UTATA wa MABILLIONI ya EPA: Ni kiasi gani kilichorudishwa na mafisadi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
$25m properties nabbed over BoT fraud

home+sub+1+pix.jpg

The Bank of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.

By MIKE MANDE, JOSEPH MWAMUNYANGE and WILFRED EDWIN
THE EAST AFRICAN

August 23 2008 at 08:15

The Tanzanian government has confiscated property worth more than $25 million from 13 firms in a massive crackdown against people involved in the multimillion EPA scandal.

The seized assets include four brand new Range Rover Vogue Supercharger 2006 Model cars - each valued at $136,916 - with a total value of $547,664 and four Mercedez Benz CLK 230 Kompressor Model cars - each valued at $28,139 - with a total value of $112,556.

Other properties include apartments, hotels, petrol stations, real estate firms in Dar es Salaam, Arusha and Mwanza and plots in prime areas of Dar es Salaam valued at $25 million.

The government is now preparing charges against the culprits whose cases will start in November this year. The properties were seized under the Emergency Powers Act.

"We have confiscated the properties of those people allegedly being involved in External Payment Arrears Accounts (EPA) of the Central Bank who have become extremely wealthy by corrupt means," said President Jakaya Kikwete last week. "No one will be spared."

The president said that individuals implicated in siphoning funds from the EPA account have up to November 1 to return the money or face prosecution.

President Kikwete said that so far, Tsh64.8 billion ($56 million) has been recovered by the team and returned to the government, which has now created an account for the EPA money away from the Central Bank.

"The Attorney General and his team recommended that the time for recovery of the said funds be extended to October 31, 2008 so as to give room for those that had requested for an extension to return the money, to do so," he said.

He added: "But after November 1, 2008 all those who fail to return the money will be prosecuted. As for the other nine firms for which the committee was still seeking Interpol's help, we will have to wait until such time that the police get the necessary information in order for further action to be taken against them."

The president said that there would be no extension of the October 31 deadline.

The nine firms were said to have obtained the money from the Central Bank but lacked any kind of documents authorising them to access the EPA account.

In order to maintain checks and balances at the Central Bank, the president said the Governor is no longer the chairman of the Board. Auditing of the bank would thus be done with a broader representation.

President Kikwete revealed that some of the recovered money would be utilised to support farming by providing affordable fertiliser. Some Tsh20 billion ($11.5 million) will go to the Tanzania Investment Bank (TIB) to enhance its capacity to lend to the agricultural sector.

Other recommendations by the three-man team which investigated the scandal were that the government should establish a link between the parent ministry (Finance) and the Central Bank, some of the governor's powers be diluted to encourage good governance, disciplinary action be taken against bank officers who facilitated the transactions and that further investigations be carried out on the nine firms.

Although the move to confiscate the properties is widely applauded, some government critics have accused the government of lacking moral obligation to prosecute those who have returned the money.

Dr Willibrod Slaa, a Chadema MP, said last week that the government should have prosecuted those who were found to have been involved in the scandal, and not just make them repay.

He said that although some measures have been taken, there is no word from the president whether the fraudsters who have returned the stolen money will be taken to court.

The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, said President Kikwete should have adopted a tougher approach in dealing with serious allegations of grand corruption in the country, and that there should be no let up in the fight against graft.

Mr Sitta said the government must become extra brutal in dealing with high-level corruption in the corridors of power.

"It appears that more importance is being placed on individual rights than national interests. There is no such thing as the human rights of an individual involved in economic sabotage being violated," he said.

According to Mr Sitta, the government should get tough on looters as ordinary people may find it hard to comprehend if individuals implicated in massive scandals are found walking freely in the streets.

The Kigoma North MP, Zitto Kabwe, said if President Kikwete had given amnesty to EPA money looters, proper procedures should have been followed and parliament officially notified over the decision.

"He did not say what action would be taken against the EPA suspects after they return the stolen money," he said.
 
Je, tunaweza kupata breakdown ya hizo assets zilizofilisiwa toka kwa mafisadi? Kama ni nyumba au mahoteli basi address zake zitolewe pamoja na thamani ya nyumba hizo, na kama ni magari basi model ya magari hayo na mwaka wa kila gari viwekwe hadharani na pia tunataka kujua ni nani aliyetathmini thamani ya nyumba hizo na magari hayo ili tuone kama hiyo thamani ya mali zilizofilisiwa ni kweli inafika $25 million au ni usanii wa JK na serikali yake.
 
Na ile Range Rover ya Malegesi iliyoletwa kwa ndege nayo imetaifishwa?
 
Je, tunaweza kupata breakdown ya hizo assets zilizofilisiwa toka kwa mafisadi? Kama ni nyumba au mahoteli basi address zake zitolewe pamoja na thamani ya nyumba hizo, na kama ni magari basi model ya magari hayo na mwaka wa kila gari viwekwe hadharani na pia tunataka kujua ni nani aliyetathmini thamani ya nyumba hizo na magari hayo ili tuone kama hiyo thamani ya mali zilizofilisiwa ni kweli inafika $25 million au ni usanii wa JK na serikali yake.

The seized assets include four brand new Range Rover Vogue Supercharger 2006 Model cars — each valued at $136,916 — with a total value of $547,664 and four Mercedez Benz CLK 230 Kompressor Model cars — each valued at $28,139 — with a total value of $112,556.
[/size][/color]

Mkulu uwa unasoma unachocopy and paste au unaweka tu?
 
Mkulu uwa unasoma unachocopy and paste au unaweka tu?

Nasoma mkuu, lakini inawezekana hizo ni estimations tu ambazo haziko sahihi, ndiyo maana nimeomba list ya mali zote na kujua nani aliyezifanyia tathmini, si ajabu hayo magari ya 2006 thamani yake imeshashuka kutokana na depreciation, si ajabu hizo nyumba zima thamani ya $5 million tu, lakini tukiambiwa tathmini imefanywa na mtaalamu toka pale chuo kikuu cha Ardhi basi tutaamini, lakini hivi hivi tu itakuwa ni usanii. Kumbuka wametwambia wamekusanya $60 billioni lakini hadi hii leo wameshindwa kutoa majina ya waliorudisha na amount iliyorudishwa na kila mhusika na kutwambia pesa hizo zimewekwa wapi.
 
Je, tunaweza kupata breakdown ya hizo assets zilizofilisiwa toka kwa mafisadi? Kama ni nyumba au mahoteli basi address zake zitolewe pamoja na thamani ya nyumba hizo, na kama ni magari basi model ya magari hayo na mwaka wa kila gari viwekwe hadharani na pia tunataka kujua ni nani aliyetathmini thamani ya nyumba hizo na magari hayo ili tuone kama hiyo thamani ya mali zilizofilisiwa ni kweli inafika $25 million au ni usanii wa JK na serikali yake.

Natumai upinzani utasoma maswali uliyouliza na ni vyema wakianza kuhoji kwa kutumia point hizi. Siyo kusema vaguely eti wachukuliwe hatua but ask the right questions. Hivi kati yao hakuna wanasheria? Akina Mvungi wanatakiwa kujua kuwa ni vyema kuuliza maswali ambayo baadaye yatakuja kuwa bana. Kwa mfano model ya magari haitoshi peke yake, ni lazima tujue imetumika miaka mingapi? Na kama ulivyosema engine number etc ziwekwe hadharani, kama waliuza kwenye mnada ilikuwa lini na nani alinunua?
Usanii wa serikali yetu tumeuchoka!
 
Not good enough.

I'm afraid the public only wants names. Name and shame the callous plunderers of this deeply impoverished nation
 
$25m properties nabbed over BoT fraud

home+sub+1+pix.jpg

The Bank of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.

By MIKE MANDE, JOSEPH MWAMUNYANGE and WILFRED EDWIN
THE EAST AFRICAN

August 23 2008 at 08:15

The Tanzanian government has confiscated property worth more than $25 million from 13 firms in a massive crackdown against people involved in the multimillion EPA scandal.

