SoC02 Utawala Bora ni Uzalendo sio matokeo ya Siasa wala Diplomasia

Stories of Change - 2022 Competition

Jmmlelwa

New Member
Jul 31, 2022
1
0
Utawala bora tunaweza kusema ni namna ambavyo waliopewa dhamana wanaendendesha taasisi na shughuli za umma katika kusimamia rasilimali za umma, haki za binadamu kwa kuzinagatia sheria ambazo kama nchi imejiwekea likini siasa nikimnukuu moja kati ya platinum member wa jamii forum akimjibu swali Herbalist DR MziziMkavu JF- Expert Member mnamo 16November 2009 alisema siasa ni utekelezaji wa mkataba kati ya watawala na watawaliwa ambao msingi wake katiba.

Baada ya kulewa maana ya hivyo vote viwili ningependa tujiulize na tutafakali maswali kadhaa kwanini kumekuwa na kutowajibika kwa viongozi wetu? Kwa nini kumekua na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu? Kwa nini wakiukaji wakubwa wa katiba yetu ni viongozi na wanasia tunao waamini? Je hii si ishala ya wazi kua hakuna utawala bora?

Watawala wanatumia nguvu nyingi kujiimarisha kisiasasa na kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi, wapinzani nao wanatumi nguvu nyingi kupigania maslahi yao nyuma yama matatizo na changamoto za wananchi. Hivi sasa kuna vuguvugu la katiba mpya jambo ambalo ni jema lakini kwa bahati mbaya ukiwasikiliza kwa makini wanaopigania katiba mpya unagundua kuwa wamebeba maslahi ya kisiasa yatakayowahakikishia wao nafasi ya ushindi rahisi katika siasa na wametupilia mbali maslahi ya wananchi licha ya kuwa ndio wanatumika kama sababu ya mapigano yao.

Kiongozi na mwanasiasa
Katika namna iliyo njema tulipaswa kuwatizama watu hawa kiongozi na mwanasiasa kwa namna tofauti lakini ni tofauti kabisa sisi tuna waona kam kitu kimoja na hasa tukimpendele mwanasiasa bora kwa kumvisha taji la kiongozi bora. Kisha tumeweka mfumo mgumu ambao haumruhusu kiongozi bora kuingia katika nafasi, ukitizama namna ambavyo viongozi wetu wanawajibika unaweza pata mtazamo halisi juu ya hili, kumekuwa na kuteuliwa na kutenguliwa kwingi sana hii ni kwasababu walio kwenye mfumo si viongozi ni wanasisa.


Upinzani na utawala bora

Wapinzani ni nyenzo muhimu kusukuma utawa bora lakini kami si uzalendo miongoni mwa wapinzani basi upinzani ni nyenzo ya kubomoa utawala bora na kuvuruga amani ya nchi. Mfano mzuri kwa nchi zetu za afrika upinzani ndio wamekua wahalifu wakubwa wa amani wakijaribu kutunishia misuri watawala kwa kutumia ushawishi wa umma walio nao na kwa kutumia silaha wakati mwingine ambapo wanaenda kuvuga amani ya nchi na kuathiri wananchi.

Mataifa yenye nguvu na utawala bora
Katika kile mataifa yenye nguvu yanakiita misaada, mkipo, usimamizi wa demokrasia na vingine vingi vimekuwa vikiweka Afrika na Tanzania katika wakati dumavu kimaendeleo. Wamefanikiwa kukamata akili za watu na hasa wanasiasa ambao ndio tunawapa dhamana ya uongozi katika nchi zetu tunaweza sema (ukoloni mamboleo) hii imefanya viongozi wetu kuamini maamuzi wapewayo na mataifa mengine yenye nguvu ambayo kwa namna moja au nyingine yaliwafanya wendelee katika jamii zao lakini wanasahau kuwa hali ya kijamii, kihistoria na hata rasilimali ni tofauti kabisa hivyo tunapaswa kutafuta namna sahihi ya kuamua kutokana na hali zetu

Matifa yenye nguvu yamekuwa yakiwapa nguvu wanasiasa wa upinzani wema na wabaya kwa maslahi yao wenyewe ikiwa wanasiasa hao watashika dola mbeleni.

Kwanini uzalendo haupo
Hakuna asiejua kuwa anawajibu wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria na taratibu, sote tunajua hilo lakin bado kuna changamoto kubwa sana katika hili. Binfsi nafikili kuna sababu kazaa za kiuchumi na kijamii, nikianza na sababu za kiuchumi, ni kwamba wengi wetu tunatamani kutoka katika dimbwi la umasikini nap engine kua na uwezo mkubwa wa kifedha hivyo kufanya watu kutoridhika na mishahara yao kama ambavyo kitabu kitakatifu kituoagiza kutosheka na mishahara yetu katika luka 3:14. Likini pia inaweza kuchochewa na masuala ya kijamii kama mmomonyoko wa maadili nk.

Juzi juzi tuneona namna ambavyo wanachma wa chama kimoja cha upinzani walikiuka katiba na makakubaliano wakilindwa na speaker wa bunge kimakosa unajiuliza? Nini kiliwasukuma juu ya kiburi hiki ili hali ni wanasiasa ambao jamii ilikua ikiwaamini juu ya weledi wao? Labda kuna mengine lakini nafikiri jua ya maslahi binafsi wala si ya taifa ama chama chao.

Nini kifanyike
Ni vigumu ku dhibiti urafi katikati ya watu wenye njaa kali nay a mda mlefu na pia sehemu nyenye tofauti kubwa kati ya wenye nacho na wasio nacho, katika hili kuna kiongozi mmjoja alionekana kua na mwelekeo mzurii licha ya mapungufu yake. Itakua vigumu pia kufikia utwala bola pasipo kuimalisha jamii zetu ki maadili, tukifanikisha hayo sasa tufikilie namna bora ya kuhakikisha watawala wanawajibika kwa kadri watakiwavyo na si watakavyo na ili kufanikisha hili tunao wajibu katika ya fuatayo;

Kuchagua viongozi sahihi na si wanasisa kwa nguvu na ushawishi wao juu ya vyama vya siasa watokavyo
Kuwa na katiba inayo mbana yeyote wenye mmlaka kuwajibika bila kujali nafasi yake kwa watawala wa juua au katika jamiii

Uzalendo pia linaweza kuwa jambo ambalo lipo mikononi mwetu tukiamua kua wazalendo basi tuaweza ni wajibu wetu kulijenga taifa, vijana wengi ndio tutakao kua viongozi wakesho basi tukasimamie haki

Mgawanyo wa mamlaka ni muhimu sana si kazi lahisi mtu mmoja au wachache kufanya maamuzi ya watu zaid ya million 60 mfano rais wananchi ana mamlaka ya kuteua watu zaid ya 200 hii ni vigumu kuteua watu wanaofaa, ataishia kuteua watu wanaonekana hasa wanasisa kwenye majukwaa

Hitimisho: Kamwe siasa haita tupa utawala bora tuwekeze katika uzalendo japo kuwa tuanaweza kua tumechelewa lakini kama mti ukuavyo na Imani tunaweza kuumwagiria taritibu na ukazaa matunda hata kama hatuta nufaika nayo sisi basi vizazi vijavyo vinufaike.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom