Utatu usio Mtakatifu!

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,249
8,456
Mbinguni Kuna utatu Mtakatifu unaofanya kazi yake kwa umoja na kupewa jina la MUNGU. Mungu Baba yupo katika kiti cha enzi, Mungu mwana anatuombea na alijidhihirisha kwa kufanyika mwili ili atuokoe, na Mungu Roho mtakatifu ambaye yupo nasi siku zote akituongoza kutenda yaliyo mema japo haonekani.

Vilevile hapa TZ kuna utatu unaofanya kazi zake kwa pamoja kila mmoja akiwa na Jukumu lake alilopewa. Huu umepewa Jina la MTANDAO. Kuna JK, EL na RA hawa kila mmoja analo jukumu lake kama ilivyo huko mbinguni kuleta ukombozi kwa nchi yetu. Lakini Huu utatu unaweza kweli kufanikisha hili.

JK yupo katika kiti cha enzi, yeye ndiye Baba wa Taifa, EL ndiye Mwana, anajidhihirisha kwetu kwa njia mbalimbali kila kukicha hakosa hata siku moja kujidhihirisha kwetu kwa njia ya redio, TV na magazeti. RA yeye haonekani ila yupo kati yetu kila siku, ni mshauri kwa njia ya vyombo vya habari especially magazeti na amekuwa akifanya kazi kubwa ya kutuongoza wananchi kuiona serikali inafanya kila lililojema katika kutuletea maisha bora kwa kila mTZ kwa kasi, nguvu na ari japo zimekuwa kuukuu sasa.

Je utatu huu utatufikisha unakotupelekea, nawauliza wana JF!!!!!
 
Utatu usio mtakatifu

Na Maggid Mjengwa,


NIMEPATA kuyaandika haya; kuna namna mbili kwa mtu kusafisha chumba chake; unaweza kufagia chumba, ukazoa takataka na kuzitupa. Lakini waweza pia kuzifagilia takataka chini ya jamvi.

Ukifanya hilo la mwisho bado atakayeingia chumbani kwako ataona chumba kimesafishwa. Huko ni kujidanganya kwa mwenye chumba. Akiendelea na tabia hiyo, iko siku uchafu ule utaanza kuvunda na kunuka. Asipoinua jamvi kuondoa uchafu unaovunda iko siku ataambiwa na wengine; kuwa chumba chako kinanuka.

Katika nchi yetu tumeanza kuziona dalili za siasa kuchanganyika na dini na biashara. Huu ni utatu usio mtakatifu. Hapa kuna tatizo. Kuna takataka tunazozifagilia chini ya jamvi, kisha tunaimba; nchi yetu ni ya amani na utulivu. Kwamba nchi yetu ni safi kabisa.

Kufanya hivyo si kuitendea haki nchi yetu tuliyozaliwa. Tatizo tunaliona. Ni wajibu wetu wa kizalendo kuzungumza kinagaubaga, kuwa hapa kuna tatizo. Maana Watanzania sisi tuna hulka ya ajabu kidogo. Wakati mwingine tunaamini kuwa kama jambo unalinyamazia, basi halipo hata kama lipo.

Tatizo unaliona, lakini unachofanya ni kunyamaza kimya tu. Kinachofanyika hapa ni kufagilia tatizo chini ya jamvi badala ya kufanya jitihada ya kuliondoa.

Kuna tatizo kubwa katika uongozi wetu wa kisiasa. Tumeruhusu siasa kungiliwa na dini na biashara kwa maana ya baadhi ya wafanyabiashara hata viongozi wa kidini wanaitumia siasa katika kufanikisha malengo yao. Kinachotokea sasa pia ni hata kwa baadhi ya wanasiasa kuitumia dini na wafanyabiashara kufanikisha malengo yao.

Kuna hali ya ” kuna mgongo wangu niukune wa kwako”. Mfanyabiashara anatoa ufadhili wake katika siasa ili baadae siasa imsaidie katika biashara yake. Kiongozi wa taasisi ya kidini anaipigia debe siasa kwenye nyumba ya ibada ili siasa nayo imsaidie katika kujijenga. Hapa tuna viongozi wa taasisi za kidini waliojiingiza katika biashara na siasa. Bado tuna misamaha ya kodi kwa vinavyoingizwa nchini na taasisi za kidini. Wakati mwingine misamaha hii kimsingi ni kwa taasisi za kidini zinazofanya biashara. Naam. Hata kwenye baadhi ya taasisi za kidini kuna uozo na ufisadi uliokubuhu.

