Utata wagubika kupungua uzito kwa Kim Jong-Un

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Televisheni ya Taifa la Korea Kaskazini imerusha maoni ya wananchi kuhusu afya ya Kiongozi wa Taifa hilo, Kim Jong-un baada ya video iliyokuwa ikimwonesha kupungua uzito kusambaa, hali ya nadra kutokea nchini humo kwa afya ya kiongozi wa nchi kujadiliwa kwenye chombo cha habari.

Korea Kaskazini imejiweka katika hali ya kujitenga zaidi ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, ikikiri kuwa na uhaba wa chakula mapema mwezi huu. Wakati huo, afya yake imeendelea kugonga vichwa vya habari kimataifa, huku kifo chake, endapo kitatokea ghafla, kitazua utata wa mrithi wake na uthabiti wa taifa hilo.

Kim anayetajawa kuwa mvutaji mkubwa wa sigara, ameongezeka uzito kwa kiasi kikubwa tangu alipoingia madarakani mwaka 2011. Kufikia mwaka 2016, Kim alitajwa kuwa na uzito wa kilo 130, akiongeza kilo 40 tangu mwaka 2011. Mwaka jana pekee, aliongeza uzito wa kilo 10, na kufikisha uzito wa kilo140, kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi la Korea Kusini. Baba yake Kim, Kim Jong-il na babu yake, Kim Il-sung walikuwa na uzito mkubwa na wote walifariki kwa ugonjwa wa moyo.

“Kumwona Kiongozi wetu wa Taifa akiwa amepungua uzito kumetusikitisha mno,” raia mmoja wa Korea Kaskazini alionekana katika Televisheni ya Taifa akizungumzia afya ya Kim. “Kila mtu anazungumzia jinsi alivyotokwa na machozi baada ya kuona hali yake ya afya,” alisema raia huyo.

Wachambuzi wanasema propaganda hiyo inalenga kuufikirisha ulimwengu kuwa raia wa Korea Kaskazini wanampenda kiongozi wao kufikia kiasi cha kutokwa na machozi baada ya kuona hali yake ya kiafya. Propaganda hiyo inalenga pia kumtukuza Kim na kumfanya aonekane mchapakazi kiasi cha kukosa muda wa kula kutokana na kazi nyingi.

Kupungua uzito kwa Kim katika siku za hivi karibuni hakuhusianishwi na ugonjwa, kwani ameweza kuhudhuria matukio muhimu ya kitaifa mwezi huu.

Maisha ya Kim pamoja na afya yake ni mwiko kuzungumzwa hadharani nchini Korea Kaskazini. Mamlaka za Pyongyang hazijawahi kuthibitisha idadi ya watoto alionao.

Chanzo: AFP

1624877528226.png
 
Back
Top Bottom