cocochanel
Platinum Member
- Oct 6, 2007
- 26,768
- 73,435
buswelu moja mdada ameshamaliza kujaribu kuficha madudu yake hapo Arusha au? Ni kidogo hajieoeei.. akivhunguzwa au lawama zikimjia asijiulize kwa kuonyesha kuna majambo.
Huyo hence angejaribu kusoma alama za nyakati
Anaweza kujikuta amepelekwa Nanyumbu kua mrajisi wa wilaya wa vyama vya ushirika
kuna wafanyakazi wamefanya sherehe huyu dada kuhamishwa
Mbona uzi wa kuhusu huyo dada ulitoka tangia juzi.
Inademekana huyo dada ni chakula cha Bashite.
Bashite kamwqmbia atulie kwanza kwa sababu bashite alimiahidi kumleta DSM
Sasa umeandika nini wewe mlimbwende?buswelu moja mdada ameshamaliza kujaribu kuficha madudu yake hapo Arusha au? Ni kidogo hajieoeei.. akivhunguzwa au lawama zikimjia asijiulize kwa kuonyesha kuna majambo.
Sasa umeandika nini wewe mlimbwende?
Lionee!
Jikite kwenye mada wewe weeUmenimichi kuninukuu.. karibu.
Bado hujaambulia mzee tajiri naona.. eeeeeh
Soma takwimu za makusanyo ya kodi kiwilaya utaipata Kahama...Arusha watu wana hela zaid ya Kahama Mkuu,, na kuna mzunguko wa hela tofauti na kahama ,
Kahama ipo vizuri Mkuu lakini tukubali haifiki kwa Arusha jiji .
Jikite kwenye mada wewe wee
Hahahaaaaa sio songea tu pale mjini mbona angefurahi ila.ingesoma lituhi huko manda ndio ange isoma.gps vizuriYani kwa uzi huu natumai uyo Dada sasa hivi anaenda petrol station kujaza mafuta anaondoka arushakesho saa moja na nusu mkienda TRA kahama mtamkuta
Anabahati arusha kahama siyo mbali angetupwa songea uko alafu huu Uzi ukaja mda huu mungu wangu leo angeshinda anajihalishia tu
Kiukweli tunamchoma hivihivi lakini MUNGU atamwokoa na uchochezi huu wa vidole vyetu! kapige kazi dogo kahama kuko vizuri tu! usiogope usijidanganye kuacha kazi kwa kutegemea labda vimiradi vya kuku inaweza kula kwako nenda kwanza kaa hata baada ya miezi sita ndo utafute alternative kwa amani na usalama zaidi.Why mnamuandama huyu dada???
Akihama au asipohama wewe mshahara utaongezeka? Kuna watu mmekaa kiumbea kufatilia maisha ya watu wengine tuMwandishi wetu,Arusha
Sakata la aliyekuwa meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato nchini(TRA) mkoani Arusha kitengo cha madeni ,Irene Hance kukataa uhamisho wa kwenda wilayani Kahama limechukua sura mpya mara baada ya mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi,Richard Kayombo kutamka ya kwamba taasisi hiyo inafuatilia suala hilo.
Kayombo,ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache mara baada ya mamlaka hiyo kuwabadilisha vigogo 34 wa mamlaka hiyo kwenye vituo vyao vya kazi nchi nzima muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kumtumbua aliyekuwa kamishna mkuu wa mamlaka hiyo,Charles Kicheere.
View attachment 1143971View attachment 1143972View attachment 1143973View attachment 1143973View attachment 1143974View attachment 1143974
Takribani uhamisho huo ulipotoka wiki mbili zilizopoita Hance amekuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida katika kituo chake cha Arusha huku wenzake wakiwa wamesharipoti katika vituo vyao vipya jambo ambalo limeibua utata ndani ya taasisi hiyo nyeti nchini.
Akihojiwa na waandishi wa habari hivi karibuni Kayombo alitamka kwamba suala la uhamisho wa watumishi wa TRA ni suala la ndani ya taasisi hiyo na sio mahali pengine.
“Suala hilo ni suala la kiutawala na wala sio mahali popote ,suala la uhamisho ni suala la ndani kama kuna ukiukwaji wowote tofauti na kinachotakiwa kufanyika basi tutaifahamisha jamii”alisema Kayombo
Hatahivyo,alisisitiza kwamba yeye binafsi anashindwa kuelewa ni kwanini suala la uhamisho wa watumishi wa TRA hususani mkoani Arusha limekuwa jambo zito kuliko mikoa mbalimbali nchini.
Wiki iliyopita meneja wa TRA mkoani Arusha,Faustine Mdesa alikaririwa na vyombo vya habari akitamka ya kwamba Hance sio mtumishi wake na tayari alishampatia barua ya uhamisho kwenda Kahama.
“Ninachotambua huyo sio mtumishi wangu kwani nilishampatia barua ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi ambacho ni Kahama siwezi kumzungumzia mtu ambaye sio mtumishi wangu”alikaririwa Mdesa
Suala la uhamisho wa Hance limeibua mkanganyiko ambapo mara kwa mara amekaririwa na vyombo vya habari akitamka ya kwamba tayari amesharipoti kwenye kituo chake kipya cha kazi wilayani Kahama tangu Juni 26 mwaka huu na anaendelea na majukumu yake ya kazi huku akionekana katika kituo chake cha zamani akiendelea na majukumu.
“Mwandishi nimesharipoti tangu Juni 26 mwaka huu kwenye kituo change kipya cha kazi na ninaendelea na majukumu yangu ya kazi Kahama”alikaririwa Hance
Kuhusu suala la kutamba mbele ya wafanyakazi wake kuwa hawezi kwenda Kahama kwa kuwa ana mahusiano mazuri na baadhi ya vigogo wa taasisi hiyo makao makuu Hance alisema kwamba hayo ni masuala ya kiofisi na kwamba hawezi kujibu chochote.
Hatahivyo,taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi zinadai kwamba leo Julai Mosi mwaka huu Hance hajaonekana ofisini na taarifa zinadai kwamba amefunga safari kuelekea makao makuu ya TRA kwa lengo la kutengeneza mazingira ya yeye kuendelea kubaki katika kituo chake cha kazi mkoani Arusha.
Mwisho.
Kweli kabisa yaani niUchonganishi tuu..yeye ni mtumish kunataratibu za kiutumishi istoshe anazikamilishaHabari ndefu haina hata hoja za msingi
Acheni kumtisha....wengi humu hatujui exactly nini kimetokea...hata hivyo ana uhuru wa kuamua kwani hiyo kazi ni lazima?.......hata akiamua kuacha aache tuKama kweli anagoma naona mkuu anamchora tu. ..asome alama za nyakati. anaweza fanyiwa surprise...