Hakuna dhambi kwa kiongozi wa kidini au mfanyabiashara kujihusisha na siasa, lakini, katika ubia huu wa siasa, dini na biashara hakuna utaratibu uliowekwa ili ufuatwe kwa minajili ya kuepuka mikanganyiko itakayopelekea kuwakanganya na kuwaathiri Watanzania wanyonge walio wengi. Kuna umuhimu wa jambo hili kuwekwa katika Katiba ya Nchi.

Ni vema na busara kabisa tukawa na taratibu na nidhamu ya kuzifuata taratibu. Na nidhamu ya kufuata taratibu inatokana na sheria na adhabu zinazoendana na kukiukwa kwa taratibu hizo.

Na hapa mpira uko ndani ya Chama tawala, CCM. Chama Cha Mapinduzi ni chama tawala, hivyo kina wajibu wa kwanza wa kuandaa taratibu zitakazofuatwa ndani ya chama hicho inapohusiana na uongozi wa kisiasa. CCM hakipaswi kuwa ni chama kinachopambana ili kiishi. Tayari kiko madarakani, hiki si chama cha upinzani.

Ndani ya CCM imeanza kuboboka misingi iliyopelekea kuanzishwa kwa Chama hicho tukianzia na vyama mama vya TANU na Afro- Shiraz. Hili ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, Vyama mama kwa CCM, TANU na Afro- Shiraz, vilikuwa ni kimbilio la makabwela, kimbilio la wanyonge.

Lakini, CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao, wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi. Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; ”Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM”. Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!
CCM ya sasa inakimbiliwa hata na baadhi ya viongozi wa taasisi za kidini. CCM ya sasa ni taasisi kubwa. Ndani yake ina watu wa kila namna. Kuna makundi. Kuna majungu na fitna. Kuna kupakaziana, kuchafuana na kusafishana.

Naam. Kuna wanaokimbilia ndani ya CCM kwa kuamini katika malengo na madhubuni ya kuanzishwa kwa chama hicho. Lakini kuna wanaokimbilia ndani ya CCM wakiwa na malengo na madhumuni ya kwao binafsi yasiohusiana kabisa na ya CCM. Kwao wao, CCM ni sawa na daraja la miti la kuwasaidia kuvuka na kufika wanakotaka kwenda.

Baadhi wako tayari kutumia mamilioni ya shilingi kukimbilia uongozi ndani ya chama hicho. Wanakimbilia ndani ya chama kujificha, kuficha maovu yao, kulinda na kutetea maslahi yao binafsi na ya makundi yao.

CCM ina nafasi ya kujisahihisha na kuuvunja utatu huu usio mtakatifu. Si udhaifu kwa kiongozi au wanachama wa chama cha siasa kukiri udhaifu na kujisahihisha. Mwl. Nyerere katika kijitabu chake cha ” Tujisahihishe” anaandika; ”Nataka kutaja makosa machache ambayo mara nyingi huzuia Umoja wowote kuwa imara hata ushindwe kutimiza madhumuni yake.

Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko, nzige, kiangazi, nk, matatizo yao mengi hutokana na ubinafsi”
”Swali ambalo twalisikia mara kwa mara; ” Hali yetu ya baadaye itakuwaje? Mtu anayeuliza anafikiri kuwa TANU iliundwa kwa faida yake yeye binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi, TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tuzo! Anasahau kabisa, kuwa TANU inajishughulisha na haja za jumuiya kwa ujumla.

Lakini, kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake ya Jumuia, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake! Huu ni ubinafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakiuhukumu chama chetu kwa mahitaji ya jamii yao, bali watakihukumu kwa mahitaji ya nafsi zao wenyewe, chama hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama”

Mwl. Nyerere anaendelea; ” Dalili nyingine ya ubinafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana, ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema; ”Nitasema kweli daima. Fitina kwangu ni mwiko.” Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua.” (J.K Nyerere ”Tujisahihishe”,1962).

Hakika, uongozi wa Chama Cha Mapinduzi ungefikiria kukichapa tena kitabu hiki cha Mwalimu na kukigawa kwa viongozi na wanachama wake. Ni kitabu kinachopaswa kusomwa pia na kila mzalendo wa nchi hii. Maana, aliyoyaandika Mwalimu Nyerere mwaka 1962 ndio yaanayotokea sasa .


0788 111 765
CHANZO: kwanzajamii.com
 
JER ni utatu ambao uliachiwa kujijenga ndani ya chama tawala yaani CCM....kwa maneno yake J akihojiwa na BBC ya Tido wakati fulani alisema pasi na kuuma maneno kuwa walianza mchakato wa kuunda mtandao uliozaa matunda mwaka 2005 tangu mwaka 1995 pale kura ziliposhindwa kutosha na bwana uwazi kushinda na hatimaye kukalia kiti cha enzi.