The seized assets include four brand new Range Rover Vogue Supercharger 2006 Model cars — each valued at $136,916 — with a total value of $547,664 and four Mercedez Benz CLK 230 Kompressor Model cars — each valued at $28,139 — with a total value of $112,556.

Other properties include apartments, hotels, petrol stations, real estate firms in Dar es Salaam, Arusha and Mwanza and plots in prime areas of Dar es Salaam valued at $25 million.

The government is now preparing charges against the culprits whose cases will start in November this year. The properties were seized under the Emergency Powers Act.

“We have confiscated the properties of those people allegedly being involved in External Payment Arrears Accounts (EPA) of the Central Bank who have become extremely wealthy by corrupt means,” said President Jakaya Kikwete last week. “No one will be spared.”

The president said that individuals implicated in siphoning funds from the EPA account have up to November 1 to return the money or face prosecution.

President Kikwete said that so far, Tsh64.8 billion ($56 million) has been recovered by the team and returned to the government, which has now created an account for the EPA money away from the Central Bank.

“The Attorney General and his team recommended that the time for recovery of the said funds be extended to October 31, 2008 so as to give room for those that had requested for an extension to return the money, to do so,” he said.

He added: “But after November 1, 2008 all those who fail to return the money will be prosecuted. As for the other nine firms for which the committee was still seeking Interpol’s help, we will have to wait until such time that the police get the necessary information in order for further action to be taken against them.”

The president said that there would be no extension of the October 31 deadline.

The nine firms were said to have obtained the money from the Central Bank but lacked any kind of documents authorising them to access the EPA account.

In order to maintain checks and balances at the Central Bank, the president said the Governor is no longer the chairman of the Board. Auditing of the bank would thus be done with a broader representation.

President Kikwete revealed that some of the recovered money would be utilised to support farming by providing affordable fertiliser. Some Tsh20 billion ($11.5 million) will go to the Tanzania Investment Bank (TIB) to enhance its capacity to lend to the agricultural sector.

Other recommendations by the three-man team which investigated the scandal were that the government should establish a link between the parent ministry (Finance) and the Central Bank, some of the governor’s powers be diluted to encourage good governance, disciplinary action be taken against bank officers who facilitated the transactions and that further investigations be carried out on the nine firms.

Although the move to confiscate the properties is widely applauded, some government critics have accused the government of lacking moral obligation to prosecute those who have returned the money.

Dr Willibrod Slaa, a Chadema MP, said last week that the government should have prosecuted those who were found to have been involved in the scandal, and not just make them repay.

He said that although some measures have been taken, there is no word from the president whether the fraudsters who have returned the stolen money will be taken to court.

The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, said President Kikwete should have adopted a tougher approach in dealing with serious allegations of grand corruption in the country, and that there should be no let up in the fight against graft.

Mr Sitta said the government must become extra brutal in dealing with high-level corruption in the corridors of power.

“It appears that more importance is being placed on individual rights than national interests. There is no such thing as the human rights of an individual involved in economic sabotage being violated,” he said.

According to Mr Sitta, the government should get tough on looters as ordinary people may find it hard to comprehend if individuals implicated in massive scandals are found walking freely in the streets.

The Kigoma North MP, Zitto Kabwe, said if President Kikwete had given amnesty to EPA money looters, proper procedures should have been followed and parliament officially notified over the decision.

“He did not say what action would be taken against the EPA suspects after they return the stolen money,” he said.

Bado ni sanaa na propaganda ya kuonyesha kwamba JK kafanya kweli. Hakuna aliyekamatiwa mali labda kama sasa wameambiwa wazifiche. Lakini jambo la msingi, kama umekamata mali zake, unasubiri alipe kutoka wapi? Kama umeshikilia akaunti zake, unataka alipe fedha kutoka wapi? kama hana hata pasi ya kusafiria, unataka alipe kutoka wapi? Lakini kwa kuwa umekamata mali zake na kwa kuwa emetenda kosa la jinai (kughushi, kuiba) kwanini hawapelekwi mahakamani? Yaani hapo juu anasema wasiolipa ndio watakaopelekwa mahakamani, waliolipa basi waendelee kutesa. Haiingii akilini
 
