilia sana tukaamini Kikwete akiendela na kasi hii hakika maendeleo tutayaona.Kabla hatujakaa vizuri akaunda tume ya kuangalia upya mikataba mibovu ya madini matokeo yake mpaka leo hatuyaoni.

  Nilianza kutilia shaka dhamira ya Rais Kikwete baada ya kugundua alikuwa akirundika miradi mikubwa Bagamoyo nyumbani kwake.Nilishangaa kusikia mpango wa kujenga International Airport,Ujenzi wa barabara Bagamoyo - Chalinze,Bandari kubwa ya kisasa,kijiji cha michezo,kituo cha mikutano cha kimataifa sijui AICC itapelekwa wapi na Chuo kikuu.Ukifuatilia miradi itakayopelekwa Bagamoyo unazidi kushangaa ni kwanini Kikwete asiwaombe kura wakaazi wa Bagamoyo pekee ambao kaamua kuwasukumizia maendeleo na kuwaacha watanzania wa sehemu nyingine wamchague kiongozi ataepeleka maendeleo bila kujali sehemu walizotoka.

  Kikwete kaanzisha ufa ambao mwanzo haukuwepo wa kiongozi kurundika maendelo sehemu walizozaliwa Nyerere hakuufanya,Mkapa hakuthubutu zaidi ya kujenga daraja la Mkapa ambalo lilifungua mawasiliano,Mwinyi hakufanya upuuzi wa jinsi hii.Kitendo cha Rais Kikwete kitaweza kuwashawishi marais wengine kufanya upuuzi huu au kuwashawishi wananchi kuanza kuchagua rais kutika eneo lao kwakujua atapendelea sehemu aliyotoka.Bahati mbaya Afrika imewahii kuzalisha viongozi wa aina ya kikwete,kenya walikuwa na Daniel Arap Moi,Congo walikuwa na Mobutu Seseko Kuku wazabanga,Ivory Coast walikuwa na Félix Houphouët-Boigny na Tanzania tunaye Kikwete.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Kikwete ni Kuwa anamsikiliza sana Hassan Mwinyi ambaye hakuwa anaelewana sana na Rais Julius Kambarage Nyerere kwasababu ya uanzishwaji wa ubepari wa kimakundi an upendeleo kwa baadhi ya waisilamu wafanyabiashara. Kwahiyo Usawa huo ulitulia wakati wa Mkapa lakini sasa umeimarika Mtu kama Mbunge wa Igunga alikuwa powerful sana wakati wa utawala wa Mkapa.

  Nchi yetu hii kama hatutaangalia tutatumbukia kwenye udini mbaya na ninaomba mungu kuwa ukabila hautaanzishwa au Ujeshi.
   
 5. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  sidhani mada zenye mlengo wa kukuza na kushabikia udini zinz tija yoyote, sana sana tutachangia hali hiyo kuongezeka
  .
   
Loading...