J na E walikuwa pamoja UDSM na inawezekana uswahiba wao ulianzia huko...ni marafiki wa siku nyingi na pengine wana sababu nyingi za kuwa marafiki...alipo J na E yupo na kinyume chake..haya yamethibitishwa na wenyewe katika nyakati tofauti na kwa karibuni ni pale E akihojiwa na Tido akiwa TBC alisema...."mimi na mheshimwa...hatukukutana barabarani...."

Akiongea na wanahabari kukanusha kuhusu habari ya kuwa alishaunda baraza la mawaziri wakati fulani mwaka 2005, J alithibitisha kuwa kweli yeye, E na R ni marafiki lakini habari hiyo ya baraza ilikuwa uzushi.

Kuna makosa huwa vizazi vinayafanya na matokeo yake ikawa ni mwanzo wa mwisho wa kizazi hicho na wanaowazunguka...kama kuna kosa kizazi cha sasa katika CCM kilifanya basi ni kuwaacha JER wajijenge kwa kiasi hicho..sasa JER ni kama mti wenye ukubwa wa mbuyu na uimara wa mpingo...nionavyo hakuna atakaeweza kuung'oa tena mti huo ndani ya CCM..kila atakayejaribu atakwenda na maji...mh 6 yeye alionjeshwa tu nini athari ya kucheza na mti huo...bahati mbaya ni kuwa wazee katika chama walijua kitambo kuwa E hakuwa safi kadhalika R. Wazee waliamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite na kutaraji kuwa kwa kuwa waliokuwa vijana wakati ule 1995 sasa wamekua, wasingeweza kufanya wanayofanya sasa..walikosea...hulka haipotei kabisa na mjasiri haachi asili...au kwa kizungu...what goes around comes around..

Lengo la JER lilikuwa ni kukalia kiti cha enzi na kumiliki kila eneo lihusikalo na kufanya maamuzi.....wamefanikiwa...EPA, buzwagi, richmond, dowans, vitambulisho vya taifa, kilimo kwanza na power tillers zake ni mfano wa machache tunayoyafahamu...

Nani amekohoa na JER ikapata mafua kutoka katika mfumo...hakuna.

Kitu JER hawakuwahi kukifikiria katika mipango yao ni nguvu ya umma...walidhani uzuri wa sura...weupe wa nywele(zamani ilikuwa dalili ya hekima lakini siku hizi hapana) na rangi ya ngozi vingewazubaisha wadanganyika kwa muda wote...walikosea sana...

Jana walipitisha katika CC yao kwenye jumba letu jeupe uamuzi wa kuwalipa Dowans 94bn kutoka katika mifuko yetu wadanganyika...wamekosea tena....tutawahukumu...tumewaonyesha nini tunaweza kuwafanya katika uchaguzi uliopita...waendelee na mipango yao lakini tutawaweka kwenye miti na kuwasulubu wakati ukifika na si mbali kama wanavyojidanganya..wajifunze kwa Nicolae Ceausescu....ikiwa historia ina maana yoyote kwao...

Amma kwa wanaowazunguka...hawako salama...mwanzo wa mwisho wa kizazi chao ni huu...na makosa wamefanya wazee wao...salama kwao ni kuwaacha wazee wao na wao kwenda njia zao..inawezekana, kama makongoro alivyofanya na baba yake akiwa hai..wakiendelea kujiongopea kwamba wanaweza kurekebisha hali wakiwa ndani wanakosea...hawana nafasi hiyo...Chiligati kawamaliza...wakizubaa shauri zao...wakati ukifika, itakula kwao...wajifunze kwa wahafidhina wa chama cha Ben Ali huko Tunisia...

Nawasilisha..
 
Pamoja na mbinu zao chafu, nguvu ya umma imeanza kuwaangusha. Ipo siku tena i karibu watakapofikishwa mahakamani kujibu uchafu waliofanya na kuwatesa wananchi.
 
kwa maana ya historia kwao, nadhani ina nguvu mara 100 zaidi ya hata hao wakina Ben Ali na Cesescu!! Hawa watu tumewaingiza madarakani sisi wenyewe (japo wanajiaminisha kuwa ni nguvu ya pesa zao), M7 aliwahi kusema kuwa yeye aliingia madarakani kwa nguvu na taabu ambapo kila mtu aliyekuwepo alishuhudia lakini hawa ni waoga na taasisi wanazotumia kuwakinga sifikirii kama muda mfupi ujao zitakuwa na uwezo hata wa kuwapa taarifa za kinachoendelea. Asante kwa hoja yako
 
Back
Top Bottom