Utawala katili wa dikteta Idd Amini Dada wa Uganda

wwww

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
350
252
Ebu tujikumbushe utawala wa dikteta aliyekuwa rais wa Uganda wakati ule. Rais ambaye alikuwa hapendi kabisa kukosolewa na mtu yeyote na yule aliyediriki kumkosoa alikiona cha mtema kuni. Ni kipindi ambacho wananchi wengi wa Uganda waliuwawa kikatili hasa wapinzani wa Serikali ya Idd Amini ambayo ilikuwa inaongozwa kwa mkono wa chuma.

Hiki ni kipindi ambacho mto Kagera uligeuka kaburi la Waganda wengi, miili yao iliyojaa majeraha na mingine isiyokuwa na baadhi ya wiungo ilionekana ikielea kila wakati. Utawala wa Idd Amini ulikuwa ni wa kikatili sana, watu wengi walipotea bila sababu na wengine kutoonekana kabisa. Watu walizikwa wakiwa hai.

Utawala huu ulijaa majivuno na wapambe waliojipendekeza kwa Idd Amini ndio waliopewa madaraka. Uteuzi wake haukuzingatia taaluma yoyote ila kumsifia tu na yeyote aliyemsifia alipewa zawadi ya kupewa cheo. Serikali yake haikufanya chochote cha maana zaidi ya kuvurugavuruga tu kila kona na kila kukicha. Serikali yake ilivuruga kabisa uhusiano na nchi nyingi duniani.

Hata hivyo utawala ule ulikatishwa kabla ya muda wake. Vita vya Tanzania na Uganda vilikatisha utawala wa Idd Amini kutawala nchi ya Uganda milele. Wateule wa Idd Amini waliumia sana kwani walikuwa wamezoea kujikweza na kuonekana Miungu watu ndani ya ardhi ya Uganda na Nje ya nchi hiyo. Mbaya zaidi hawa wateule walikuwa wanajipanga kubadilisha KATIBA ya nchi yao ili kuondoa kipengele cha ukomo wa Rais. Maadalizi ya awali yalikuwa yamekamilika ili kumuwezesha Idd Amini aweze kutawala milele ili na wao wanufaike milele.

Tujadili!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom