OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,073
- 103,291
1. Utawala huu wa awamu ya 5 ndio utawala unaovunja haki za watu kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijawahi kuonekana nchini, ndani ya muda wake mfupi wa miaka miwili ya utawala huu, magazeti zaidi ya matatu yameshafungiwa sasa, magazeti yote hayo yalionekana kuwa mwiba kwa Serikali kwa kuhoji na kuandika mambo mbalimbali juu ya hali ya Nchi yetu. Si hilo tu, bado kuna zuio lisilo la kikatiba la Rais juu ya mikutano ya hadhara, huku mamia ya watu wakiwa wameshtakiwa, na wengine kuhukumiwa vifungo na faini, kwa kutumia sheria mbaya ya mitandao ya mitandao ya kijamii, kwa sababu tu ya kutoa maoni yao ambayo yako kinyume na Serikali. Yote haya ni rekodi mpya ya uvunjivu wa haki za wananchi nchini mnayopaswa kuikataa.
2. Ni ndani ya kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 5, ndipo utu umekosekana kabisa nchini, wananchi wanavunjiwa nyumba zao walizozijenga kwa jasho lao bila hata kulipwa fidia, huku hata mahakama zetu pamoja na Katiba ya nchi kutokuheshimiwa kwa Serikali kuvunja hata nyumba ambazo mahakama imeweka zuio, nyie Wanakijichi ni mashuhuda wa hili, ndugu zenu wa Kimara wamedhalilishwa kwa kuvunjiwa nyumba zao bila fidia na kurudishwa kwenye umasikini. Hali hiyo si Dar tu hapa, wananchi wanavunjiwa nyumba zao bila fidia mikoa mbalimbali nchini, hivi karibuni ni Tabora. Mnao wajibu wa kuwafuta machozi hawa, kwa kuhakikisha mnakikataa chama tawala.
3. Ni kipindi hiki pia ndio tumeshuhudia watu wanaouwawa hovyo hovyo hovyo tu, nanyi ni mashahidi hapa Dar, kila siku inaokototwa miili tu ya watu kule ufukweni Coco Beach, wakiwa wameuawa. Serikali haijawahi kusema chochote juu ya miili hiyo inayookotwa, tuna serikali isiyojali uhai wa watu wake. Si hilo tu, mbunge mwenzangu Tundu Lissu amepigwa risasi zaidi ya 30 zaidi ya mwezi mmoja sasa, mmesikia mtu yoyote amekamatwa kwa tukio hilo? Na msidhani wanaoathirika ni watu wa Upinzani tu, la hasha, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Ambaye ni CCM, amepotea tangu mwezi julai, mama mpaka leo hajapatikana. Kuinyima kura CCM ni kuonyesha uhai wa hawa watu una maana kwenu, ni kuonyesha mnajali.
4. Serikali hii imekataa kuwapa haki yenu ya kuwa na mchakato mpya wa Katiba Mpya, mchakato utakaoanzia kwenye maoni ya Tume ya Jaji Warioba, maoni yenu wananchi. Rais anasema kwa kiburi kuwa hakuwaahidi Katiba, na wapambe wake wanazunguka huku na huku kupinga uwepo wa mchakato wa Katiba mpya. Kukikataa chama tawala kwenye uchaguzi huu ni kukiambia kuwa mamlaka ya uongozi ni yenu nyie wananchi, na kwamba mnataka mchakato wenu wa Katiba uendelee.