SoC01 Utatuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta ya Ustawi wa Jamii

Stories of Change - 2021 Competition

NICOLAUS NGILIULE

New Member
Jul 15, 2021
0
0
USTAWI WA JAMII ni sekta ambayo inadili na uangalizi na utoaji wa huduma stahiki kwa Makundi maalumu ya watu kama vile walemavu, wasiojiweza, wazee, watoto na familia Zisizojiweza, huduma zitolewazo ni kama vile utoaji wa huduma za afya, huduma za vyakula, kuwapa Elimu,na hata malazi na mahitaji mengineyo.

Sekta hii imekuwa chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa muda mrefu na imekuwa kuwa Ikisaidiwaa na Wizara hiyo katika utatuzi wa changamoto mbalimbali, kwa makundi hayo maalumu Ili kuweza kupunguza madhara yatokanayo endapo kutakuwa na ukosefu wa baadhi ya huduma, kwa mfano kupunguza magonjwa kama vile Udumavu na utapiamlo kwa watoto waishio katika Familia za hali ya chini. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zikitumika na wa na Jamii wenyewe.

Kwa kushirikiana na Sekta husika pamoja na wizara zinaweza kusaidia kuondoa changamotooo Mbalimbali nakuifanyaa jamii katika makundi hayo maalumu kuishi katika hali stahiki ya kimaisha.

UTOAJI WA ELIMU
Elimu juu ya ustawi wa jamiii inatakiwaa kutolewa kwa kina ilikuiwezesha Jamii kuwa nauelewa juu wa makundi haya maalumu mfano kuwa na uelewa Kuwa ni wajibu wa jamii kuwa uangalizi wa wazee na kuwatunza nakuwapa Mahitaji yao muhimu kama vile malazi, chakula,na mavazi na huduma bora za Afya na hivyo kupunguza vifo vyao.Elimu hii inaweza kutolewa kupitia Vituo Mbalimbali vya televisheni, radio,magazeti na machapisho mbalimbali.

UHAMASISHAJI
Wana jamii wanahitaji kuhasishwa juu ya kutoa misaada kwa watu Wasiojiweza nakuweza kuwasaidia hivyo kupunguza uhitaji wa makundi haya Maalumu. Mfano kupitia nyumba za ibada kama vile Makanisa na Misikiti Kuwahimiza waumini wao kuwasaidia, walemavu, na wasiojiweza kwani Ndio upendo wakweli, kupitia hivyo tutaweza kutatua changamoto,hizo mfano Kutembelea nyumba zinazolelea watoto yatim na walemavu na kuwapa misaada ya vyakula ,mavazi,na pesa za kujikimu pia.

UTAMBUZI WA FURSA ZILIZOPO
Jamiii pamoja na Serikali kwa ujumla kupita sekta hii ya ustawi wa jamii inaweza kuwasaidia na kuwawezesha watu katika makundi haya maalumu kutambua fursa mbalimbali zinazowazunguka na kuwasaidia kuwapa mitaji iliwaweze kujitafutia vipato vyao wenyewe. Mfano kufungua Biashara ndogondogo kama vile kuuza matunda,na bidhaa za manyumbani.

UDHIBITI WA FEDHA ZA TASAF
Kumekuweko na mtindo wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii kuwa zikitumiwa ndivyo sivyo na baadhi ya watumishi Wasio waadilifu hivyo kupelekea baadhi ya watu kukosa huduma stahiki. Udhibiti Huu unaweza kufanywa kupitia vyombo vyetu vya TAKUKURU, lakini pia kupitia levo ya chini kabisa kupitia wananchi wenyewe kuweza kutoa taarifa endapo fedha zinatolewa kwa watu wasio stahiki.

Pia kuanzishwa kwa mabaraza ya vijiji yatakayoweza kutambua zile kaya ambazo ndio zenye uhitaji stahiki kutoka na hali zao za kimaisha zilivyo. Lakini pia Kuwepo na Ongezeko la Bajeti ya wizara katika sekta ya Ustawi wa jamii kwaajili ya kuwafikia watu wengi iwezekanavyo .

USHIRIKI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Ujumuishwaji wa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kutoa misaada ya moja kwa Moja katika makundi maalumu kwa kutoa fedha zitakazo weza kuwawezesha walemavu, Na wasiojiweza kupata mahitaji yao ,lakini pia mashirika yanaweza kuendesha semina Mbalimbali zinaweza kutoa ufafanuzi yakinifu juu ya namna sahihi za kuweza kuwatunza Na kuwalea watu wasio jiweza pamoja na wazee hivyo kuwa epusha na majanga Mbalimbali yanayoweza kuwapata kama ,magonjwa na upweke nahivyo kuwaongezea Muda wa kuishi na kuongeza Maendeleo ya jamii kwa ujumla wake.

KUTUNGWA KWA SHERIA ZITAKAZOSIMAMIA HAKI ZA MAKUNDI MAALUM
Bunge linaweza Kuwa msaada mkubwa sana kwa kuweza kuanzisha sheria zitakazo weza kuwalinda Walemavu,wasio jiweza kwa kutunga sheria zitakazo kuwa na adhabu kali kwa wale wote Watakaofanya uonevu na unyanyasaji kwa makundi maalumu na hivyo kuwezesha Watu kuacha tabia hizo ambazo ni mbaya kwa jamii kiujumla.Mfano wale watu ambao Wana imani potofu juu ya walemavu na kuwa na matamanio ya kuwa pata baadhi Ya viungo vyao kwa malengo ya kujipatia utajiri ama kwa malengo yao binafsi.

KUDHIBITI NDOA ZA UTOTONI
Hii njia itapunguza idadi ya watoto watakaozaliwa ambao huendaWakawa katika hatari ya kuwa katika malezi ambayo hayatakuwa bora na kuwa pelekea Kuwa tegemezi, lakini pia ndoa za utotoni huwa hazidumu nahuwa zinavunjika kwa muda Mfupi mno hivyo kupelekea watoto walio patikana kuwa katika hatari ya kuwa watoto Wa mtaani nahivyo kuhitaji utegemezi kutoka kwa jamiii inayowazunguka.

Hivyo kwa Kuanzishwa kwa sheria zinazo toa katazo kwa watoto ambao ni waumri mdogo kuingia Katika ndoa za mapema,pia kuhamasisha watoto hao kwenda shule kuta punguza ndoa Hizo za mapema na kuondoa madhara yatokanayo na ndoa hizo

KUWEZESHWA KWA WAKINAMAMA
Njia hii pia inaweza kuwezesha uangalizi wa wazee katika Jamiii kwani wakinamama ndio watu wenye majukumu yakuwatunza wazee kwa kuwasaidia Katika majukumu yao yamuhimu kama vile kuwandalia nyakula kuwa fulia nguo na kuwa na uangalizi wa karibu. Mfano kuundwa kwa mifuko ya kinamama katika kata na vijiji kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya utunzaji wa watoto ,wazee na wasio jiwezaa hususani wale waliopo kwenye nyumba za watoto yatima na nyumba za kulelea wazee.

VIJANA KUPEWA ELIMU YA JINSIA
Njia hii itawasaidia vijana kujitambua pale wanapofika atika umri wa kubalehe nahivyo kutokujihusisha na ngono zembe hivyo kupunguza watoto Watokanao na ngono zembe. Mfano vipindi wanafunzi wawapo mshuleni kuwepo na semina Elekezi kwa vijana kuhusu kuwa makini na kujua halizao zakiweza kuzizuia hisia zao katika kipindi Cha hatari hasa pale wanapo kuwa wameanza kubalehe kutawasaidia kuepuka madhara Yatokanayo na hayo,kwa kujiweka bize kwa kufanya mazoezi na kujisomea kutawasaidia Kujiepesha na vishawishi kama hivyo nya kimapenzi.
 
Back
Top Bottom