Utata waibuka TRA Arusha, Meneja aliyehamishwa agoma kuondoka

Fake news, umbea mtupu, tafuta kitu cha maana watu wafaidike sio huu umama wako! Mfyuuuu. Bs
 
hili ndilo tatizo kubwa ndani ya TRA kuna watu wamejenga himaya,namsii DG achukue hatua haraka huu ni mtego kwani Presidaa anaelewa kila kitu kinachoendelea ndani ya TRA ushauri wangu fukuza kabla ya wewe ujatumbuliwa asikushike sharubu,siku ya siku kila mtu anabeba msalaba wake
 
Mwandishi wetu,Arusha

Wakati Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) ikifanya mabadiliko ya kiutendaji kwa watumishi wake mbalimbali nchini utata umeibuka mkoani Arusha ambapo aliyekuwa meneja msaidizi wa TRA mkoani Arusha kitengo cha madeni,Irene Hance anadaiwa kugoma kuhamia katika kituo chake kipya cha kazi.

Hatahivyo,meneja wa TRA mkoani Arusha,Faustine Mdesa amezungumza na waadishi wa habari na kusema kwamba msaidizi wake ameshapewa barua ya kuhamia kwenda katika kituo chake kipya cha kazi na endapo amegoma kwenda hilo sio suala lake.

“ huyo sio mfanyakazi wangu ameshachukua barua yake ya kwenda Kahama sasa suala la yeye kutokwenda hilo mimi halinihusu lakini ukweli ni kwamba huyo sio mtumishi wangu kwa sasa”alisema Mdesa

Katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni Hance amepelekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuwa meneja msaidizi kitengo cha ukaguzi huku aliyekuwa ofisa wa kodi mkoani Arusha,Nuhu Seleman amehamishiwa mkoani Mbeya kuwa meneja msaidizi kitengo cha madeni.

Taarifa za Hance kugoma kuhamia kwenye kituo chake cha kazi zimeibua hisia kali hususani kwa baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kwamba huenda analindwa na baadhi ya vigogo kutoka ngazi za juu serikalini.

Hatahivyo,mwandishi alifika katika ofisi za TRA Arusha ghorofa ya kwanza ili kuthibitsha taarifa hizo na kukutana na katibu mukhtasi wake ambaye jina lake halijatambulika ambapo alidai kuwa ametoka majira ya mchana na yuko nje katika majukumu yake ya kazi.

“ Alikuwepo hapa asubuhi lakini kwa sasa ametoka yuko nje kwenye majukumu yake ya kazi labda uniachie namba zako ili akirudi nimpatie akupigie”alisema katibu mukhtasi huyo

Juhudi za kumpata Hance ili kuthibitisha madai hayo zimeshindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi hakuweza kujibu.

Mwisho.
sisi wa kahama tunamsubiri
 
Back
Top Bottom