Utawala wa Israel wateketeza mashamba ya mizaituni na mabwawa ya maji Ukingo wa Magharibi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Utawala wa Israel wateketeza mashamba ya mizaituni na mabwawa ya maji Ukingo wa Magharibi

Katika mwendelezo wa jinai na ukatili wake, utawala wa Israel umeteketeza zaidi ya miti 550 ya mizaituni yenye matunda na mabwawa kadhaa ya kuhifadhia maji katika mkoa wa Tubas, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Mu’tazz Basharat, afisa anayeshughulikia faili la makazi katika mkoa huo amesema kuwa, askari wa utawala katili wa Kizayuni wametekeleza jinai hiyo majira ya saa 12 asubuhi ya leo.

Amezidi kufafanua kwamba eneo hilo lenye mashamba bado kesi yake iko katika mahakama za Israel ambapo imepangwa kutajwa tarehe 25 ya mwezi huu wa Juni.

Basharat amesema kwamba askari wa utawala wa Kizayuni bado wanaendeleza unyama wao wa kuharibu mashamba ambapo katika tukio la leo wamekata kikamilifu miti ya mizaituni zaidi ya 550 yenye umri wa miaka mitano sambamba na kufunga mabwawa ya kuhifadhia maji katika eneo hilo.

Afisa huyo anayeshughulikia faili la makazi katika mkoa wa Tubas, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan amesema kuwa ardhi hizo ni mali ya raia wa Palestina wanaoishi katika mji wa Tammun wa mkoa huo.

Hii si mara ya kwanza kwa utawala haramu wa Kizayuni kuteketeza mashamba ya mimea tofauti ya Wapalestina, jinai ambazo zinafanywa na utawala huo pandikizi kwa lengo la kuwashinikiza Wapalestina hao kusalimu amri mbele ya utawala huo khabithi wa Israel.

PALESTINA
 
Hawa wazungu waliondoka bure ulaya na kwenda kung'ang'ania jangwa,baada ya miaka mia sijui wataishi wapi
 
Back
Top Bottom