Utata wagubika soka ya Hispania. Real Madrid na Barcelona watishia kugoma mechi zao kuoneshwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Soka la Hispania lipo chini ya Shirikisho lao la soka RFEF, ambao wao wana LA LIGA kama chombo huru kinachosimamia Ligi kuu na Daraja la kwanza

Sasa kutokana na uhuru huo LA LIGA chini ya Javier Tebas wana mambo mengi wanafanya kinyume na mitazamo ya wengi, huku wakisema ni kibiashara zaidi

Uliwahi kutokea mgogoro wa kwanza kati ya Shirikisho na LA LIGA kuhusu kuweka mechi siku za juma, kama Jumatatu na Ijumaa, wakafikishana mpaka Baraza la michezo la Hispania

Sasa mgogoro wa sasa ni mkataba wa LA LIGA ana CVC Media Partners, ambapo La Liga wanataka kuwauzia 10% ya hisa ili wasimamie haki za kurusha ligi yao, huku wakitoa pesa nyingi

Bahati mbaya sana Rais Perez wa Real Madrid alikuwa wa kwanza kushtukia mpango huo kuwa hauna faida kwa klabu! Kwakuwa wakiuza haki zao wataingiza hasara ya Euro 800 Million kwa miaka 50 ijayo

LA LIGA wao wanasema ni mpango wa kusaidia klabu kujikwamua kiuchumi ila klabu kama Real Madrid na Barcelona wamegoma, wanasema ni mpango wa muda mfupi kiuchumi ila hasara ya muda mrefu

Kwa pamoja Real Madrid na Barcelona wamegoma kuubariki mkataba huo na wamesema ikitokea wamesaini LA LIGA basi wao wataondoa rasmi mechi zao kurushwa kwenye TV

Na leo taarifa rasmi kutoka Shirikisho la soka Hispania limesema mkataba huo ni batili na hawautambui! Hivyo Madrid na Barcelona wana support ya Shirikisho la soka
 
Kitambo nishawahi kusema hii la Liga ina mambo kama ya soka la bongo
 
Huo mkataba utawazuia kuingia super league ndio maana hawautaki
 
Real madrid sio kwamba tu wamepinga hiyo deal kati ya LA Liga na CVC, bali wamewafungulia mashtaka, so kama wengine wata support hiyo ishu kuna uwezekano La Liga wakafeli kwenye mission yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom