UTATA wa MABILLIONI ya EPA: Ni kiasi gani kilichorudishwa na mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTATA wa MABILLIONI ya EPA: Ni kiasi gani kilichorudishwa na mafisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 24, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,183
  Trophy Points: 280
  $25m properties nabbed over BoT fraud

  [​IMG]
  The Bank of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.

  By MIKE MANDE, JOSEPH MWAMUNYANGE and WILFRED EDWIN
  THE EAST AFRICAN

  August 23 2008 at 08:15

  The Tanzanian government has confiscated property worth more than $25 million from 13 firms in a massive crackdown against people involved in the multimillion EPA scandal.

  The seized assets include four brand new Range Rover Vogue Supercharger 2006 Model cars - each valued at $136,916 - with a total value of $547,664 and four Mercedez Benz CLK 230 Kompressor Model cars - each valued at $28,139 - with a total value of $112,556.

  Other properties include apartments, hotels, petrol stations, real estate firms in Dar es Salaam, Arusha and Mwanza and plots in prime areas of Dar es Salaam valued at $25 million.

  The government is now preparing charges against the culprits whose cases will start in November this year. The properties were seized under the Emergency Powers Act.

  "We have confiscated the properties of those people allegedly being involved in External Payment Arrears Accounts (EPA) of the Central Bank who have become extremely wealthy by corrupt means," said President Jakaya Kikwete last week. "No one will be spared."

  The president said that individuals implicated in siphoning funds from the EPA account have up to November 1 to return the money or face prosecution.

  President Kikwete said that so far, Tsh64.8 billion ($56 million) has been recovered by the team and returned to the government, which has now created an account for the EPA money away from the Central Bank.

  "The Attorney General and his team recommended that the time for recovery of the said funds be extended to October 31, 2008 so as to give room for those that had requested for an extension to return the money, to do so," he said.

  He added: "But after November 1, 2008 all those who fail to return the money will be prosecuted. As for the other nine firms for which the committee was still seeking Interpol's help, we will have to wait until such time that the police get the necessary information in order for further action to be taken against them."

  The president said that there would be no extension of the October 31 deadline.

  The nine firms were said to have obtained the money from the Central Bank but lacked any kind of documents authorising them to access the EPA account.

  In order to maintain checks and balances at the Central Bank, the president said the Governor is no longer the chairman of the Board. Auditing of the bank would thus be done with a broader representation.

  President Kikwete revealed that some of the recovered money would be utilised to support farming by providing affordable fertiliser. Some Tsh20 billion ($11.5 million) will go to the Tanzania Investment Bank (TIB) to enhance its capacity to lend to the agricultural sector.

  Other recommendations by the three-man team which investigated the scandal were that the government should establish a link between the parent ministry (Finance) and the Central Bank, some of the governor's powers be diluted to encourage good governance, disciplinary action be taken against bank officers who facilitated the transactions and that further investigations be carried out on the nine firms.

  Although the move to confiscate the properties is widely applauded, some government critics have accused the government of lacking moral obligation to prosecute those who have returned the money.

  Dr Willibrod Slaa, a Chadema MP, said last week that the government should have prosecuted those who were found to have been involved in the scandal, and not just make them repay.

  He said that although some measures have been taken, there is no word from the president whether the fraudsters who have returned the stolen money will be taken to court.

  The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, said President Kikwete should have adopted a tougher approach in dealing with serious allegations of grand corruption in the country, and that there should be no let up in the fight against graft.

  Mr Sitta said the government must become extra brutal in dealing with high-level corruption in the corridors of power.

  "It appears that more importance is being placed on individual rights than national interests. There is no such thing as the human rights of an individual involved in economic sabotage being violated," he said.

  According to Mr Sitta, the government should get tough on looters as ordinary people may find it hard to comprehend if individuals implicated in massive scandals are found walking freely in the streets.

  The Kigoma North MP, Zitto Kabwe, said if President Kikwete had given amnesty to EPA money looters, proper procedures should have been followed and parliament officially notified over the decision.

  "He did not say what action would be taken against the EPA suspects after they return the stolen money," he said.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,183
  Trophy Points: 280
  Je, tunaweza kupata breakdown ya hizo assets zilizofilisiwa toka kwa mafisadi? Kama ni nyumba au mahoteli basi address zake zitolewe pamoja na thamani ya nyumba hizo, na kama ni magari basi model ya magari hayo na mwaka wa kila gari viwekwe hadharani na pia tunataka kujua ni nani aliyetathmini thamani ya nyumba hizo na magari hayo ili tuone kama hiyo thamani ya mali zilizofilisiwa ni kweli inafika $25 million au ni usanii wa JK na serikali yake.
   
 3. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bubu!!!
  achana na hizi porojo ndugu yangu
  Hakuna kitu kama hicho jamani huu ni usanii ndani ya serikali jamani
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na ile Range Rover ya Malegesi iliyoletwa kwa ndege nayo imetaifishwa?
   
 5. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Mkulu uwa unasoma unachocopy and paste au unaweka tu?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,183
  Trophy Points: 280
  Nasoma mkuu, lakini inawezekana hizo ni estimations tu ambazo haziko sahihi, ndiyo maana nimeomba list ya mali zote na kujua nani aliyezifanyia tathmini, si ajabu hayo magari ya 2006 thamani yake imeshashuka kutokana na depreciation, si ajabu hizo nyumba zima thamani ya $5 million tu, lakini tukiambiwa tathmini imefanywa na mtaalamu toka pale chuo kikuu cha Ardhi basi tutaamini, lakini hivi hivi tu itakuwa ni usanii. Kumbuka wametwambia wamekusanya $60 billioni lakini hadi hii leo wameshindwa kutoa majina ya waliorudisha na amount iliyorudishwa na kila mhusika na kutwambia pesa hizo zimewekwa wapi.
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Natumai upinzani utasoma maswali uliyouliza na ni vyema wakianza kuhoji kwa kutumia point hizi. Siyo kusema vaguely eti wachukuliwe hatua but ask the right questions. Hivi kati yao hakuna wanasheria? Akina Mvungi wanatakiwa kujua kuwa ni vyema kuuliza maswali ambayo baadaye yatakuja kuwa bana. Kwa mfano model ya magari haitoshi peke yake, ni lazima tujue imetumika miaka mingapi? Na kama ulivyosema engine number etc ziwekwe hadharani, kama waliuza kwenye mnada ilikuwa lini na nani alinunua?
  Usanii wa serikali yetu tumeuchoka!
   
 8. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Je any chance kujua majina? who are those people? au ni siri?
   
 9. C

  Chuma JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  the EPA Team are still on research!!!!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tunataka majina tuwajue wezi wetu
   
 11. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Not good enough.

  I'm afraid the public only wants names. Name and shame the callous plunderers of this deeply impoverished nation
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Bado ni sanaa na propaganda ya kuonyesha kwamba JK kafanya kweli. Hakuna aliyekamatiwa mali labda kama sasa wameambiwa wazifiche. Lakini jambo la msingi, kama umekamata mali zake, unasubiri alipe kutoka wapi? Kama umeshikilia akaunti zake, unataka alipe fedha kutoka wapi? kama hana hata pasi ya kusafiria, unataka alipe kutoka wapi? Lakini kwa kuwa umekamata mali zake na kwa kuwa emetenda kosa la jinai (kughushi, kuiba) kwanini hawapelekwi mahakamani? Yaani hapo juu anasema wasiolipa ndio watakaopelekwa mahakamani, waliolipa basi waendelee kutesa. Haiingii akilini
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Serikali inayowapigia magoti mafisadi, itakuwa na ubavu wa kuwashikisha adabu?
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hakuna alie msafi katika serikali yake ndio maaana anaogopa ku take action....heri tukae kwenye serikali ya jeshi hata kwa miaka 5 tuwe na uzalendo......porojo zimezidi sasaa
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,183
  Trophy Points: 280
  Date::8/25/2008
  Mabilioni ya EPA utata mtupu

  *Ni kutokana na takwimu za marejesho kutofautiana

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  WAKATI uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete, kuongeza muda wa kulipa fedha kwa watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) ukiibua mjadala mzito, imebainika kuwa fedha alizotaja ni chache ikilinganishwa na zilizotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, kwa ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

  Utata huo umeibuka baada ya Rais Kikwete kusema wakati akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita kwamba, mpaka sasa fedha zilizokusanywa ni Sh53 bilioni, ambazo ni pungufu kwa kiasi cha Sh60 bilioni alizotangaza Mkulo kwa wafadhili na zile alizotaja Mwenyekiti wa Timu hiyo ya Rais, Johnson Mwanyika mbele ya wahariri wa vyombo vya habari hapo Machi, 13, mwaka huu.

  Uchunguzi wa taarifa tofauti zilizotolewa na serikali, umebaini kuwa kiwango hicho cha Sh53 bilioni alichotaja Rais Kikwete pia kinatofautiana na kiasi cha Sh64 bilioni kilichotangazwa na Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ndiyo msimamizi na mtekelezaji wa maagizo yote ya chama hicho tawala.

  Hata hivyo, alipoulizwa Mkulo jana kwa njia ya simu kwamba taarifa zake za awali kwa IMF zilitoka katika chanzo kipi, alikuwa akihoji: "Hivi wewe unataka niseme nini wakati Rais amekwisha zungumza bungeni?"

  Mkulo alijitetea kwamba, kitendo chochote cha yeye kuzungumzia suala hilo ni sawa na utovu wa nidhamu kwa Rais hivyo hawezi kusema lolote.

  Hata hivyo, alipoelezwa kwamba azma si kuzungumzia mchakato bali kujua alipoeleza watendaji wa IMF alikuwa na taarifa kutoka chanzo kipi kwani anaonekana kuwaingiza gizani wafadhili na umma kwa ujumla, alijibu: "Hivi wewe ukoje, sina la kusema."

  Mkulo licha ya kukwepa, lakini wakati timu ikiwa kati kati ya uchunguzi wake, Aprili, mwaka huu alieleza watendaji wa IMF kwamba kulikuwa na kiasi cha Sh60 bilioni ambacho Timu ya Rais ilikuwa imekikusanya.

  Hata hivyo, kiwango hicho ambacho kilitangazwa mbele ya watendaji wa ngazi za juu wa IMF, kinatofautiana kwa takriban Sh7 bilioni ikilinganishwa na zilizotajwa na rais wakati akihutubia umma kupitia bungeni.

  Tofauti hiyo inaibua utata zaidi, kwani Mkulo, Mwanyika na CC-CMM kwa pamoja walitoa takwimu hizo, Timu Rais ikiwa haijamaliza kazi yake ya uchunguzi na matokeo yake takwimu alizopewa na Rais kuzitangaza baada ya timu kumaliza kazi zikawa na utofuati mkubwa unaosababisha utata kwamba, takwimu sahihi ni ipi kwani zote zilitoka kwenye vyanzo hivyo hivyo.

  Mbali na Waziri Mkulo, Mwanyika alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na marejesho ya fedha hizo katika Hoteli ya Movenpick, alisema kazi ya kuchunguza mali ikiwemo majumba ndani na nje ilikuwa ikiendelea.

  Mwanyika ambaye alizungumza akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, alisema siku hiyo wakati akija kulikuwa na matarajio ya kwamba zilikuwepo Sh60 bilioni.

  Katika mkutano huo ambao IGP Mwema aliwafananisha watuhumiwa wa EPA na magaidi hatari wanaoweza kuilipua nchi wakifuatiliwa kizembe, Mwanyika alisema fedha zilizokusanywa zimewekwa kwenye akaunti maalumu ambayo hakuitaja ilipo (benki).

  Hata hivyo, taarifa ya Mwanyika ilitofautiana na iliyotolewa Machi 13, mwaka huu na CC ya CCM ambayo ilisema Sh64 bilioni zilikuwa zimekusanywa.

  Taarifa hiyo ya CCM iliyotiwa saini na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Kapteni John Chilligati, iliisifia Timu ya Rais kwa kazi nzuri kwa maelezo kwamba ilikuwa imekusanya kiasi cha Sh 64 bilioni, ambazo ni nyingi.

  Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kilichofanyika chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete, jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali, likiwamo suala hilo.

  Sehemu ya taarifa ya CC-CCM ilisema: "Timu hiyo inaendelea kuzibana kampuni husika kurejesha fedha zilizochukuliwa kwa njia haramu. Hadi sasa timu imefanikisha kurejeshwa kwa jumla ya Sh 64 bilioni."

  Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Timu ya Rais ilikuwa ikiendelea kuwabainisha wanahisa wote wa makampuni yaliyochukua fedha hizo kwa njia za udanganyifu na hasa wahusika wakuu wa uchukuaji wa fedha hizo za EPA.

  Kwa kufanya uchunguzi katika taarifa hizi tatu, imebainika hadi sasa bado mabilioni ya EPA yamebaki kuwa suala tata.

  Maswali zaidi yanajitokeza, kubwa ikiwa taarifa kati ya hizo ipi ni sahihi na kwamba je, Mkulo aliwadanganya wafadhili, au Timu ya Rais ilidanganya umma ilipotoa taarifa yake kwa wahariri au Rais amedanganywa na timu?

  Ufisadi katika EPA ambayo ilifunguliwa wakati wa ujamaa kuziba pengo la ukosefu wa bidhaa uliotokana na ukosefu wa fedha za kigeni, ulijitokeza katika kipindi cha mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi wa kimataifa chini ya Kampuni ya Ernst&Young.

  Kabla ya Arnst&Young, tayari Kampuni ya Deloitte &Touche ilikwishaanza ukaguzi na kubaini ufisadi huo, hasa Sh40 bilioni ambazo zililipwa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture, lakini ghafla mkataba wake na BoT ukasitishwa.

  Baada ya kubainika ufisadi huo, Rais Kikwete alitengua mkataba wa aliyekuwa gavana wa Benki Kuu, marehemu Daud Ballali na kumteua gavana mpya na kuunda timu maalumu ya kuchunguza na kuhakikisha fedha zinarudishwa na watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  Hata hivyo, baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi hapo Agosti 18, akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita pamoja na mambo mengine Rais Kikwete alisema fedha zilizokusanywa zilikuwa Sh53 bilioni na kuwaongeza muda watuhumiwa ambao hawajarejesha fedha hizo hadi Oktoba 31, mwaka huu vinginevyo Novemba mosi watafikishwa mahakamani.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,183
  Trophy Points: 280
  Zitto nakubaliana na wewe hizo pesa haziko ndiyo maana wameshindwa kuweka majina ya waliorudisha pesa hizo hadharani. Watachomoa pesa toka hazina ili watuzuge, lakini tukiwadai list ya majina ufisadi wao utakuwa mgumu kuukamilisha

  Zitto: Pesa za EPA hazipo

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hadi sasa taifa halipaswi kuamini kuwa fedha zilizoibwa kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), zimerejeshwa hadi hapo itakapothibitishwa.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma, Zitto alisema kauli ya Rais Kikwete kuwa fedha za EPA zielekezwe kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, inatia shaka iwapo kweli zimerejeshwa na zitaendelea kurejeshwa.

  Alisema kauli hiyo ina makosa makubwa na inaibua mashaka kuhusu uwepo wa fedha zenyewe, kwani maeneo ambayo rais amesema fedha hizo zielekezwe, ni maeneo ambayo hayawajibiki kwa Bunge, hali inayoweka kikwazo cha kujua kama kweli wezi wa EPA wamerejesha fedha hizo.

  “Inawezekana kabisa serikali ikaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia TRA na kupata sh bilioni 133, halafu ikazielekeza kwenye Mfuko wa Pembejeo na TIB na tukaambiwa kuwa hizi ndizo fedha za EPA zilizorejeshwa, kumbe sivyo,” alisema.

  Alisema kazi ya kupanga matumizi ya fedha za umma ni ya Bunge na si ya rais na kwamba alichopaswa kufanya ni kuliomba Bunge liidhinishe matumizi ya fedha hizo kwa Waziri wa Fedha kuwasilisha muswada bungeni.

  “Alichopaswa rais kukitamka ni kuwa serikali yake inakusudia kuleta muswada wa matumizi wa fedha hizo bungeni ili kuliomba Bunge likubali kuidhinisha na si kutoa amri kuwa fedha hizo zielekezwe kwenye Mfuko wa Pembejeo na kwenye Benki ya TIB,” alisema.

  Zitto alisema, TIB haiwajibiki bungeni na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo nao hauwajibiki bungeni, bali unawajibika kwa bodi yake na Bunge halitaweza kukagua fedha hizo.

  Alisema, rais amekiuka utaratibu kwa kutoa amri ya kuzielekeza fedha hizo katika maeneo ambayo kimsingi hayawezi kujadiliwa na Bunge, hivyo taifa lina sababu ya kutilia shaka urejeshwaji wa fedha hizo hadi hapo serikali itakapokuwa wazi zaidi.

  Akizungumzia uchumi, Zitto alisema, Rais Kikwete hakupaswa kuishia kujisifu kuwa uchumi unakua, bali alipaswa kueleza ni kwa kiasi gani amefanikiwa kumfanya mwananchi wa kawaida anufaike na uchumi huo.

  “Hata Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliacha uchumi mpana, ukikua katika kasi ya kuridhisha, kwa hiyo jukumu la serikali ya Kikwete lilikuwa kuhakikisha ukuaji huo unaboresha maisha ya mwananchi, kitu ambacho hajakifanya hadi sasa licha ya kuahidi maisha bora kwa kila Mtanzania,” alisema.

  Alisema serikali imeshindwa kupata suluhisho la kuboresha kilimo nchini na ndiyo maana uchumi unakua lakini wananchi wengi ni wakulima wa vijijini na hali zao za maisha bado duni.

  Alisema ili Watanzania waweze kuwa na maisha bora, sekta ya kilimo inabidi ikue kwa asilimia nane hadi kumi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

  “Kwa umaskini tulionao, kuna haja ya serikali na wadau nchini kufanya mapitio ya kuboresha Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) ili uchangie zaidi maendeleo ya vijijini, hususan katika sekta ya kilimo na miundombinu,” alisema.

  “Kwa mfano, hivi sasa kuna mfumuko wa bei lakini mkulima wa kijijini bado analazimika kuuza mazao yake kwa bei ndogo ya kijijini, lakini mkulima huyo anaponunua bati au mbolea vinavyopatikana mjini, anakuta ni ghali sana,” alisema.

  Alisema tatizo la serikali ya Kikwete ni kuutazama uchumi katika mtazamo wa uchumi wa mjini tu ‘urban economy’ na kusahau mambo ya msingi ambayo yanaweza kuchochea uchumi wa vijijini ‘rural economy’, kama kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa wingi, kushughulikia bei na masoko ya wakulima, na ujenzi wa miundombinu ya barabara na maji vijijini.

  “Hivi sasa ni asilimia tatu tu ya wakulima nchini ndio wanapata mikopo ya kilimo, asilimia 18% ya wakulima ni wale wanaotegemea msaada wa ndugu, jamaa na marafiki wenye uwezo kuwasaidia gharama za kilimo, mathalani unakuwa na ndugu yako anaishi mjini anakununulia mbolea ndipo unalima. Kuna haja ya kuwa na mwelekeo wa kisera katika kilimo, hatuwezi kufanikiwa tukiendelea hivi. Hatuzalishi, ebu jiulize, tupo wabunge wengi, lakini ni wangapi wana mashamba?” alihoji Zitto.
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  si majina tu na mali walizokama na thamani yake. vinginevyo tunazugwa. huwezi kuonge kuhusu wezi huku unacheka na kutabasamu hovyo.
   
 18. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  PESA ZA EPA huenda zimehusika kwenye Party la juzi kwenye harusi sasa mnahojihoji nini?
   
 19. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Party si rahisi maana watu wametoka bila kula, msosi ulichelewa kishenzi kwa sisi wenye njaa mbaya tuliwahi kutoka sijui wenzetu walobaki kama walikula. Lakini tunaambiwa Lau Masha, alikwenda kupeleka zawadi akiwa na "WAFANYAKAZI WENZAKE WA IMMA ADVOCATES" sasa watu wakajiuliza, si alisema ameondoka? Yeye ni Waziri au mfanyakazi/partner wa IMMA?
   
 20. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tujukumbushe, je, kati ya hawa nani aliyefilisiwa?
  https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=2670&page=102

  http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/1/17/print.php/8011702.php
   
Loading...