Tafsiri rahisi ya utawala wa Kiimla ni aina ya utawala ambapo anayeongoza nchi hujipa ridhaa ya kuongoza yeye mwenyewe.
Ni ukweli usiopingika kwamba Jk hakuchaguliwa na wananchi. Tofauti na Watawala wengine wa Kiimla (dictator), Jk yeye alitumia kiini macho cha sanduku la kura. Anataka kuhadaa watu kuwa alichaguliwa kwa kupigiwa kura kumbe sivyo hivyo. Naomba nitoe machache kueleza kuwa hakuchaguliwa na wananchi:
1. Yeye ndiye Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wananchi wanapiga kura, kwa vitendo vyake vya kuamrisha vyombo vya usalama kutumia mabomu ya machozi wakati wa kampeni mf. Mbulu, ni wazi kuwa hakuwa anaridhika na msimamo wa wananchi. Kuwasomba watu kwa kutumia magari ili wahudhurie mikutano yake alikuwa analazimisha kufanya mapenzi na Watanzania bila ridhaa yao.
2. Tume ya uchaguzi inawajibika kwake na haikuwa tayari kusikiliza malalamiko toka vyama vingine. mfano, alikkuwa anafanya kampeni mpaka usiku kinyume na sheria. Je kama alikuwa anavunja sheria bila kuchukuliwa hatua zozote, atashindwa kuamrisha NEC imtangaze hata kama hajashinda? Watautoa wapi ubavu huo. kama NEC ingelifanya chochote ambacho kingeonesha kuwa JK na Dr. Slaa walikuwa na haki sawa basi mwenyekiti wa Tume angefukuzwa kazi kwani yeye ndiye aliyemteua. Baada ya kumfukuza kazi tungeambiwa kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kama ilivyotokea kwa baadhi ya Wasimamizi (ngazi ya Jimbo).
3. Jk alijua kuwa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (ambayo CCM hawataki ibadilishwe) hata kama atatangzwa pasipo uhalali hakuna anayeweza kwenda mahakamani (labda The Hague). Hata kama mtu angeenda mahakamani haki isingepatikana. Hivi kuna ulazima gani kwa JK kusubiri kura halali ambazo zinaweza kumfanya asiwe rais aliyechaguliwa na wananchi wakati anajua anaweza kuupata urais kwa kuchakachua? katiba yetu hata mwendawazimu inaweza kumpa urais