Hakuna alie msafi katika serikali yake ndio maaana anaogopa ku take action....heri tukae kwenye serikali ya jeshi hata kwa miaka 5 tuwe na uzalendo......porojo zimezidi sasaa
 
Date::8/25/2008
Mabilioni ya EPA utata mtupu

*Ni kutokana na takwimu za marejesho kutofautiana

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

WAKATI uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete, kuongeza muda wa kulipa fedha kwa watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) ukiibua mjadala mzito, imebainika kuwa fedha alizotaja ni chache ikilinganishwa na zilizotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, kwa ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Utata huo umeibuka baada ya Rais Kikwete kusema wakati akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita kwamba, mpaka sasa fedha zilizokusanywa ni Sh53 bilioni, ambazo ni pungufu kwa kiasi cha Sh60 bilioni alizotangaza Mkulo kwa wafadhili na zile alizotaja Mwenyekiti wa Timu hiyo ya Rais, Johnson Mwanyika mbele ya wahariri wa vyombo vya habari hapo Machi, 13, mwaka huu.

Uchunguzi wa taarifa tofauti zilizotolewa na serikali, umebaini kuwa kiwango hicho cha Sh53 bilioni alichotaja Rais Kikwete pia kinatofautiana na kiasi cha Sh64 bilioni kilichotangazwa na Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ndiyo msimamizi na mtekelezaji wa maagizo yote ya chama hicho tawala.

Hata hivyo, alipoulizwa Mkulo jana kwa njia ya simu kwamba taarifa zake za awali kwa IMF zilitoka katika chanzo kipi, alikuwa akihoji: "Hivi wewe unataka niseme nini wakati Rais amekwisha zungumza bungeni?"

Mkulo alijitetea kwamba, kitendo chochote cha yeye kuzungumzia suala hilo ni sawa na utovu wa nidhamu kwa Rais hivyo hawezi kusema lolote.

Hata hivyo, alipoelezwa kwamba azma si kuzungumzia mchakato bali kujua alipoeleza watendaji wa IMF alikuwa na taarifa kutoka chanzo kipi kwani anaonekana kuwaingiza gizani wafadhili na umma kwa ujumla, alijibu: "Hivi wewe ukoje, sina la kusema."

Mkulo licha ya kukwepa, lakini wakati timu ikiwa kati kati ya uchunguzi wake, Aprili, mwaka huu alieleza watendaji wa IMF kwamba kulikuwa na kiasi cha Sh60 bilioni ambacho Timu ya Rais ilikuwa imekikusanya.

Hata hivyo, kiwango hicho ambacho kilitangazwa mbele ya watendaji wa ngazi za juu wa IMF, kinatofautiana kwa takriban Sh7 bilioni ikilinganishwa na zilizotajwa na rais wakati akihutubia umma kupitia bungeni.

Tofauti hiyo inaibua utata zaidi, kwani Mkulo, Mwanyika na CC-CMM kwa pamoja walitoa takwimu hizo, Timu Rais ikiwa haijamaliza kazi yake ya uchunguzi na matokeo yake takwimu alizopewa na Rais kuzitangaza baada ya timu kumaliza kazi zikawa na utofuati mkubwa unaosababisha utata kwamba, takwimu sahihi ni ipi kwani zote zilitoka kwenye vyanzo hivyo hivyo.

Mbali na Waziri Mkulo, Mwanyika alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na marejesho ya fedha hizo katika Hoteli ya Movenpick, alisema kazi ya kuchunguza mali ikiwemo majumba ndani na nje ilikuwa ikiendelea.

Mwanyika ambaye alizungumza akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, alisema siku hiyo wakati akija kulikuwa na matarajio ya kwamba zilikuwepo Sh60 bilioni.

Katika mkutano huo ambao IGP Mwema aliwafananisha watuhumiwa wa EPA na magaidi hatari wanaoweza kuilipua nchi wakifuatiliwa kizembe, Mwanyika alisema fedha zilizokusanywa zimewekwa kwenye akaunti maalumu ambayo hakuitaja ilipo (benki).

Hata hivyo, taarifa ya Mwanyika ilitofautiana na iliyotolewa Machi 13, mwaka huu na CC ya CCM ambayo ilisema Sh64 bilioni zilikuwa zimekusanywa.

Taarifa hiyo ya CCM iliyotiwa saini na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Kapteni John Chilligati, iliisifia Timu ya Rais kwa kazi nzuri kwa maelezo kwamba ilikuwa imekusanya kiasi cha Sh 64 bilioni, ambazo ni nyingi.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kilichofanyika chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete, jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali, likiwamo suala hilo.

Sehemu ya taarifa ya CC-CCM ilisema: "Timu hiyo inaendelea kuzibana kampuni husika kurejesha fedha zilizochukuliwa kwa njia haramu. Hadi sasa timu imefanikisha kurejeshwa kwa jumla ya Sh 64 bilioni."

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Timu ya Rais ilikuwa ikiendelea kuwabainisha wanahisa wote wa makampuni yaliyochukua fedha hizo kwa njia za udanganyifu na hasa wahusika wakuu wa uchukuaji wa fedha hizo za EPA.

Kwa kufanya uchunguzi katika taarifa hizi tatu, imebainika hadi sasa bado mabilioni ya EPA yamebaki kuwa suala tata.

Maswali zaidi yanajitokeza, kubwa ikiwa taarifa kati ya hizo ipi ni sahihi na kwamba je, Mkulo aliwadanganya wafadhili, au Timu ya Rais ilidanganya umma ilipotoa taarifa yake kwa wahariri au Rais amedanganywa na timu?

Ufisadi katika EPA ambayo ilifunguliwa wakati wa ujamaa kuziba pengo la ukosefu wa bidhaa uliotokana na ukosefu wa fedha za kigeni, ulijitokeza katika kipindi cha mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi wa kimataifa chini ya Kampuni ya Ernst&Young.

Kabla ya Arnst&Young, tayari Kampuni ya Deloitte &Touche ilikwishaanza ukaguzi na kubaini ufisadi huo, hasa Sh40 bilioni ambazo zililipwa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture, lakini ghafla mkataba wake na BoT ukasitishwa.

Baada ya kubainika ufisadi huo, Rais Kikwete alitengua mkataba wa aliyekuwa gavana wa Benki Kuu, marehemu Daud Ballali na kumteua gavana mpya na kuunda timu maalumu ya kuchunguza na kuhakikisha fedha zinarudishwa na watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Hata hivyo, baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi hapo Agosti 18, akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita pamoja na mambo mengine Rais Kikwete alisema fedha zilizokusanywa zilikuwa Sh53 bilioni na kuwaongeza muda watuhumiwa ambao hawajarejesha fedha hizo hadi Oktoba 31, mwaka huu vinginevyo Novemba mosi watafikishwa mahakamani.
 
Zitto nakubaliana na wewe hizo pesa haziko ndiyo maana wameshindwa kuweka majina ya waliorudisha pesa hizo hadharani. Watachomoa pesa toka hazina ili watuzuge, lakini tukiwadai list ya majina ufisadi wao utakuwa mgumu kuukamilisha

Zitto: Pesa za EPA hazipo

na Edward Kinabo
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hadi sasa taifa halipaswi kuamini kuwa fedha zilizoibwa kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), zimerejeshwa hadi hapo itakapothibitishwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma, Zitto alisema kauli ya Rais Kikwete kuwa fedha za EPA zielekezwe kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, inatia shaka iwapo kweli zimerejeshwa na zitaendelea kurejeshwa.

Alisema kauli hiyo ina makosa makubwa na inaibua mashaka kuhusu uwepo wa fedha zenyewe, kwani maeneo ambayo rais amesema fedha hizo zielekezwe, ni maeneo ambayo hayawajibiki kwa Bunge, hali inayoweka kikwazo cha kujua kama kweli wezi wa EPA wamerejesha fedha hizo.

“Inawezekana kabisa serikali ikaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia TRA na kupata sh bilioni 133, halafu ikazielekeza kwenye Mfuko wa Pembejeo na TIB na tukaambiwa kuwa hizi ndizo fedha za EPA zilizorejeshwa, kumbe sivyo,” alisema.

Alisema kazi ya kupanga matumizi ya fedha za umma ni ya Bunge na si ya rais na kwamba alichopaswa kufanya ni kuliomba Bunge liidhinishe matumizi ya fedha hizo kwa Waziri wa Fedha kuwasilisha muswada bungeni.

“Alichopaswa rais kukitamka ni kuwa serikali yake inakusudia kuleta muswada wa matumizi wa fedha hizo bungeni ili kuliomba Bunge likubali kuidhinisha na si kutoa amri kuwa fedha hizo zielekezwe kwenye Mfuko wa Pembejeo na kwenye Benki ya TIB,” alisema.

Zitto alisema, TIB haiwajibiki bungeni na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo nao hauwajibiki bungeni, bali unawajibika kwa bodi yake na Bunge halitaweza kukagua fedha hizo.

Alisema, rais amekiuka utaratibu kwa kutoa amri ya kuzielekeza fedha hizo katika maeneo ambayo kimsingi hayawezi kujadiliwa na Bunge, hivyo taifa lina sababu ya kutilia shaka urejeshwaji wa fedha hizo hadi hapo serikali itakapokuwa wazi zaidi.

Akizungumzia uchumi, Zitto alisema, Rais Kikwete hakupaswa kuishia kujisifu kuwa uchumi unakua, bali alipaswa kueleza ni kwa kiasi gani amefanikiwa kumfanya mwananchi wa kawaida anufaike na uchumi huo.

“Hata Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliacha uchumi mpana, ukikua katika kasi ya kuridhisha, kwa hiyo jukumu la serikali ya Kikwete lilikuwa kuhakikisha ukuaji huo unaboresha maisha ya mwananchi, kitu ambacho hajakifanya hadi sasa licha ya kuahidi maisha bora kwa kila Mtanzania,” alisema.

Alisema serikali imeshindwa kupata suluhisho la kuboresha kilimo nchini na ndiyo maana uchumi unakua lakini wananchi wengi ni wakulima wa vijijini na hali zao za maisha bado duni.

Alisema ili Watanzania waweze kuwa na maisha bora, sekta ya kilimo inabidi ikue kwa asilimia nane hadi kumi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

“Kwa umaskini tulionao, kuna haja ya serikali na wadau nchini kufanya mapitio ya kuboresha Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) ili uchangie zaidi maendeleo ya vijijini, hususan katika sekta ya kilimo na miundombinu,” alisema.

“Kwa mfano, hivi sasa kuna mfumuko wa bei lakini mkulima wa kijijini bado analazimika kuuza mazao yake kwa bei ndogo ya kijijini, lakini mkulima huyo anaponunua bati au mbolea vinavyopatikana mjini, anakuta ni ghali sana,” alisema.

Alisema tatizo la serikali ya Kikwete ni kuutazama uchumi katika mtazamo wa uchumi wa mjini tu ‘urban economy’ na kusahau mambo ya msingi ambayo yanaweza kuchochea uchumi wa vijijini ‘rural economy’, kama kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa wingi, kushughulikia bei na masoko ya wakulima, na ujenzi wa miundombinu ya barabara na maji vijijini.

“Hivi sasa ni asilimia tatu tu ya wakulima nchini ndio wanapata mikopo ya kilimo, asilimia 18% ya wakulima ni wale wanaotegemea msaada wa ndugu, jamaa na marafiki wenye uwezo kuwasaidia gharama za kilimo, mathalani unakuwa na ndugu yako anaishi mjini anakununulia mbolea ndipo unalima. Kuna haja ya kuwa na mwelekeo wa kisera katika kilimo, hatuwezi kufanikiwa tukiendelea hivi. Hatuzalishi, ebu jiulize, tupo wabunge wengi, lakini ni wangapi wana mashamba?” alihoji Zitto.
 
PESA ZA EPA huenda zimehusika kwenye Party la juzi kwenye harusi sasa mnahojihoji nini?

Party si rahisi maana watu wametoka bila kula, msosi ulichelewa kishenzi kwa sisi wenye njaa mbaya tuliwahi kutoka sijui wenzetu walobaki kama walikula. Lakini tunaambiwa Lau Masha, alikwenda kupeleka zawadi akiwa na "WAFANYAKAZI WENZAKE WA IMMA ADVOCATES" sasa watu wakajiuliza, si alisema ameondoka? Yeye ni Waziri au mfanyakazi/partner wa IMMA?
 
Tujukumbushe, je, kati ya hawa nani aliyefilisiwa?



Siri kashfa ya EPA zafichuka

January 17, 2008


na Tamali Vullu na Irene Mark


SIRI za kampuni zinazotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu wa shilingi bilioni 133 kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimeanza kufichuka.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa, kampuni nne kati ya 20 zilizo katika orodha hiyo zinamilikiwa na mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya kiasia, Jayantkumar Chandubhai Patel.

Aidha, uchunguzi huo umebaini pia kwamba, mmoja kati ya wakurugenzi wa kampuni moja zinazotajwa katika sakata hilo ni kiongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kigogo huyo wa CCM anatajwa kumiliki kampuni moja na aliyepata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sigara Tanzania.

Mbali ya ugunduzi huo, Tanzania Daima imebaini pia kuwa, jalada la moja ya kampuni zilizotajwa kujipatia fedha kwa hila kupitia akaunti hiyo ya malipo ya madeni ya nje iitwayo Changanyikeni Resort Complex yenye namba za usajili 47792, halionekani katika ofisi za Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA).

Changanyikeni, inayotajwa kuwa ni kampuni inayomilikiwa na mmoja wa watu maarufu (jina tunalo), ni miongoni mwa kampuni 20 zilizotajwa katika taarifa ya Kampuni ya Ukaguzi ya nje ya Ernst & Young kwamba jalada lake linapatikana BRELA.

Lakini, licha ya kufuatilia tangu majina ya makampuni hayo yalipowekwa hadharani, Tanzania Daima, imeshindwa kulipata jalada la kampuni hiyo.

Aidha, Tanzania Daima ilifanya juhudi za kuzungumza na Naibu Msajili wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, Andrew Mkapa, kuhusu kutopatikana kwa jalada la kampuni hiyo ya Changanyikeni, lakini ilishindikana.

Gazeti hili halikuruhusiwa kuonana na Mkapa, baada ya Katibu Muhtasi wake kuzungumza naye kwa njia ya simu na kuwataka waandishi wa habari hizi kuonana na msaidizi wake, aliyejulikana kwa jina la Rehema Kitambi.

?Bosi hapa kuna waandishi wa Tanzania Daima, wanataka kukuona kuhusu jalada la Changanyikeni,? alisikika Katibu Muhtasi huyo akimweleza bosi wake.

Baada ya maelezo hayo, Katibu wa Mkapa, aliwataka waandishi wa habari hizi kukumwona msaidizi wa Mkapa kwenye chumba namba 405 jirani na ofisi hiyo.

Hata hivyo, msaidizi huyo hakupatikana na mmoja wa watumishi waliokuwamo ndani ya ofisi hiyo aliwaeleza waandishi kwamba Rehema yupo mkutanoni na haifahamiki atarejea ofisini saa ngapi.

Mbali na jalada la kampuni hiyo kukosekana, Tanzania Daima ilifanikiwa kuona majalada ya kampuni nyingine 14 na kupata majina ya wamiliki wake.

Kampuni hizo ni Ndovu Soap Limited ambayo wamiliki wake ni Jayantulal Chandubhai Patel na Sidik Yacoubu yenye namba za usajili 20536 ambayo ilisajiliwa Februari 3, 1992.

Nyingine na wamiliki wake wakiwa kwenye mabano ni Excellent Service Limited (Emil Samanya Peter Sabas na Elisifa Ngowi), iliyosajiliwa Mei 13, 1992 na kupewa namba 26959. Liqiud Service Limited (Rajab Maranda na Thabit Katunda) ambayo usajili wake ulifanyika Desemba 12, 2004 na kupewa namba 15007.

Clyton Marketing (Edwin Mtoi na Elisifa Ngowi) iliyosajiliwa Juni 6, 2005, Bora Hotels and Apartments (Jayantkumar Chandubhai Patel na Devandra Patel), ilisajiliwa Septemba 8, 2005, Bina Resort Limited (Jayantikumar Chandubhai Patel na Devendra Patel) iliyosajiliwa Machi 31, 2005.

Nyingine ni Njake Hotels & Tours ya mjini Arusha (Japhet Lema, Anna Lema, Abel Lema, Derick Lema na Benard Lema ambao nao ni wakazi wa Arusha) iliyosajiliwa Aprili 10, 2003, Maltan Mining Company (Jantkumar Chandubhai Patel na Hariharier Radhakrishna) iliyosajiliwa Machi 8, 1993 na Navy Cut Tobacco (Jantkumar Chandubhai Patel na Radakrishna) iliyosajiliwa Oktoba 12, mwaka 1995.

Kampuni nyingine ni Bencon Limited, B.V Holdings, Venus Hotels na V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel, ambazo zote zilisajiliwa Aprili 4, 2005 na Kampuni ya Karnel Meals Holdings Ltd inayomilikiwa na John Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukaza ambayo usajili wake ulipatikana Agosti 4, 1998.

Awali, Mkapa alizitaja kampuni nyingine kuwa ni Kagoda Agriculture, inayomilikiwa na John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis William anayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo.

Nyingine ni Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 ambayo inamilikiwa na Kizza Selemani na Farijala Hussein, Malegesi Law Chambers inayomilikiwa na Beredy Malegesi ambayo ilisajiliwa Septemba 24, 2001.

Wamiliki wengine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki Kampuni ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi 22, 2005 na Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8, 2005.

Makampuni hayo yalibainika kuwa yalilipwa zaidi ya sh bilioni 133 isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) iliyopo BoT.

Hayo yamebainika baada ya Kampuni ya Ernst & Young kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wake serikalini.

Baada ya kuisoma ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Ballali kutokana na kasoro zilizobainishwa.

Aidha, kutokana na kasoro zilizobainishwa na mkaguzi huyo, Rais Kikwete aliiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu kukutana haraka, ili kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wanaotuhumiwa kuhusika na kulisababishia hasara taifa.

Pamoja na hatua hiyo, rais alisimamisha shughuli za ulipaji wa madeni kupitia akaunti ya EPA, hadi taratibu za uhakiki wa malipo hayo utakapotengenezwa upya.

Rais pia alimwagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuongoza kazi ya uchunguzi wa tuhuma za kampuni akishirikiana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aliwapa muda wa miezi sita kukamilisha uchunguzi huo na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuhusika na wizi huo.

Pamoja na mambo mengine, Mwanasheria Mkuu na timu yake wanatakiwa kuhakikisha kuwa, fedha zote zilizolipwa isivyo halali kwa kampuni hizo zinarudishwa serikalini.

Tuhuma za ufisadi na ubadhirifu wa BoT zilitolewa hadharani na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2007/08 na baadaye akawasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kulichunguza suala hilo.


https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=2670&page=102

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/1/17/print.php/8011702.php
 
Jamani kuweni waagalifu sana na hii habari ya kukamatwa mali za watuhumiwa. Ndiyo ni kweli mali hizi zilikamatwa mnamo mwanzoni mwa "Operation EPA" lakini sheria inasema mali ikamatwe sio zaidi ya miezi sita. Ndio maana wengi wao sasa wanaeda kwenye vyombo husika kusema sheria ifuate mkondo wake. Mmoja wao ni Malegesi ambaye sasa akaunti zake zimefunguliwa baada ya kuwabana wahusika. Chunguzeni mtapata ukweli. Wengine wako mbioni kupambana ili mali zao ziachiliwe vile vile. Hata hivyo hizi mali ni sehemu ndogo sana ya EPA. Vile vile Kamati ya Mwanyika ilizubaa kiasi fulani kukamata pesa taslimu na baadhi ya mafisadi walizificha nje hasa China!
 
Back
Top Bottom