Utata wagubika onesho la Ray C Kagera

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Nimesoma kwenye gazeti moja linalochapishwa mkoani kagera kila wiki liitwalo Malengo Yetu toleo la leo kuwa Ray C aliwatapeli wakazi wa mkoa huo kwa kumtumia dada anayefafana naye kwa sura kufanya shoo badala yake.

lakini cha ajabu ni kuwa baadhi ya mashabiki hawakulewa mpaka walimbamba ray feki akiwa katika harakati za kuondoka kwenda kwao karagwe.

gazeti hili halipo halimo kwenye mtandao lakini nimescan habari hiyo ili kudhibitisha post yangu

hivui wasanii wanafikia kufanya uhuni wa hivi ,tutapona ?

RAY C Kagera.JPG Habari ya Ray ktk Malengo Yetu
AU unaweza kusoma gazeti hilo uk wa kwanza ingawa siyo zuri,ombo kwa wamiliki kubadilisaha ubora wa gazeti hilo HALIVUTII KABISA ebu cheki mbele
DSC05214.JPG Malengo Yetu kwa mbele
 
SHOO ZA VIJIJINI... Show nyingi zinazofanywa vijijini huwa waaandaaji wanatafuta watu ambao wanaigiza kuimba nyimbo mbalimbali za wasanii wetu,Masanja wa Ze Origino komedy,Bambo,Rose Mhando etc hilo si la ajabu... tena wengi wanawapatia au kuwazidi wasanii wenyewe... Hapa Dar tembelea Kwa Macheni,Meeda,San Cirro,Lango la Jiji,Kimboka by Night,Rozanas,Kisuma,Millenium Mbagala,Zakhem Mbagala kuna show hizo bila kusahau taarifa za habari za kurekodiwa Uwanja wa Fisi...
 
Hii second degree utapeli, ebanaee yaani wamefanana kiasi hiko kiasi watu wasimtambue? Au nao wote walitoka karagwe? So hatua iliyochukuliwa ni ipi manake unaweza kukuta kuwa Ray C hakuwa na onyessho huko bali jina lake tu ndo limetumika
 
Hilo gazeti linatoka Mkoa wa Kagera tu?, Watu wa Bukoba hebu tupeni info.

Gazeti linatolewa mkoani kagera lakini linauzwa katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga na Mara kama upo katika mikoa hiyo unaweza kulisoma lakini katika habari hiyo Ray C alihojiwa na katika maelezo yake yaliyopo katika gazeti hilo inaonesha naye alihusika katika usanii huo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom