Utata wa kifo cha Nyerere: Siri zaidi zafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata wa kifo cha Nyerere: Siri zaidi zafichuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Mar 22, 2012.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  * Ndugu walitaka apelekwe China, Mkapa akagoma
  * Profesa Mwakyusa alimtelekeza, Gachuma akajitosa
  * Mazingira ya kutia mashaka yaelezwa, hali inatisha


  Na Waandishi Wetu, Musoma

  Baada ya Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), kumtaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa aeleze kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kilitokana na nini, ndugu mwingine ameibuka na kuishutumu Serikali ya Mkapa kuwa ilimtesa Mwalimu Nyerere kwa kutompa matibabu ya uhakika kutoka kwa daktari wake, Profesa David Mwakyusa.

  Ndugu huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema Profesa Mwakyusa, hakupata kwenda kijijini Butiama kumtibu Mwalimu wakati akiumwa, badala yake alimtumia daktari mmoja aliyetajwa kwa jina la Malima, kumtibu Mwalimu Nyerere. Dk. Malima anatajwa kuwa mmoja wa madaktari waliopendwa mno na Mwalimu na wakazi wengi wa Butiama.

  "Mwalimu aliugua, hali ikawa mbaya, Profesa Mwakyusa hakupata kwenda Butiama kumtibu, badala yake akawa anamtumia Dk. Malima. Alikuwa akitibu kwa kutumia simu. Huyu ndiye mtu ambaye tunaweza kusema alimsaidia Mwalimu kuongeza siku za kuishi.

  "Dk. Mwakyusa alienda Butiama siku alipoambiwa hali ya Mwalimu inazidi kuwa mbaya, ndipo akapanda ndege, wakaja wakamchukua na kwenda naye Dar es Salaam.

  "Lakini wakati huo mfanyabiashara, Christopher Gachuma, alishakwenda kumjulia hali Mwalimu. Akamkuta anataabika kweli kweli. Nakumbuka nilikuwapo na Gachuma alilia machozi. Akamweleza Mwalimu, ‘naomba Mwalimu nikupeleke Nairobi ukatibiwe'. Mwalimu akakataa kata kata, akasema; "kama hawataki... hawa hawataki kunitibu niache nifie hapa hapa nyumbani kwangu". Gachuma alimbembeleza sana, lakini Mwalimu alikataa," amesema ndugu huyo.

  Ndugu huyo amesema kwamba siku chache baadaye, walimu wawili waliomfundisha Mwalimu Nyerere - Mwalimu James Irenge na Mwalimu Kirigini - walifika nyumbani kwa Mwalimu, Mwitongo kumjulia hali mwanafunzi wao (Mwalimu Nyerere).

  "Nakumbuka siku hiyo walikwenda moja kwa moja hadi chumbani. Wakakuta Mwalimu anateseka kwa maumivu makali. Walimu wale walilia machozi. Wakamwuliza Mwalimu kuhusu matibabu, akawajibu kuwa mipango inafanywa apelekwe Uingereza. Wakakataa wakisema huko ni hatari, bora apelekwe China," amesema ndugu huyo.

  Mwalimu Kirigini alifariki dunia miezi kadhaa baada ya Mwalimu Nyerere kufariki dunia.

  JAMHURI lilipowasiliana na Gachuma, alisema yeye alitoa wazo la kumpatia matibabu baada ya kukuta yupo kitandani anaumwa, na yeye kama Mjumbe wa NEC alikuwa na wajibu wa kumjulia hali kiongozi wake.

  "Nilikwenda kumuona, alikuwa anaumwa. Kimsingi nilichomwambia nikasema Mwalimu kuliko kukaa hapa nyumbani ni bora ukatafuta 'second opinion' ya madaktari, akaniambia tayari serikali imekwishamfanyia 'appointment' ya kumpeleka nje," alisema Gachuma na kuongeza:

  "Alikuwa kitandani anaumwa, ila baada ya siku moja au mbili nilipotoka pale [nyumbani kwa mwalimu] ndipo alipopelekwa nje ya nchi."

  Jamhuri ilipowasiliana na Profesa Mwakyusa aliyekuwa daktari binafsi wa Mwalimu Nyerere kwa njia ya simu jana, lakini baada ya salamu mambo yalienda hivi:

  Mwandishi: Profesa baadhi ya wanafamilia ya Mwalimu Nyerere wanasema ulimtelekeza baba yao, ulikuwa humpi matibabu inavyostahili.

  Prof. Mwakyusa: Sikusikii vizuri, naongea na nani?

  Mwandishi: Profesa naitwa Balile

  Prof. Mwakyusa: Unasemaje? Nipo kwenye gari Ruvu sikusikii.

  Baada ya kusema hivyo, Mwandishi alimtumia ujumbe (SMS) huu: "Profesa shikamoo. Naitwa Deodatus Balile, Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI. Muda mrefu nakutafuta. Tumepata taarifa kutoka familia ya Mwalimu Nyerere na wanasema wakati Mwalimu anaumwa ulimtelekeza ukawa unamtuma Dk. Malima badala ya kumtibu wewe kama daktari wake. Unasemaje? Asante."

  Ujumbe huo ulionyesha kumfikia, na mwandishi alipompigia tena simu baada ya muda akapokea simu, na hata kabla ya kuitikia akasema: "Nipo kwenye gari sikusikii vizuri… naongea na nani?" kisha akaiacha simu hewani huku zikiwapo sauti za matangazo ya mpira kuashiria alikuwa karibu na redio iliyofunguliwa sauti ya juu.

  Kwa upande wake Dk. Malima, simu yake ilipokewa na mtoto, aliyeikimbiza kwa mtu mwingine aliyezungumza kwa sauti ya kike na kusema; "Bado yuko hospitalini." Alipoulizwa angerejea nyumbani saa ngapi, mtu huyo alisema hajui. Baada ya muda siku ilizimwa.

  Mwalimu wa Mwalimu Nyerere azungumza

  Baada ya kauli ya Mbunge Nyerere kumtaka Mzee Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu, Mwalimu Irenge amejitokeza na kusema amefurahishwa mno kusikia kuwa amepatikana kiongozi jasiri wa kuhoji namna Mwalimu alivyougua hadi kufariki dunia.

  "Mfikishieni pongezi nyingi Mbunge Nyerere... huyo mtoto amefanya jambo la maana sana kuuliza jambo hili, miaka yote nalia kwa sababu naamini Mwalimu aliuawa.

  "Kwa kuwa suala hili limeulizwa hadharani, sasa nipo radhi kufa. Nikifa nitakwenda moyo wangu ukiwa na furaha kwa sababu nimekuwa nikijiuliza ni nani anayeweza kuhoji namna Mwalimu… mwanafunzi wangu alivyokufa," amesema Mwalimu Irenge mwenye umri wa miaka zaidi ya 120.

  Mwalimu Irenge alianza kumfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge kuanzia mwaka 1934 hadi 1936. Alistaafu kazi mwaka 1977. Tangu wakati huo anaishi jirani na shule hiyo. Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Mwalimu Irenge alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema binafsi hakuafiki Mwalimu kupelekwa kutibiwa nchini Uingereza.

  Alisema alipinga kwa sababu alijua Waingereza si marafiki wa kweli wa Mwalimu kwa kuwa aliongoza harakati za kuwang'oa katika Tanganyika na katika mataifa mengine, hasa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikiunga mkono utawala wa kidhalimu wa Wazungu wachache.

  Vincent Nyerere amkomalia Mkapa

  Mbunge wa Musoma Mjini, Nyerere (Chadema), ametetea uamuzi wake wa kumtaka Rais (mstaafu) Mkapa aeleze mazingira ya kifo cha Mwalimu Nyerere, akisema ni Watanzania wengi ambao wamekuwa wakitaka kupata majibu hayo.

  Katika mahojiano maalumu na JAMHURI yaliyofanyika Arumeru mkoani Arusha, Nyerere amesema Watanzania wanachotaka ni majibu ya swali alilomwuliza Mkapa.

