Utatu usio mtakatifu: Siasa, dini na biashara

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
409
30
KUNA namna mbili kwa mtu kusafisha chumba chake; unaweza kufagia chumba, ukazoa takataka na kuzitupa. Lakini waweza pia kuzifagilia takataka chini ya jamvi.

Ukifanya hilo la mwisho bado atakayeingia chumbani kwako ataona chumba kimesafishwa. Huko ni kujidanganya kwa mwenye chumba. Akiendelea na tabia hiyo, iko siku uchafu ule utaanza kuvunda na kunuka. Asipoinua jamvi kuondoa uchafu unaovunda iko siku ataambiwa na wengine; kuwa chumba chako kinanuka.

Katika nchi yetu tumeanza kuona dalili za siasa kuchanganyika na dini na biashara. Huu ni utatu usio mtakatifu. Hapa kuna tatizo. Kuna takataka tunazozifagilia chini ya jamvi, kisha tunaimba; nchi yetu ni ya amani na utulivu. Kwamba nchi yetu ni safi kabisa.

Kufanya hivyo si kuitendea haki nchi yetu tuliyozaliwa. Tatizo tunaliona. Ni wajibu wetu wa kizalendo kuzungumza kinagaubaga, kuwa hapa kuna tatizo. Maana Watanzania sisi tuna hulka ya ajabu kidogo. Wakati mwingine tunaamini kuwa kama jambo unalinyamazia, basi halipo hata kama lipo. Tatizo unaliona, lakini unachofanya ni kunyamaza kimya tu. Kinachofanyika hapa ni kufagilia tatizo chini ya jamvi badala ya kufanya jitihada ya kuliondoa.

Kwa mtazamo wangu, kuna tatizo kubwa katika uongozi wetu wa kisiasa. Tumeruhusu siasa kuingiliwa na dini na biashara kwa maana ya baadhi ya wafanyabiashara hata viongozi wa kidini wanaitumia siasa katika kufanikisha malengo yao. Kinachotokea sasa pia ni hata kwa baadhi ya wanasiasa kuitumia dini na wafanyabiashara kufanikisha malengo yao.

Kuna hali ya " kuna mgongo wangu niukune wa kwako". Mfanyabiashara anatoa ufadhili wake katika siasa ili baadaye siasa imsaidie katika biashara yake. Kiongozi wa taasisi ya kidini anaipigia debe siasa kwenye nyumba ya ibada ili siasa nayo imsaidie katika kujijenga. Hapa tuna viongozi wa taasisi za kidini waliojiingiza katika biashara na siasa. Bado tuna misamaha ya kodi kwa vinavyoingizwa nchini na taasisi za kidini. Wakati mwingine misamaha hii kimsingi ni kwa taasisi za kidini zinazofanya biashara. Naam. Hata kwenye baadhi ya taasisi za kidini kuna uozo na ufisadi uliokubuhu.

Hakuna dhambi kwa kiongozi wa kidini au mfanyabiashara kujihusisha na siasa, lakini, katika ubia huu wa siasa, dini na biashara hakuna utaratibu uliowekwa ili ufuatwe kwa minajili ya kuepuka mikanganyiko itakayowakanganya na kuwaathiri Watanzania wanyonge walio wengi. Ndiyo maana, katika makala iliyopita, nilizungumzia umuhimu wa jambo hili kuwekwa katika Katiba.

Ni vema na busara kabisa tukawa na taratibu na nidhamu ya kuzifuata taratibu. Na nidhamu ya kufuata taratibu inatokana na sheria na adhabu zinazoendana na kukiukwa kwa taratibu hizo.

Na hapa mpira uko ndani ya chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM). CCM ni chama tawala, hivyo kina wajibu wa kwanza wa kuandaa taratibu zitakazofuatwa ndani ya chama hicho inapohusiana na uongozi wa kisiasa. CCM hakipaswi kuwa ni chama kinachopambana ili kiishi. Tayari kiko madarakani, hiki si chama cha upinzani.

Ndani ya CCM imeanza kubomoka misingi iliyokianzisha, kuanzia vyama mama vya TANU na Afro- Shiraz. Hili ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, vyama mama kwa CCM, TANU na Afro- Shiraz, vilikuwa ni kimbilio la makabwela, kimbilio la wanyonge.

Lakini, CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao, wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan CCM. Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!

CCM ya sasa inakimbiliwa hata na baadhi ya viongozi wa taasisi za kidini. CCM ya sasa ni taasisi kubwa. Ndani yake ina watu wa kila namna. Kuna makundi. Kuna majungu na fitna. Kuna kupakaziana, kuchafuana na kusafishana.

Naam. Kuna wanaokimbilia ndani ya CCM kwa kuamini katika malengo na madhubuni ya kuanzishwa kwa chama hicho. Lakini kuna wanaokimbilia ndani ya CCM wakiwa na malengo na madhumuni ya kwao binafsi yasiohusiana kabisa na ya CCM. Kwao wao, CCM ni sawa na daraja la miti la kuwasaidia kuvuka na kufika wanakotaka kwenda.

Baadhi wako tayari kutumia mamilioni ya shilingi kukimbilia uongozi ndani ya chama hicho. Wanakimbilia ndani ya chama kujificha, kuficha maovu yao, kulinda na kutetea maslahi yao binafsi na ya makundi yao.

CCM ina nafasi ya kujisahihisha na kuuvunja utatu huu usio mtakatifu. Si udhaifu kwa kiongozi au wanachama wa chama cha siasa kukiri udhaifu na kujisahihisha. Mwalimu Julius Nyerere katika kijitabu chake cha " Tujisahihishe" anaandika; "Nataka kutaja makosa machache ambayo mara nyingi huzuia Umoja wowote kuwa imara hata ushindwe kutimiza madhumuni yake. Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko, nzige, kiangazi, nk, matatizo yao mengi hutokana na ubinafsi"

"Swali ambalo twalisikia mara kwa mara; " Hali yetu ya baadaye itakuwaje? Mtu anayeuliza anafikiri kuwa TANU iliundwa kwa faida yake yeye binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi, TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tuzo! Anasahau kabisa, kuwa TANU inajishughulisha na haja za jumuiya kwa ujumla.

Lakini, kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake ya Jumuia, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake! Huu ni ubinafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakiuhukumu chama chetu kwa mahitaji ya jamii yao, bali watakihukumu kwa mahitaji ya nafsi zao wenyewe, chama hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama"

Mwl. Nyerere anaendelea; " Dalili nyingine ya ubinafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana, ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema; "Nitasema kweli daima. Fitina kwangu ni mwiko." Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua." (J.K Nyerere "Tujisahihishe",1962).

Hakika, uongozi wa CCM ungefikiria kukichapa tena kitabu hiki cha Mwalimu na kukigawa kwa viongozi na wanachama wake. Ni kitabu ambacho kinapaswa kusomwa pia na kila mzalendo wa nchi hii. Maana, aliyoyaandika Mwalimu Nyerere mwaka 1962 ndio yaanayotokea sasa ndani ya CCM. Hakika Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuona mbali.
 
Augustoons,
Nilishawahi kufikiri sana kuhusu mfumo wa mabadiliko mbalimbali ya nchi yetu ikiwemo ndani ya CCM. Mfumo uliojengeka ndani ya CCM ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu, tatizo siyo sera za chama, nadiriki kusema kama ni sera basi sera za CCM ndiyo zinazoeleweka zaidi kuliko za Chama kingine chochote, lakini tatizo hutumika tu kama rubber stamp wakati wa uchaguzi, kinachotekelezwa siyo kilichomo kwenye sera zao. Tatizo la CCM ni aina ya watu waliokishikilia chama hicho na mfumo wa uzandikiki na na wa kibabe wa uendeshaji wa chama hicho. Wanaoijua vizuri CCM watakubaliana nami kuwa CCM katika salaam zao huitikia "Chama kina wenyewe, na wenyewe ndiyo wao" lakini ukweli ni kuwa CCM ni chama cha mabepari wachache, wanaofahamiana, wanaojua wanachokitafuta, wanaowatumia watanzania wengi kwa kuwalaghai na kujiona kuwa nao pia ni wana CCM kuendeleza matakwa yao hao wachache, ndio maana hutakuja kusikia kuwa kiongozi wa ngazi za juu wa CCM amefukuzwa uanachama. Kundi hilo la watu wachache lina nguvu na ushawishi mkubwa wa kuteka fikra na mawazo ya watu wa rika zote hadi maprofesa. Kuna wazalendo wachache ambao huingizwa kwenye ngazi za juu za serikali "siyo chama" ili kufukia fikra kuwa chama ni cha wachache, watu hawa huchukua nafasi zao kwa unyenyekevu wakidhani wanawatumikia watanzania, lakini ukweli wanakuwa wanawatumikia wachache waliokishikilia chama. Dr. Kwame Nkrumah aliandika "Power Breeds Power", mfumo huo wa watu wachache umekuwa wakurithishana, na ulianza na kujengeka sana miaka ya 1990 na sasa unakomaa, watoto wa kundi hilo wanakuzwa katika mfumo huo. Kundi hilo limevaa mavazi ya mwasisi wa taifa hili Mwl. Nyerere, lakini wafuasi wa kweli wa Mwl wote hawamo kwenye hili kundi, na tumewasikia mara nyingi wakivikana vitendo vya watu hawa. Ndiyo maana hata walivyojaribu kuzuga kwa kufanyia mkutano Butiama waliondoka na aibu, kwani hakukuwa na lolote la maana zaidi ya kuchanganyikiwa na kuja kuitisha mkutano mwingine Diamond Jubilee kufafanua maamuzi ya Butiama, kama kawaida watanzania wakashawishika kwa kujifanya wameelewa lakini kimeo cha mpasuko Z'bar bado kipo palepale na 2010 tutegemee mengine tena.
Nimalizie kwa kusema, kundi hilo litaondolewa na wana CCM wenyewe, na likiondoka kundi hili, nchi hii itaanza kusonga mbele.
 
Unaposikia kuwa chama kina wenyewe basi hao wenyewe hao ndio wale wachache wanaopindisha mambo yote yaliyomo kwenye ilani na manifesto mbalimbali za mwalimu matokeo yake ni kuzalisha ufisadi.
 
Unaposikia kuwa chama kina wenyewe basi hao wenyewe hao ndio wale wachache wanaopindisha mambo yote yaliyomo kwenye ilani na manifesto mbalimbali za mwalimu matokeo yake ni kuzalisha ufisadi.

Chama tawala cha CCM kimefikia hatua ya kutoweza kujisafisha kwa namna yoyote ile na kujaribu kufanya hivyo ni kujichafua tu zaidi. Hilo halina tofauti na mfagizi wa chumba kama ilivyonenwa hapo awali na njia moja tu iliyobaki kwa mwenye nia ya kwelikweli na inayotaka moyo, ni kujiondoa humo.

Walioiteka CCM wanakuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii masikini kutokana na uwezo wao mkubwa kifedha, period. Historia inatukumbusha vizuri kabisa kuwa tabaka hili la viongozi kama tunavyoshuhudia, haliondoki hivi hivi kirahisi na hutumia kila aina ya ulaghai kubaki madarakani.

Hata hivyo kila kitu kina mwisho wake na mabadiliko lazima yatokee na hofu kubwa ni namna yatakavyokuja. Ama wananchi wakati wakidai haki yao watapewa au wataichukua wenyewe kwa njia yoyote ile. Mimi nimeanza kuhesabu muda na nadiriki kusema huo muda hauko mbali, unakaribia.
 
Moja ya tishio kubwa la kundi hili hatari la CCM ni hoja ya Mgombea Binafsi, ndani ya CCM yenyewe, kuna watu makini ambao hawafurahii kabisa hali ilivyo, lakini kwa kutokuona mbali na kwa maslahi ya muda mfupi wako radhi waendelee kutaabika. Itakapopitishwa hoja ya mgombea binafsi, ndipo itakuja julikana wafia dini ni wepi na waliokuwa wana buy time tu wote wataondoka na ndio kiama cha kundi hili baya la akina Makamba & Co. Kwa sasa si rahisi kabisa kwa kundi hili kukubali hoja hii, hii inatoa tu picha kuwa si rahisi kundi hili kukubali kushindwa. Hakuna mji udumuo chini ya jua. Kengele imelia, watanzania wale wanaishia na kizazi kipya kinaibuka, saa ipo, haki itakapokuja kutawala juu ya nchi hii.
 
Kinto,
Mkuu nadhani inabidi uzisome upya sera za CCM kabla hujazipandisha chat kiasi hicho...
CCM wanavyodai ni kwamba nchi yetu ni ya UJAMAA na KUJITEGEMEA.. sasa naomba unambie uzuri wa sera iliyotangazwa na chama kisha nambie kile kinachofanyika (kufagia uchafu chini ya Uvungu) au kingefanyika nini ikiwa nchi yetu leo hii tunategemea Wawekeshaji toka nje..(kufagia na kuutoa nje uchafu)..
Labda umeshindwa kuelewa maana halkisi ya usemi huu "Chama kina wenyewe, na wenyewe ndiyo wao" lakini ukweli ni kuwa CCM ni chama cha mabepari wachache...
Jibu umelisema mwenyewe mkuu....
Twende hatua kwa hatua..
 
Mkubwa Mkandara, nimekupata vizuri, lakini ninachosisitiza ni kwamba, maandiko ya CCM (mwelekeo wa sera za CCM, itikadi yake, na ilani ya 2005) ukisoma yanatoa matumaini makubwa kwa maendeleo ya watanzania, lakini kinachofanyika ni tofauti na kilichomo ndani ya sera zao. Na kwa ufupi hakuna jipya, mambo ya miaka ya 60 na 70 ndo yamo kwenye sera zao za leo, kwa maana hiyo watu walewale wanazunguka mlemle wakiendeleza yaleyale yaliyotufikisha hapa, ambayo miaka zaidi ya 45 hawajaweza kutekeleza. Kwa hiyo, ama ni sera za ulaghai ambazo hazitekelezeki zinazotumika kutudanganya ili waendelee kutawala au ni ufisadi wa lile kundi la watu wachache wanaokwamisha utekelezaji wake. Bado ninashawishika kwamba, kama kuna kuwa na nia ya dhati na means za kutekeleza sera hizi, mabadiliko yataonekana. Narudia, tatizo la CCM si sera zake, bali ni utekelezaji wake
 
Wataalamu wa sikolojia ya binadamu wanasema ni vigumu sana kwa ubongo uliotunga kitu wenyewe kukibadili kile kitu, kwa vile kunakuwa na "conflict" pia "pride" na "continuity" inayomfanya aliyemo atake kubaki humo.
Hivyo ili kuwezesha chama kubadilika ni kwa wanachama wapya kuingia wakiwa na mawazo mapya imara na tayari kuyatekeleza na kuyatetea.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom