Utatu wa maajabu ya anga leo usiku (usiku wa Ijumaa)

LOSEJMASAI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
332
856
Leo Usiku (Usiku wa Ijumaa) vitu vitatu vya Anga ya juu vitatokea kwa pamoja.

1. Usiku wa leo tutakuwa na Full Moon. Kama hakutakuwa na mawingu eneo ulilopo basi leo usiku mwezi utaoneka wote.

upload_2017-2-10_13-25-45.jpeg




2. Itakapo fika 7.44 p.m East Time (Ambayo sawa na saa Tisa Usiku na Dakika 44 kwa Dar es salaam) Kutakuwa na nusu-kupatwa kwa Mwezi (partial Lunar eclipse).
upload_2017-2-10_13-24-34.jpeg


NB: Kupatwa kwa Mwezi kunatoka pale tu kunapokuwa na Full moon.

3. Kimondo cha kijani na mkia wa purple pia kitaonekana kikipita karibu zaidi na dunia kuliko kawaida. kimondo hiki kinaitwa 45P/Honda-Mrkos-Pajdušáková. Hiki kimondo kinazunguka jua mara moja kila baada ya miaka mitano. Asubuhi ya kuamkia jumamosi kitakuwa umbali wa maili milioni 7 kutoka dunia (Mara 30 zaidi ya umbali kati ya dunia na mwezi). itakuwa bahati sana kukiona kutokana na kuanza kukucha pia na umbali. Lakini kwa wenye binoculars au telescope watakiona kwa urahisi zaidi

comet.jpg


Source: NASA
Three of the most beautiful things in the universe are about to happen. All at once
https://www.nytimes.com/2017/02/09/science/penumbral-lunar-eclipse-friday-comet-45p.html
This Triple Cosmic Experience Is Coming Friday Night

NB: Kwa atakaye shuhudia tujuzane.
 

Attachments

  • upload_2017-2-10_13-25-17.jpeg
    upload_2017-2-10_13-25-17.jpeg
    3.5 KB · Views: 91
Wambie hao NASA wazuie hili tukio kwanza maana tupo buzy na ya Mr.Makonda then tutarudi!
 
Hizi habari wewe umezipata wapi?
Je, ni za kweli?
Naomba unithibitishie ili niweze kukesha.
 
Mida ya saa mbili nilikua maeneo fulani nikaona mwezi leo una sura fulani hivi nikapiga picha sijui ndiyo maandalizi ya hiyo saa sita au vipi
IMG_20170210_194006.jpg
 
Back
Top Bottom