  "Hapa hakuna ugomvi kama baadhi ya watu wanavyodhani, nilichofanya ni kuuliza swali, sasa ni wajibu wa Mkapa na wanaohusika kutoa majibu, tena majibu yanayojitosheleza. Kama Mzee Mkapa amekuwa akidanganya kwa miaka mingi, ajue sasa wananchi wanataka majibu, na mimi nimeanza kuingiwa na shaka juu ya uadilifu na ukweli wa Mzee Mkapa.

  "Kwenye msiba wa baba yangu Josephat Kiboko Nyerere, ndiye aliyenikabidhi ubani, sasa anaposema hanijui, hii inanipa shaka juu ya ukweli wa yale ambayo mara zote ameyasimamia," amesema Nyerere.

  Amekiri kuwa kaka yake, Joseph Butiku amempigia simu na kumtaka ‘amwache' Mzee Mkapa.

  "Butiku ni kaka yangu, amenipigia simu, lakini nashukuru kwamba ametambua kuwa nilichofanya kwanza ni kujibu uongo uliotolewa jukwaani, kwamba mimi sina uhusiano na familia ya Baba wa Taifa. Mimi Mwalimu ni baba yangu mkubwa… huo ndiyo ukweli hata kama Mkapa anataka au hataki.

  "Butiku akaniambia kuwa kama nilichokozwa nilikuwa na haki ya kujitetea. Kwa kweli nilichofanya ni kujitetea maana kama Watanzania wangeamini uongo kuwa mimi si wa familia ya Nyerere, hiyo ingeniathiri maana wananchi wasingeniamini. Lakini sasa ukweli umejulikana.

  "Uchunguzi wangu umebaini kuwa Mkapa alidanganywa na viongozi wa CCM. Yupo kiongozi alimwambia kuwa Nyerere ni mwiba jukwaani kwa hiyo atafute namna ya kumzima, hasa kwa kuwa anatumia jina la ‘Nyerere'.

  "Mzee Mkapa naye bila kujua akaingia kichwa kichwa, baadaye nasikia anasema huo ulikuwa utani. Jukwaani hakuna utani, sisi Chadema hatuna utani, kama wao (CCM) wanafanya utani, sisi hatujui utani," amesema.

  Tendwa naye apigwa kombora

  Nyerere alimgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na kumtaka asiingilie masuala ya ukoo, badala yake aendelee na masuala ya vyama.

  "Tendwa kasema eti kumzungumzia Baba wa Taifa ni kuhatarisha amani katika taifa. Lakini anajua kuwa mimi nilishambuliwa kwa hiyo nilikuwa na kila sababu ya kujitetea. Yeye ni Msajili wa Vyama vya Siasa, si msajili wa ukoo.

  "Kwangu mimi kumzungumzia Mwalimu ni haki kwa sababu zaidi ya kuwa Baba wa Taifa, ni mlezi wangu. Nimesomeshwa kwa kutumia fedha za akaunti maalumu ya Mwalimu katika benki ya NBC. Akitaka kujua aende apitie rekodi za fedha zilivyokuwa zinatolewa ili nilipiwe ada. Hana mamlaka ya kunizuia kumtaja baba yangu mkubwa. Sasa hivi kuna sala maalumu, kwa hiyo anataka hata nisisali hiyo sala ya kumwombea Mwalimu?" Amehoji.

  Kwa siku kadhaa sasa, Nyerere ameibua mjadala mkali ndani na nje ya nchi kwa uamuzi wake wa kumtaka Mkapa aeleze ukweli wa kifo cha Mwalimu Nyerere.

  Alisema Mkapa hawezi kutamba kuwa ni miongoni mwa watu wanaomuenzi Mwalimu, kwa vile baada ya kushika madaraka alihakikisha anauza viwanda na mashirika yote ya umma, vitu vilivyoasisiwa na Mwalimu.

  Alitoa mfano wa Benki ya NBC iliyokuwa ya umma ambayo Mkapa aliiuza kwa bei ya kutupa kwa makaburu wa Afrika Kusini. Mwalimu aliongoza harakati za kuzuia kuuzwa kwa benki hiyo, na hadi anafariki dunia alikuwa ‘haelewani' na Mkapa juu kuuzwa kwa benki hiyo.

  Mashirika ya umma zaidi ya 400 yaliyoachwa na Mwalimu yaliuzwa chini ya uongozi wa Mkapa wa miaka 10.


   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  PHP:
  Alisema Mkapa hawezi kutamba kuwa ni  miongoni mwa watu wanaomuenzi Mwalimukwa vile baada ya kushika  madaraka alihakikisha anauza viwanda na mashirika yote ya ummavitu  vilivyoasisiwa na Mwalimu.
  Haya sasa!
  Auaye kwa upanga atakufa kwa upanga.

   
 3. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ...nini ni Lengo la hii tamthiliya ya Nyerere inayotaka kuanza saiv...?
   
 4. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  tumechoka na habari hizi, sasa walikuwa wapi kusema hayo enzi hizo wanasema leo wakati Nyerere amefariki, inasaidia nini sasa??? Nyerere ndo atafufuka??/

  bongo bana watu wanajitafutia umaarufu kwa vitu vya ajabu ajabu sana?? wangetoa taarifa hizo mapema not now?
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni miaka mingi imepita tangu Mwalimu alipofariki bila hoja za namna hii kuibuka. Iweje kampeni za Jimbo la Arumeru mashariki ndiyo iwe chanzo? Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani....amina.
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Mwalimu alikuwa na maumivu makali sana kwa sababu alikuwa na Saratani ya Damu tangu kabla ya mwaka 1989. Kama kifo chake kinatokana na kutopelekwa kwa wakati kwenda kutibiwa hilo ndilo la kujadiliana kwani Mwaka 1989 alipelekwe Uingereza na kufanyiwa Operesheni kuondoa sehemu iliyoshambuliwa na Kansa.
   
 7. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  haya masuala yanachanganya sana ...ngoja nitafute kakonyagi kadogo nizimue ili niweze kufikiri,,,nitarudi baadae
   
 8. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ...nyie glet thnnkaz nini lengo na madhumuni ya huu uzi?
   
 9. papason

  papason JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wamagamba si nyie wenyewe ndio mlioanzisha vita ya mawe wakati mnaishi kwenye majumba ya vioo, subirini 'tuwanyoe na kuwakarabati' vilivyo .............jino kwa meno!!!1
   
 10. Fund

  Fund Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuzote lifanyikalo gizani !hounyeshwa hadharani tu,nazidi kuingalia hiyo muvi.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Vyama vya siasa vikizingatia misingi na maana sahihi ya kampeni haya yote hayatajitokeza...hebu elezeni sera za vyama vyenu na si kushambuliana...wapiga kura hatuwaelewi na hatuhitaji kujua mambo yenu binafsi.
   
 12. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mbona kasheshe - Mzee Mkapa ana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa moyo kuhusiana na hili jambo, whatever the truth
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Tabia ya Mkapa ya kuropoka na kudharau watu inamtokea puani, sasa movie ndiyo inaanza.Hii ngoma huyu mkimbizi hatoki.
   
 14. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Safi saana kama kweli bmw alimfanyizia huyo mzee maana alikuwa haishi kumtusi mwinyi na alimkataa jmk kwa makusudi ili bmw awe rais yakamkuta mdini saana huyo marehemu jkn
   
 15. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  CCM(chama cha mauaji)
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hakika safari hii mpaka mwaka 2015 tutaona na hata kusikia mengi.
   
 17. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kweli hii ndo bongo. Tumekuwa tukiambiwa hapa kuwa mwalimu alienda Uingereza akiwa mzima wa afya na kurudi marehemu. Leo tunaambiwa alikuwa taabani kabla hata hajaondoka. Aisee!
   
 18. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hebu twambie kwa undani kuna tatizo gani hizi habari kuletwa sasa? Je zingekuwa zimeletwa mapema zingesaidia nini kama unaona zilizotoka sasa hivi hazisaidii kitu?

  Tiba
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Ni kuendelea kufichua yaliyokuwa yamejificha.
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  The movie continues ukisikia kifo cha CCM kinakaribia ndio sasa. Wacha tujiangalie hii movie itamalizikia wapi!!!!Inatisha.
   
Loading...