Utata watanda nchi anakotibiwaDr Ulimboka TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata watanda nchi anakotibiwaDr Ulimboka TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Jul 5, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.

  Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

  “Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
  Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”

  Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.

  Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

  “Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”

  source Mwananchi
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Unataka kujua aliko ili iweje?!
   
 3. Ticha

  Ticha Senior Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  habari za magazeti ndo unaona za uhakika,mwandishi wa BBC toka s.afrika Leo karipoti kuwa kaenda kumuona ila ndugu zake wakakataa kumuhoji lakini kamuona.anaendelea na matibabu.

  Mnasoma magazeti ya umbea tu.
   
 4. s

  saita Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la muhimu ni dr. Ulimboka kupata matibabu ya maana na kuridi tena nchini na kueleza kilichotokea ili unafiki ujitenge na ukweli wa viongozi wetu. Hakuna tija kufahamu aliko hata kidogo.
   
 5. s

  saita Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utata huo unasababishwa na umuhimu wa kumlinda dr. Ulimboka hasa baada ya kujua kuna wautu wenye nia mbaya ya kutaka kummalizia kabisa.
   
Loading...