Utatuzi wa wamachinga ilikuwa ni kuwatoza kodi. Hiyo ndo ingeleta Win-Win kwa machinga na Serikali

Sheria zipo zifuatwe...

Machinga watembeza matenga mabegi waendelee na umachinga wao sehemu zinazoingilia bila Trespassing.

Wafanyabiashara wengine wafanye biashara kwenye maeneo yanayoruhusiwa / yametengwa, wajitahidi hata kuungana wachukue fremu.

Kodi hakuna anayependa kulipa ni Sheria kwahio wao na wengine wote tutake tusitake tutazitoa tu labda wale watembeza bidhaa kwenye mabegi / matenga maofisini bila trespassing.

Sidhani kama kwa nchi yetu the only option ya kujipatia mkate wa kila siku ni kuchuuza, ukiona huku hakuna opportunity jaribu pale..., ukizingatie walio juu hawana msaada wowote...

 
Nimekuja kuona kumbe machinga walivyokuwa maeneo ya mijini walikuwa wanapata chochote kwa urahisi kwa sababu walikuwa scattered, mfano Bagamoyo road; walikuwepo kuanzia Mwenge, Tangi bovu, Afrikana, Mbuyuni, hadi Tegeta, hapa utaona hawa walikuwa wanagawana riziki zao.

Kitendo cha kuwakusanya wote hao na kuwapeleka sehemu moja wakafanyie biashara zao mfano Bunju, hapa tayari patakuwepo na kugombania wateja na mostly naamini kipato chao cha siku wengi kitapungua na umasikini utaongezeka.

Nachokiona sasa, baadhi yao wameamua kuweka mabanda yao katikati ya mitaa, kwenye njia za ndani sio main road, ili angalau waendelee kubaki karibu na yale maeneo waliyokuwepo mwanzo yenye wateja wao, hivyo tutegemee baada ya muda mfupi, njia za kwenye mitaa nazo zitakuwa hazipitiki kwa urahisi, machinga watahamia huko.

Solution yako ya kukusanya kodi ni nzuri, lakini hujasema hiyo kodi itakusanywa kwa mtindo upi, kama ni ule wa Magufuli na zile elfu ishirini ambazo mwisho wa siku kelele zilikuwa zinapigwa pesa haijulikani zinakwenda wapi naona ule ulifeli.

Lakini pia, muhimu zaidi watafutiwe sehemu sahihi za kufanya biashara zao ili iwe rahisi kwa serikali kukusanya hizo kodi, mfano kule Machinga complex, kuna vizimba havina watu miaka yote kwasababu hapakuwepo na wateja wafanyabiashara wakapakimbia.
Wajiunge wapangishe fremu

Hii ya kutafutiwa wote watapata?.
Serikali itakutafutia fremu?
Hata km ni vizimba lazima ufate utaratibu wa Soko
 
Back
Top Bottom