Utatu wa Magufuli: Meya kada wa CCM, Mkurugenzi kada wa CCM na DC kada wa CCM halafu tunaulizana " Mchwa" wanatoka wapi kwenye Halmashauri zetu?!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,598
141,415
Eneo pekee ambalo sikumuelewa mpendwa wetu hayati Magufuli ni pale alipowateua Makada wa CCM kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri.

Sina shida kwenye ukuu wa wilaya kwani hata enzi za Tanu Madereva waaminifu wa chama walipokaribia kustaafu wakiteuliwa kuwa maDC ila kwa Wakurugenzi tulihitaji wataalamu siyo wanasiasa.

Labda kwa vile ukiteua Mkurugenzi ndio unakuwa umemteua Msimamizi wa Uchaguzi katika wilaya au Halmashauri

Huu utatu wa Meya + DED + DC = Makada wa CCM plus Madiwani wote ni Makada wa CCM basi Jumla kuu ni lazima iwe maumivu makali kwenye fedha za Halmashauri zetu

Mungu wa mbinguni utuhurumie sisi Waja wako!
 
Eneo pekee ambalo sikumuelewa mpendwa wetu hayati Magufuli ni pale alipowateua Makada wa CCM kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri...
Mtasema mazuri ya Magufuli, ni kweli yapo lakini mabaya yake yana madhara makubwa jana, Leo na zaidi siku zijazo.
 
Eneo pekee ambalo sikumuelewa mpendwa wetu hayati Magufuli ni pale alipowateua Makada wa CCM kuwa Wakurugenzi wa Halmashaur...
Mama kaanza kuteua taratibu wakurugenzi kutoka kwenye utumishi japo nao sio wa kuwaamini just refer sakata la mkuu wa Mkoa wa Mara na wale wakuu wa Idara plus wakuu wa Idara aliowahamisha vituo Bashungwa..

Dawa imepatikana kwamba wakitimuliwa wanarudi kwenye vyeo na salary za kimuundo so watakuwa na woga kiasi this time around.
 
Back
Top Bottom