Utawala usio haki na athari zake-machinga mbeya kielelezo cha mparaganyiko wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala usio haki na athari zake-machinga mbeya kielelezo cha mparaganyiko wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Nov 14, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jitihada za Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kupambana na wamachinga ili kuzuia vurugu hizo ziligonga mwamba kwa siku mbili mfululizo, na wakati wamachinga wakipambana, muda wote walikuwa wakiimba nyimbo za kumkataa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.

  Sugu ambaye alisafiri usiku kucha kutoka Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge, alifika jijini Mbeya majira ya saa 3:00 asubuhi na kwenda moja kwa moja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kuonana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kabla ya kuzungumza na wamachinga katika kituo cha daladala cha Kabwe kilichopo eneo la Mwanjelwa Mjini hapa.
  Akizungumza na maelfu ya wananchi pamoja na wamachinga waliojitokeza kwenye mkutano huo, Sugu alisema amekubaliana na viongozi wa Mkoa pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuwa wamachinga hao waendelee na shughuli zao kama kawaida katika maeneo waliyokuwa wakifukuzwa hadi pale Halmashauri ya Jiji itakapowapatia maeneo mazuri ya kufanyia biashara zao.

  "Tumekubaliana kuwa wamachinga waendelee na shughuli zao wakati Uongozi wa Halmashauri ya Jiji ukijiandaa kuja na mikakati itakayokubaliwa na wamachinga wenyewe juu ya kuwapatia eneo zuri la kufanyia biashara," alisema Sugu huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakimsikiliza.

  Sugu alisema pia wamekubaliana kuwaachia watu wote waliokamatwa na Polisi kuanzia juzi hadi jana kutokana na mapambano yaliyokuwa yakiendelea baina ya askari na wamachinga waliokuwa wakipinga kuhamishwa kwenye maeneo yao ya biashara.
  Alisema pia amekubaliana na viongozi wa Mkoa wa Mbeya kuwaondoa askari wote mitaani na kuwaacha wananchi wafanye shughuli zao kwa amani bila hofu kama ilivyokuwa zamani kabla ya kutokea kwa mapambano hayo.

  Source-IPPMEDIA
   
Loading...