Yanatengenezwa mazingira kuja kuwalipa mabilioni fisadi

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,406
7,188
Kuna hofu kwa raia wazalendo kwamba kuachiwa na dpp watuhimiwa wa ufisadi kunakotokea sasa bila kuhusishwa mahakama huenda kukapelekea madai ya mabilioni toka hazina kuu ya taifa.

Tuhuma kuhusiana na IPTL ya harbinder sighn na rugemalila ziliwekwa wazi. Tangu wahujumu hao kutupwa lupango tanesco ilitulia na matumizi na utendaji wa shirika lililokua linatoa mabilioni kwa hila ukaboreka.

Wananchi wangependa kujua kama rugemalira ameonekana hana hatia au ameachiwa vipi. Mfanyabiashara mkubwa hivyo kumzuia lupango miaka minne bila kosa gharama yake akidai hakika ni mabilioni. Umma tuliyoamini ni fisadi tuelezwe kama kuna maafikiano ya kuachiwa. Kama ni ubinadamu tu au amerejesha thamani aliyofisidi tujue.

Isije ikawa awamu ya 6 inatengeneza mazingira ya fisadi waliyoshughulikiwa awamu ya 5 kuweza kufisidi tena umma kwa kudai fidia serikali baada ya kuachiwa. Tumeona pia waziri wa nishati akibadilishwa isije kua maandalizi ya kutia chumvi juu ya kidonda.
 
Kwani awamu ya iliwakuta na hatia?

Ikiwa aliyewakamata mpk kaondoka alishindwa kuthibitisha makosa yao ss mama afanyeje!
 
January ndo kichaka cha kubariki ufisadi mpya mkuu. Sijuhi nn hatma ya pampu za mafuta pale bandarini, ewura na uchakachuaji mafuta. Escrow na richmond vinatizamiwa upya na utitiri wa vituo vya lake oil kila baada ya 10km. Ichukue hii mkuu
 
Kwani awamu ya iliwakuta na hatia?
Ikiwa aliyewakamata mpk kaondoka alishindwa kuthibitisha makosa yao ss mama afanyeje!
siku mkija kujua wanaowarudisha nyuma wanatumia udhaifu wenu mtakuwa mmesaidika sana.

sheria ni wembe,ila wajanja wanapakaa mafuta,wapumbavu wanashangilia ujanja huo.
 
January ndo kichaka cha kubariki ufisadi mpya mkuu. Sijuhi nn hatma ya pampu za mafuta pale bandarini, ewura na uchakachuaji mafuta. Escrow na richmond vinatizamiwa upya na utitiri wa vituo vya lake oil kila baada ya 10km. Ichukue hii mkuu
Umesema kitu mkuu. Tungojee kuona
 
Back
Top Bottom