Utawala wa Awamu ya Tano hauna time na utu na mwanadamu?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,785
102,156
1. Utawala huu wa awamu ya 5 ndio utawala unaovunja haki za watu kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijawahi kuonekana nchini, ndani ya muda wake mfupi wa miaka miwili ya utawala huu, magazeti zaidi ya matatu yameshafungiwa sasa, magazeti yote hayo yalionekana kuwa mwiba kwa Serikali kwa kuhoji na kuandika mambo mbalimbali juu ya hali ya Nchi yetu. Si hilo tu, bado kuna zuio lisilo la kikatiba la Rais juu ya mikutano ya hadhara, huku mamia ya watu wakiwa wameshtakiwa, na wengine kuhukumiwa vifungo na faini, kwa kutumia sheria mbaya ya mitandao ya mitandao ya kijamii, kwa sababu tu ya kutoa maoni yao ambayo yako kinyume na Serikali. Yote haya ni rekodi mpya ya uvunjivu wa haki za wananchi nchini mnayopaswa kuikataa.

2. Ni ndani ya kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 5, ndipo utu umekosekana kabisa nchini, wananchi wanavunjiwa nyumba zao walizozijenga kwa jasho lao bila hata kulipwa fidia, huku hata mahakama zetu pamoja na Katiba ya nchi kutokuheshimiwa kwa Serikali kuvunja hata nyumba ambazo mahakama imeweka zuio, nyie Wanakijichi ni mashuhuda wa hili, ndugu zenu wa Kimara wamedhalilishwa kwa kuvunjiwa nyumba zao bila fidia na kurudishwa kwenye umasikini. Hali hiyo si Dar tu hapa, wananchi wanavunjiwa nyumba zao bila fidia mikoa mbalimbali nchini, hivi karibuni ni Tabora. Mnao wajibu wa kuwafuta machozi hawa, kwa kuhakikisha mnakikataa chama tawala.

3. Ni kipindi hiki pia ndio tumeshuhudia watu wanaouwawa hovyo hovyo hovyo tu, nanyi ni mashahidi hapa Dar, kila siku inaokototwa miili tu ya watu kule ufukweni Coco Beach, wakiwa wameuawa. Serikali haijawahi kusema chochote juu ya miili hiyo inayookotwa, tuna serikali isiyojali uhai wa watu wake. Si hilo tu, mbunge mwenzangu Tundu Lissu amepigwa risasi zaidi ya 30 zaidi ya mwezi mmoja sasa, mmesikia mtu yoyote amekamatwa kwa tukio hilo? Na msidhani wanaoathirika ni watu wa Upinzani tu, la hasha, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Ambaye ni CCM, amepotea tangu mwezi julai, mama mpaka leo hajapatikana. Kuinyima kura CCM ni kuonyesha uhai wa hawa watu una maana kwenu, ni kuonyesha mnajali.

4. Serikali hii imekataa kuwapa haki yenu ya kuwa na mchakato mpya wa Katiba Mpya, mchakato utakaoanzia kwenye maoni ya Tume ya Jaji Warioba, maoni yenu wananchi. Rais anasema kwa kiburi kuwa hakuwaahidi Katiba, na wapambe wake wanazunguka huku na huku kupinga uwepo wa mchakato wa Katiba mpya. Kukikataa chama tawala kwenye uchaguzi huu ni kukiambia kuwa mamlaka ya uongozi ni yenu nyie wananchi, na kwamba mnataka mchakato wenu wa Katiba uendelee.
 
Ktk kuumba ulimwengu Mungu aliumba mwanadamu kwa sura na mfano wake, wengine walimsaliti na kuwa binadamu wabaya, ndyo mashetani pamoja na kufanana kwa sura ila ni MASHETANI, mashetani wana himaya ya utawala, na wanataka kutawala hata wale walio wema kwa mabavu na udikteta, ukilegeza moyo kwa muumba wako shetani anakudaka na kuwa mtumwa wake, ndyo tz tunavyotawaliwa, ndvyo wenye kumsaliti mungu wanavyotawala wengine na kutaka wafanane nao, bashite keshavutwa na shetani mkuu na sasa ndo msaidizi wake mkuu, mungu uturehemu
 
Umenitoa machozi mkuu
 
bc9b0c28a4ab9cd63211870d554e9fc5.jpg
 
Ni serikali hii iliotoa amri mifugo ya nchi jirani ikiingia taifisha na kweli ikataifisha ngombe wa kenya 1,362 na kenya nao kwa hasira wamitaifisha ngombe 4,000 za Tanzania .na yote hii ni kukiuka makubaliano ya ujirani mwema yaliokuapo muda wote wa awamu zote 4
 
safi sana jamaa alivyo na roho mbaya kweli tunaangukia pua labda atajifunza kitu
 
Pole sana ndugu yangu. Wenye sura za kibinadamu siyo wote nchi hii.
 
Ktk kuumba ulimwengu Mungu aliumba mwanadamu kwa sura na mfano wake, wengine walimsaliti na kuwa binadamu wabaya, ndyo mashetani pamoja na kufanana kwa sura ila ni MASHETANI, mashetani wana himaya ya utawala, na wanataka kutawala hata wale walio wema kwa mabavu na udikteta, ukilegeza moyo kwa muumba wako shetani anakudaka na kuwa mtumwa wake, ndyo tz tunavyotawaliwa, ndvyo wenye kumsaliti mungu wanavyotawala wengine na kutaka wafanane nao, bashite keshavutwa na shetani mkuu na sasa ndo msaidizi wake mkuu, mungu uturehemu

Ni utawala uliokosa baraka za mungu ktk kutawala, ni utawala kama wa kaisari, ni utawala utakaoangamiza watu wake kwa kuwafanya waishi kama mashetani kwa kuwa nao ni mashetani, utawala usioleta furaha kwa watu wake hata katika familia zao kumejaa huzuni iliyo kuu. MUNGU TUOKOE NA MADHILA HII, EE BWANA W MAJESHI
 
Mungu akubariki sana mtu wa Mungu aliyehai
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom