Utawala wa Hayati Dkt. Magufuli ulijaa kiburi, majigambo na uonevu, ufitinishi na visasi

Captain Justine

JF-Expert Member
Sep 19, 2014
1,123
2,000
Mungu atatukuzwe yeye pekee yake.
Madikteta wengine wanadumu madarakani muda mrefu ila jiwe alijikuta mungu wa tz ndipo hapo Mungu wa sirini akaona sasa yatosha.

Yule mbunge wa darasa la 7 kutoka ukanda alisema Lissu akaguliwe makalio (alitumia neno lenyewe) kwamba huenda ni shoga dah.!

Yupo mwenyeti ccm wilaya nimemsahau jina alisema anaomba rais awaruhusu kuwavunja vunja wapinzan na wote wenye kumpinga (kilikua kipindi cha kampeni).

Mimi ndiye nimewaletea tetemeko, dah.! Halafu ukute fedha zile zimetumika kinyume kabsaa na aliyoyasema.

NIFUNDISHE KUNYAMAZA.
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,516
2,000
Na kila wakati
Kurudia rudia kutaja majina yake yote wakati yanajulikana kwa kila mtz.
Kumsifu kila wakati kwenye vyombo hata kwenye zamu za kupokezana kijiti cha uongozi wa jumuia/umoja za nchi mbalimbali.
Kunyamazia matukio ya mauaji, kushambulia, utesaji, ukandamizaji wa haki, ubambikizaji wa kesi yaliyo wazi kabisa - Acquilina na kumlinda Mkurugenzi, Polisi.
Kunyamazia na hata kushangilia uminywaji wa uhuru wa maoni, habari, demokrasia na haki za vyama vya siasa kufanya kazi zao; uvunjaji wa wazi sheria/katiba ya nchi.
Matumizii ya vyombo vya serikali vinavyoendeshwa kwa kodi za wananchi kwa faida ya CCM; TBC....
Kweli nji ilikuwa chini ya Dikteta uchwara.....!!! Hili hata mafisi wengi wa Lumumba wanalifahamu. Waulize kina Nnape Naiye, Bw. Kinena, Januari Makamba, Bernard Membe, etc watakuambia....!!!!
 

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
3,979
2,000
Huo ndio mtazamo wangu ukiniuliza juu ya utawala wa HayatiMagufuli.

Kaburi kilikuwa kikubwa aliogopewa na kila kiumbe Cha Tanzania alizungumzwa sirini watu waliogopa hata kuta za nyumba zao wakihisi magufuli atakuwa anawasikia.

Ufitinishi wa kina Cyprian Musiba ulifikia kiwango cha kutisha, Musiba aliweza kumfitini yeyote na wakati wowote bila woga akijua kwamba genge lao ndio lenye sheria na bosi wao ndio sheria yenyewe aliamua nani atoweshwe nani akirimiwe.

Kina Makonda waliishi kama miungu watu, kina Polepole walijirekodi mpaka video wakicheza kwa kejeli kwenye mazulia mekundu kwenye majumba ya Serikali sisi wengine tulikaa kimya tukiamini mpanda ngazi hushuka.

Spika alimnyanyasa Lissu kama jambazi yaani Lissu alilia akanyamaza Mungu wake alimfuta machozi na nyie kina Ndugai mliyekuwa mnamtetemekea kafa sasa anaitwa mwendazake subirini na nyie mlipe yale mliyoyafanya enzi zenu mkiwa miungu watu.

Mama Samia Suluhu Hassan jitenge kabisa na hawa watu

Polepole
Cyprian Musiba
Bashiru Ally
Makonda
Ayoub Ryoba - Mkurugenzi wa TBC

Nk

Imeandikwa amelaaniwa amtegemeae binadamu.
Kuna siku mvua ilinyesha hapa Mtwara wakasikika baadhi ya wakulima kwenye redio wakitoa shukrani kwa serikali ya Awamu ya tano! Msimamizi wa Kituo cha Redio naye aliongezea "tunamshukuru na Rais Dr. JPM kwa kuleta neema ya mvua, au siyo?"
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
555
1,000
Mitano tena , wanatia huruma sana wengine wanaomba msamaha hadi vivuli vyao wengine wanakamatwa kwa ufisadi yaani tutajua mengi sana sema Ameeen
 

mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
970
500
Mwambieni Sasa Cyprian Musiba polepole na wenzenu wa mataga watambe Kama walivyokuwa wanatamba enzi za mwendazake.
Kama waliyokuwa wakisema ni haki, mimi sioni tatizo la wao kuendelea kusimamia misimamo yao hiyo, kama wewe unavyo simamia misimamo ya Tobo, utadhani ulikunywa maji aliyokupa Tobo, hivyo uko tayari kusema na kunena lolote lile, iwe kweli iwe uongo, iwe shombo au iwe chochote. Pole sana Mhabeshi!
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,516
2,000
Kuna siku mvua ilinyesha hapa Mtwara wakasikika baadhi ya wakulima kwenye redio wakitoa shukrani kwa serikali ya Awamu ya tano! Msimamizi wa Kituo cha Redio naye aliongezea "tunamshukuru na Rais Dr. JPM kwa kuleta neema ya mvua, au siyo?"

Unajua kulikuwa na Watz mabwege walikuwa wakimwona JPM kama kamungu mtu fulani hivi....!!! Yaani kila kitu Magufuli...!!!
Lakini Biblia imeweka wazi kabisa kwamba:

Yeremia 17:5,
"BWANA asema hivi, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom