Utawala bora na nidhamu ya chama cha CPC ni mifano ya kuigwa na Afrika kukabili masikini na ufisadi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Utawala bora na nidhamu ya chama cha CPC ni mifano ya kuigwa na Afrika kukabili maskini na ufisadi

Kulingana na takwimu za benki ya dunia, mwaka 1960 China ilikuwa maskini kuliko baadhi ya nchi barani Afrika.

Kwa mfano mwaka 1960, mgao wa pato la kitaifa kwaChina ulikuwa dola 89 tu, wakati DR. Congo ulikuwa dola 220, Kenya dola 97, Afrika Kusini 433 na Ghana 183.

Lakini ifikapo mwaka 2017 mgao huo kwa China ulikuwa umefikia dola 8,827, huku Kenya ikiwa na dola 1,507, Ghana 1,641, Afrika Kusini 1,615.

Mwaka 1978 China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji , matunda ya juhudi za kukuza uchumi na kuondoa umaskini yanaonekana wazi. Mnamo mwaka 2010, Pato la Taifa la China (GDP) lilizidi Japani na kuwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Ifikapo mwaka 2019, Pato la Taifa la kila mtu la China limeongezeka kufikia dola za Kimarekani 10,276.

Mapema mwaka 2021 Rais wa China Xi Jinping alitangaza kuwa serikali imefanikiwa kuondoa watu wote katika umaskini uliokithiri, ikiwa ni mbele ya ratiba iliowekwa.

Sasa nchi nyingi za Afrika zimeanza kuona kuwa mfumo wa China wa kupata maendeleo na kukabiliana na umaskini unafaa zaidi.

Mafanikio ya kipekee ya kiuchumi na kisiasa ya China yanaweza kutajwa kama "muujiza wa Wachina," ambayo nchi za Kiafrika zina mengi ya kujifunza, anasema katibu mkuu wa chama tawala nchini Kenya cha Jubilee Raphael Tuju.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Ufuatiliaji na Utafiti wa Sera nchini Zambia Bernadette Deka-Zulu, anasema sera ya serikali ya China ya kuwapa kipaumbele wananchi kwenye mipango yake ya maendeleo ndio imesaidia pakubwa kuondoa umaskini.

“Haishangazi kwamba China imeweza kuwaondoa mamia ya mamilioni ya wakazi wake wa vijijini kutoka kwa umaskini kutokana na njia ya maendeleo ambayo inaweka watu mbele”, anasema Deka-Zulu.

CPC imekuwa injini ya maendeleo na mafanikio ya kutokomeza umaskini

Kwa sasa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimetimiza miaka mia moja tangu kibuniwe.

Kwa viongoni na watu wa China CPC imekuwa ni kama gari la kusafirisha ndoto zao za maendeleo na mafanikio ya jamii yenye ustawi na hatma ya pamoja mwaka hadi mwaka.

Kwa chama kimoja kutimiza miaka 72 kwenye uongozi wa taifa pia ni muujiza mwingine.

Lakini muujiza huo Raphael Tuju anasema, haungewezekana bila kuwepo na nidhamu.

"Lazima utoe sifa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kufanikiwa kuongoza nchi kwa nidhamu na kwa umakini ambazo zimewawezesha kufanikisha muujiza wa Wachina", anasema Tuju.

Akibainisha njia bora ambayo China inakuza uchumi wake, anasema kuwa kuna mengi ambayo Afrika inaweza kujifunza kutoka kwa "muujiza wa Wachina," mojawapo ni kuwa na nidhamu kama ilivyo ndani ya CPC.

Kenya pia inaweza kujifunza kutokana na mafanikio ya China katika kupunguza umaskini. "Hakuna mfano katika historia ya ulimwengu ambapo watu wengi wameondolewa kwenye umasikini ndani ya muda mfupi kama vile tumeona nchini China," anasema.

Hata hivyo anasema mchakato wa kujifunza na kufanikiwa ni mrefu.

"Ufanisi hauwezi kupatikana mara moja. Tunajifunza kutoka kwa baadhi ya mifumo ambayo tulishuhudia wakati tulipotembelea China," anasema Tuju.

CPC pia imekuwa dhabiti katika kuadhibu wanaohusika na ufisadi bila kujali vyeo au ngazi kwenye serikali.

Maofisa wa juu kwenye chama wanaohusika na ufisadi wanashatikwa kwa mujibu wa sheria, hali inayoongeza imani ya wananchi katika CPC.

Deka-Zulu anapongeza jukumu muhimu la Chama cha Kikomunisti cha China katika kupambana na rushwa na athari zake katika ajenda ya maendeleo ya China, na kuongeza kuwa juhudi za vita dhidi ya ufisadi kwa mikoa yote pia kumehakikisha kuwa maendeleo yanafika sehemu kamili zinazolengwa.

Mafanikio ya China yamesambaa kote duniani kimkakati

Mwaka 2020 Kituo cha Uchumi na Utafiti wa Biashara cha Uingereza ambacho kinatoa ushauri wa uchumi kilitangaza kuwa uchumi wa China unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi duniani ifikapo mwaka 2028.

Ufanisi huo wa kiuchumi unamaanisha kuwa jukumu la China kwenye maswala ya dunia pia yataongezeka.

Lakini mbele ya kufikia mwaka 2028 tayari ukuaji wa haraka wa kiuchumi wa China umeleta matumaini ya ukuaji wa hatma ya pamoja kwa kusaidia nchi nyingi barani Afrika kukuza uchumi wao.

Chini ya miradi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) ilioanzishwa mwaka 2013 nchi nyingi zimepata miradi inayotekelezwa kwa mikopo nafuu kutoka China kama vile reli, bandari na viwanja vya ndege.

Miundo mbinu yote hiyo inaendana na mahitaji halisi ya nchi za Afrika ili kuzisaidia kukuza biashara, uunganishaji na uchumi.

Cavince Adhere, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa anasema Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama chombo bora cha kuchochea maendeleo ya pamoja kote duniani.

Anasema kuwa nguzo muhimu za BRI ikiwa ni pamoja na uratibu wa sera, maendeleo ya miundombinu, uwezeshaji wa biashara na ubadilishanaji wa watu kwa watu zinaleta picha kamili ya ushiriki wa moja kwa moja wa China kwenye maswala ya dunia.

"Nimefurahi kuona kuwa China sasa inapendekeza njia mpya za utekelezaji wa Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama ujenzi wa ushirikiano ikimaanisha kuwa nchi zinazoshiriki lazima ziwe na maoni, habari na kuchangia fedha, katika utekelezaji wa mradi huu, "anasema Adhere.

Kwa kuzingatia miradi hiyo ya BRI na mabadilishano ya mara kwa mara kati ya maafisa wa serikali za Afrika na China sasa ni wazi kuwa mwanya wa kufikia hatma ya pamoja ya binadamu utaendelea kupungua siku hadi siku.
 
Watanzania hawa ambao usipowapandishia mshahara tu wanapiga kelele hatar ndo wataweza kufunga mkanda kwajili yakujenga nchi yao? Watanzania ni wavivu wakufanya kazi temebarikiwa maneno mengi tu na kujidai tunataka demokrasia na uhuru wa kujieleza wakati ata ao wamagharibi wenyewe walijenga nchi zao zikasimama vyema wakati hamna haki za binadamu wala demokrasia.
 
Kweli wanalia Sana watanzania.. lakini vilio vyao Ni vilio vya machozi ya thamani! Wanalia kwa mengi, mbona kazi wanafanya sana? Je unadhani Ni wavivu? Laah!

Kazi wazifanyazo Ni kubwa mno, wengine ni wakulima, wengine wafugaji, wengine waalimu! Zote kazi ngumu lakini maslahi ni punje tu ndani ya zao walizalishalo! Wanyonyaji Ni wengi!

Mtumishi ajituma Sana daraja hapandishwi eti tunajenga taifa! Siku si nyingi anaskia mwenzaje kakwapua Bilioni 3.6 na anadunda? Kweli asilie? Afurahi tu?

Shida zote hajazubaa anaambiwa shilingi Bilioni 400± hivi Ni hasara kutokana na uzembe wa mradi wa ndege ziso faidA!
Kweli acheke?
 
Kusema kweli mfumo wa demokrasia hauja zisaidia nchi za Africa hata kidogo.

Kama ikiwezekana tuende wa China,ila naamini nchi za magharibi haziwezi kukubari na tukikomaa tutapigwa kama Ghadafi.

Kwani nchi za magharibi huwaga wanatumia demokrasia hii hii kuchomeka watu wao kwa ajili ya maslai yao.Halafu mara nyingi masnitch na mamluki wanakuwa wengi.
 
Umeongea ukweli.. wenyewe walijenga nchi zao wakiwa hawana hii mufumo wanayotumezesha sisi tuiige kwao ila sisi vyakuletewa ndo tumevikomalia kama nini... utashangaa leo mtumishi analalamikia nyongeza za mishahara ila ukimuambia jitoe kwanza tujenge nchi ya vizazi vijavyo ata hakuelewi.. kizazi hiki cha sasa sidhani kama kingeweza kudai uhuru kwakweli.
 
Utawala bora na nidhamu ya chama cha CPC ni mifano ya kuigwa na Afrika kukabili maskini na ufisadi

Kulingana na takwimu za benki ya dunia, mwaka 1960 China ilikuwa maskini kuliko baadhi ya nchi barani Afrika.

Kwa mfano mwaka 1960, mgao wa pato la kitaifa kwaChina ulikuwa dola 89 tu, wakati DR. Congo ulikuwa dola 220, Kenya dola 97, Afrika Kusini 433 na Ghana 183.

Lakini ifikapo mwaka 2017 mgao huo kwa China ulikuwa umefikia dola 8,827, huku Kenya ikiwa na dola 1,507, Ghana 1,641, Afrika Kusini 1,615.

Mwaka 1978 China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji , matunda ya juhudi za kukuza uchumi na kuondoa umaskini yanaonekana wazi. Mnamo mwaka 2010, Pato la Taifa la China (GDP) lilizidi Japani na kuwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Ifikapo mwaka 2019, Pato la Taifa la kila mtu la China limeongezeka kufikia dola za Kimarekani 10,276.

Mapema mwaka 2021 Rais wa China Xi Jinping alitangaza kuwa serikali imefanikiwa kuondoa watu wote katika umaskini uliokithiri, ikiwa ni mbele ya ratiba iliowekwa.

Sasa nchi nyingi za Afrika zimeanza kuona kuwa mfumo wa China wa kupata maendeleo na kukabiliana na umaskini unafaa zaidi.

Mafanikio ya kipekee ya kiuchumi na kisiasa ya China yanaweza kutajwa kama "muujiza wa Wachina," ambayo nchi za Kiafrika zina mengi ya kujifunza, anasema katibu mkuu wa chama tawala nchini Kenya cha Jubilee Raphael Tuju.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Ufuatiliaji na Utafiti wa Sera nchini Zambia Bernadette Deka-Zulu, anasema sera ya serikali ya China ya kuwapa kipaumbele wananchi kwenye mipango yake ya maendeleo ndio imesaidia pakubwa kuondoa umaskini.

“Haishangazi kwamba China imeweza kuwaondoa mamia ya mamilioni ya wakazi wake wa vijijini kutoka kwa umaskini kutokana na njia ya maendeleo ambayo inaweka watu mbele”, anasema Deka-Zulu.

CPC imekuwa injini ya maendeleo na mafanikio ya kutokomeza umaskini

Kwa sasa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimetimiza miaka mia moja tangu kibuniwe.

Kwa viongoni na watu wa China CPC imekuwa ni kama gari la kusafirisha ndoto zao za maendeleo na mafanikio ya jamii yenye ustawi na hatma ya pamoja mwaka hadi mwaka.

Kwa chama kimoja kutimiza miaka 72 kwenye uongozi wa taifa pia ni muujiza mwingine.

Lakini muujiza huo Raphael Tuju anasema, haungewezekana bila kuwepo na nidhamu.

"Lazima utoe sifa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kufanikiwa kuongoza nchi kwa nidhamu na kwa umakini ambazo zimewawezesha kufanikisha muujiza wa Wachina", anasema Tuju.

Akibainisha njia bora ambayo China inakuza uchumi wake, anasema kuwa kuna mengi ambayo Afrika inaweza kujifunza kutoka kwa "muujiza wa Wachina," mojawapo ni kuwa na nidhamu kama ilivyo ndani ya CPC.

Kenya pia inaweza kujifunza kutokana na mafanikio ya China katika kupunguza umaskini. "Hakuna mfano katika historia ya ulimwengu ambapo watu wengi wameondolewa kwenye umasikini ndani ya muda mfupi kama vile tumeona nchini China," anasema.

Hata hivyo anasema mchakato wa kujifunza na kufanikiwa ni mrefu.

"Ufanisi hauwezi kupatikana mara moja. Tunajifunza kutoka kwa baadhi ya mifumo ambayo tulishuhudia wakati tulipotembelea China," anasema Tuju.

CPC pia imekuwa dhabiti katika kuadhibu wanaohusika na ufisadi bila kujali vyeo au ngazi kwenye serikali.

Maofisa wa juu kwenye chama wanaohusika na ufisadi wanashatikwa kwa mujibu wa sheria, hali inayoongeza imani ya wananchi katika CPC.

Deka-Zulu anapongeza jukumu muhimu la Chama cha Kikomunisti cha China katika kupambana na rushwa na athari zake katika ajenda ya maendeleo ya China, na kuongeza kuwa juhudi za vita dhidi ya ufisadi kwa mikoa yote pia kumehakikisha kuwa maendeleo yanafika sehemu kamili zinazolengwa.

Mafanikio ya China yamesambaa kote duniani kimkakati

Mwaka 2020 Kituo cha Uchumi na Utafiti wa Biashara cha Uingereza ambacho kinatoa ushauri wa uchumi kilitangaza kuwa uchumi wa China unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi duniani ifikapo mwaka 2028.

Ufanisi huo wa kiuchumi unamaanisha kuwa jukumu la China kwenye maswala ya dunia pia yataongezeka.

Lakini mbele ya kufikia mwaka 2028 tayari ukuaji wa haraka wa kiuchumi wa China umeleta matumaini ya ukuaji wa hatma ya pamoja kwa kusaidia nchi nyingi barani Afrika kukuza uchumi wao.

Chini ya miradi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) ilioanzishwa mwaka 2013 nchi nyingi zimepata miradi inayotekelezwa kwa mikopo nafuu kutoka China kama vile reli, bandari na viwanja vya ndege.

Miundo mbinu yote hiyo inaendana na mahitaji halisi ya nchi za Afrika ili kuzisaidia kukuza biashara, uunganishaji na uchumi.

Cavince Adhere, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa anasema Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama chombo bora cha kuchochea maendeleo ya pamoja kote duniani.

Anasema kuwa nguzo muhimu za BRI ikiwa ni pamoja na uratibu wa sera, maendeleo ya miundombinu, uwezeshaji wa biashara na ubadilishanaji wa watu kwa watu zinaleta picha kamili ya ushiriki wa moja kwa moja wa China kwenye maswala ya dunia.

"Nimefurahi kuona kuwa China sasa inapendekeza njia mpya za utekelezaji wa Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama ujenzi wa ushirikiano ikimaanisha kuwa nchi zinazoshiriki lazima ziwe na maoni, habari na kuchangia fedha, katika utekelezaji wa mradi huu, "anasema Adhere.

Kwa kuzingatia miradi hiyo ya BRI na mabadilishano ya mara kwa mara kati ya maafisa wa serikali za Afrika na China sasa ni wazi kuwa mwanya wa kufikia hatma ya pamoja ya binadamu utaendelea kupungua siku hadi siku.
Hii mada ingefaa ikae jukwaa la siasa mkuu
 
Mkuu Nyani na wenzie umewachoma kwelikweli, huko waliko sijui wana hali gani
 
Kusema kweli mfumo wa demokrasia hauja zisaidia nchi za Africa hata kidogo.

Kama ikiwezekana tuende wa China,ila naamini nchi za magharibi haziwezi kukubari na tukikomaa tutapigwa kama Ghadafi.

Kwani nchi za magharibi huwaga wanatumia demokrasia hii hii kuchomeka watu wao kwa ajili ya maslai yao.Halafu mara nyingi masnitch na mamluki wanakuwa wengi.

Hapa najiuliza..

Hivi nchi kama Uganda, Burkina faso au Congo ambazo zimetawaliwa na mtu mmoja kwa muda mrefu, zina maendeleo gani ambayo tunaweza kusema ni model kwa nchi nyingine kama Tanzania

Hivi hii Tanzania yetu yenye skendo kama EPA, Escrow na hapa juzi bandarini, zikiachiwa free bila upinzani kama watch dogs. Yatafanyika mangapi bro
 
Vizuri sana. Tuwekee na idadi ya watu waliokufa kwa mamilioni kwenye hiyo michakato. Kule kuna watu wako monitored kwa sababu za kijinga tu. Makanisa yanabomolewa. Kawaulize Waislamu wa Uyghur wakusimulie.

Bongo bado sehemu bora kabisa kuishi. Tunasogea taratibu ila natamani tubakie bila chembe ya mifumo ya hawa jamaa.

Ukomunisti ni mfumo mbaya sana, hata uupake rangi kiasi gani!
 
Hapa najiuliza..

Hivi nchi kama Uganda, Burkina faso au Congo ambazo zimetawaliwa na mtu mmoja kwa muda mrefu, zina maendeleo gani ambayo tunaweza kusema ni model kwa nchi nyingine kama Tanzania

Hivi hii Tanzania yetu yenye skendo kama EPA, Escrow na hapa juzi bandarini, zikiachiwa free bila upinzani kama watch dogs. Yatafanyika mangapi bro
Imetawaliwa na mtu mmoja kweli,ila sizani kama waliendesha ktk mifumo kama ile ya China.China pamoja na kuongozwa na mtu mmoja wana mifumo mizuri ya kuwajibisha viongozi wao na ndio maana leo hii wapo hapo.

Nakupa mfano Malawi,Zambia,Kenya,Nigeria hizi nchi zimebadilisha viongozi kutoka vyama mbalimbali,lkn story ni zilezile.Tena kama Kenya wamebadilisha na katiba mpya lkn Rushwa na Ufisadi umetamalaki.

Yaani kama kuna uwezekano nchi za Africa tunge copy na kupaste mfumo wanao tumia China kuendesha nchi yao,hii demokrasia haija tusaidia ndio ukweli wenyewe.

Au nitajie nchi moja tu ya Africa unayo weza kusema imepiga hatua kubwa kimaendeleo sababu ya Demokrasia.Yaani nikitizama South Africa madudu walikokuwa nayo mpaka unachoka,Nigeria na mafuta yao nao hovyo ,hizi ni nchi za Africa zilizokuwa na uchumi lkn ukizitizama kila siku zinazidi kuteteleka.
 
Yaani kama kuna uwezekano nchi za Africa tunge post na kupaste mfumo wanao tumia China kuendesha nchi yao,hii demokrasia haija tusaidia ndio ukweli wenyewe.

Au nitajie nchi moja tu ya Africa unayo weza kusema imepiga hatua kubwa kimaendeleo sababu ya Demokrasia.Yaani nikitizama South Africa madudu walikokuwa nayo mpaka unachoka,Nigeria na mafuta yao nao hovyo ,hizi ni nchi za Africa zilizokuwa na uchumi lkn ukizitizama kila siku zinazidi kuteteleka.
Kwani kwa hao wenye mifumo unayodai rushwa haipo au wameweza kuzuia habari?
 
Rushwa na ufisadi huwezi zizuia bali utapunguza.Hata wakikamatwa wanawajibishwa tena kwa adhabu kali.

Nakupa mfano tz watu wengi mnakitizama chama tawala,ila mimi nishavipima vyama vyetu vya upinzani.Sijajua ripoti ya mwaka huu ya CAG lkn mara zote vyama vya upinzani hivi vyenye wafuasi wengi vinapata hati chafu.Sasa unajiuliza kama unashindwa kuwa mwaminifu kwa hiki kidogo wakipatacho vipi tukiwapa nchi?.
Hiyo haitoshi wanashindwa kusimamia misimamo yao,nazani uliona swala la Lowasa mtu miaka mitano mnamtangaza ni fisadi na tena unatamka kwa kinywa chako ushahidi unao,alafu ndani ya dk 5 unamsafisha na kumfanya mgombea anaye kiwakilisha chama chako,ujue kwa mtu makini sana lazima uone kuna walakini.Sababu kama unayakana maneno ya tokayo kinywani mwako,basi kuna siku tukikupa nchi hutosita kukataa maneno yako na utaisaliti nchi yako.

Sawa hata wakiviruhusi vyombo vya habari,haviwezi kubadili number zinazo wabeba kiuchumi,ujue mpaka sasa US mwenyewe pamoja na vikwazo anavyo mwekea China kila siku inazidi kupasua hanga na haya maneno si yangu hata wachumi manguli duniani wameongea kwa fact kwamba China uchumi wake unakua kwa kasi.Wachina tukubali tukatae wapo serious na maendeleo ya nchi yao hawataki ujinga ujinga.
 
Imetawaliwa na mtu mmoja kweli,ila sizani kama waliendesha ktk mifumo kama ile ya China.China pamoja na kuongozwa na mtu mmoja wana mifumo mizuri ya kuwajibisha viongozi wao na ndio maana leo hii wapo hapo.

Nakupa mfano Malawi,Zambia,Kenya,Nigeria hizi nchi zimebadilisha viongozi kutoka vyama mbalimbali,lkn story ni zilezile.Tena kama Kenya wamebadilisha na katiba mpya lkn Rushwa na Ufisadi umetamalaki.

Yaani kama kuna uwezekano nchi za Africa tunge copy na kupaste mfumo wanao tumia China kuendesha nchi yao,hii demokrasia haija tusaidia ndio ukweli wenyewe.

Au nitajie nchi moja tu ya Africa unayo weza kusema imepiga hatua kubwa kimaendeleo sababu ya Demokrasia.Yaani nikitizama South Africa madudu walikokuwa nayo mpaka unachoka,Nigeria na mafuta yao nao hovyo ,hizi ni nchi za Africa zilizokuwa na uchumi lkn ukizitizama kila siku zinazidi kuteteleka.

Mkuu bhasi tatizo ni watu wenyewe na sio mfumo.
China inakuwa kwa sababu system ipo imara kudhibiti mianya ya rushwa na ufisadi pasipo kusahau kuwa watu wake wanafanya kazi na wanapewa support katika uvumbuzi wao..

Hivyo hata Tanzania tukiondoa mifumo ya kutowawajibisha viongozi na kulea lea ufisadi pasipo kusahau, kutengeneza mazingira wezeshi ya kibiashara, uwekezaji, kazi na teknolojia kwa wananchi wazawa. Nadhani tutafika mbali tu

kuhusu democratic state nadhani Ghana yaweza kuwa ideal na bado ni chumi inayokua kwa kasi Africa wakiwa na demokrasia yao.. "mfumo upo vizuri"

kingine usidate na Figures za pato la taifa tu ukasema Nigeria ni uchumi mkubwa bila kutumia Vigezo vingine kama Human development index , ambayo inapima huo ukubwa kama unaakisi maisha ya wananchi kwa kiasi kikubwa

usishangae Mauritius, Botswana na hata Ghana wakaizidi Nigeria ambayo uchumi wake unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mafuta ambayo yanafaidisha wanaijeria wachache na makampuni ya kigeni... Huku wananchi wa chini wakiendelea kuinjoi power cuts
 
Back
Top Bottom