Utata wa kifo cha Dkt. Omary Ali Juma

Unapoambiwa karma ufanya revenge kwa mda wake na kamwe aliepukiki unatakiwa ukubali . Ni huyo huyo General Imran Kombe Spy Chief by then ndie alieandaa mazingira kama si njia ya kumuondoa yule mmasai kipenzi cha watu.

Malipo yote ni hapa hapa duniani huko ahera ni mengine.
Ivi mmasai anaondoka DG alikuwa ni kombe eh?
 
Haha mmakua hakuwataka boys2men!! Alimpa dossier Kali kinana na Mangula wawashughulikie!! Kilichotokea ni historia!! Mzee akasalimu amri katikati ya pambano!!!
Hasa baada ya mjumbe wa Kenya kukumbusha kuwa KANU ni chama cha upinzani kwahiyo wasifanye makosa kama ya kwao,
Mwenye nguvu mpe,pale ilikuwa aukwae Prof.Mwandosya.
 
kagame anaingiaje tena hapa?

cc Jestkilla a.k.a Jestina Hikizimana
Luteni Jenerali Mstaafu Imran Kombe akiwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa aliwaonya Marais wa Rwand na Burundi kutopanda ndege moja kuelekea Rwanda kwakuwa alishapata fununu juu ya njama za kutaka kumuua Rais wa Rwanda wa kipindi hiko.

Na kikundi kilichowaua Marais hao kikiongozwa na PK kilifahamika vema na Kombe.
 
Luteni Jenerali Mstaafu Imran Kombe akiwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa aliwaonya Marais wa Rwand na Burundi kutopanda ndege moja kuelekea Rwanda kwakuwa alishapata fununu juu ya njama za kutaka kumuua Rais wa Rwanda wa kipindi hiko.Na kikundi kilichowaua Marais hao kikiongozwa na PK kilifahamika vema na Kombe.


duh kumbe
 
Anaitwa Imran Kombe, alipigwa Risasi 14 kifuani na Askari wa Jeshi la Polisi kwa Madai ya kufafanisha gari aliyokuwemo na iliyoibiwa!
Sina Immunity ya kutoshughulikiwa ndio sababu sitofunguka zaid Mkuu
Aisee
 
Jenerali kombe alikuwa ni mwanajeshi na kiongozi jushaa [hodari] wa nchi yetu na hasa alijulikana pale nchi yetu ilipoingia katika mapambano ya kurudisha ardhi yetu iliyochukuliwa na dikteta IDD AMIN DADA, kwani yeye ni moja wa makanda waliopambana mstari wa mbele katika vita ya kagera.

Unaweza kujiuliza kuhusu hiyo nick name aliyokuwa anafahamika nayo katika medani za kivita, alipewa hilo jina katika vita ya kagera kutokana na yeye kukusanya vikosi vyake na kuingia Uganda kwa kuvuka mto mkorofi ambao huu mto pia unajulikana kwa jina la mto mkorofi wa ngono[sababu kuu ya huu mto kuitwa hivi ni kuwa inaaminika mtu wa kwanza kuwa na virusi vya ukimwi duniani aliishi kando ya huu mto na inajulikana ulimwenguni kote kuwa njia kuu ya kuambukizwa ukimwi ni kufanya ngono]. Baada ya kuisha kwa ile vita jenerali kombe alipandishwa cheo na kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi [CHIEF OF STAFF] ambacho alikitumikia kwa muda Fulani, na ilipofika kipindi cha utawala wa DR. ALI HASSAN MWINYI jenerali kombe aliteuliwa na kuwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa.

Katikati ya mwezi wa june mwaka 1996 jenerali kombe alivuliwa wadhifa aliokuwa nINAENDELEAenzi wa usalama wa taifa] na hii ilikuwa ni kipindi cha mwanzo kabisa cha utawala wa mheshimiwa BENJAMNI WILLIAM MKAPA kwani huyu raisi aliingia madarakani mwaka 1995. Kwahiyo baada ya kuvuliwa wadhifa wake akabaki kuwa mstaafu lakini kwa mujibu wa sheria alikuwa anapewa ulinzi na mahitaji mengine kama wastaafu wengine wa nyadhifa za juu serikalini na jeshini.

MAUAJI YA JENERALI KOMBE
Mwaka 1996 gari aina ya NISSAN PATROL iliibiwa jijini DAR ES SALAAM na mwizi maarufu wa magari wa kipindi hicho aliyekuwa akijulikana sana kwa jina moja la WHITE [nimekosa jina lake halisi kwani hakuna chanzo kilichotaja au kujua jina lake halisi], gari hilo lilikuwa limesajiliwa na namba za usajili [TZD 8592] na lilikuwa mali ya mfanyabiashara W. LADWA.

Baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za uwizi huo walianza kufanya uchunguzi kujua na kubaini ni yuleyule mwizi sugu wa magari maarufu kwa jina la WHITE. ndipo hapo mkuu wa jeshi la polisi kanda maalumu ya DAR ES SALAAM aliamuru askari wawili kwa majina ya koplo JUMA MSWA na konstebo MATABA MATIKU wakiwa na silaha aina ya PISTOL CHINESE-TYPE kwenda katika mkoani KILIMANJARO, MOSHI.

Kamanda wa DAR ES SALAAM aliamuru hivyo waende moshi kwasababu walipata taarifa kuwa jambazi WHITE yuko kati ya ARUSHA na MOSHI, wale askari wawili walivyofika moshi walipokelewa na kamanda wa Kilimanjaro huku nyuma tayari kamanda wa DAR alikuwa ameshawasiliana na kamanda wa KILIMANJARO kuwa kuna vijana wangu nimewatuma kazi huko ya kutafuta gari lilioibiwa DAR.

Kamanda wa moshi alitoa askari wake watatu na kuungana na wale wawili wa kutoka DAR, hawa askari watatu wa MOSHI walikuwa na bunduki aina ya MACHINE GUN na wakaanza msako mara moja wa kutafuta wapi gari lilipo pamoja na jambazi WHITE na ikumbukwe kipindi hicho gari aina ya NISSAN PATROL ilikuwa ni gari ya kifahari sana na zilikuwa chache sana.

Mnamo tarehe 30 juni 1996 wale askari watano wakiwa katika gari yao ya polisi katika randa randa zao za kutafuta gari iliyoibiwa, gafla waliona gari aina ya Nissan patrol amabayo ilikuwa ikifanana na ile iliyoibiwa DAR hapohapo wakaanza kuifukuzia kwa nyuma huku wakiipiga risasi, takribani risasi kumi na nne zilipigwa kwenye ile Nissan waliokuwa wanaifukuzia wale askari.

Katika zile risasi zilizopigwa kuna risasi zililenga tairi na hivyo kupelekea gari la jenerali kombe kuanza kuserereka na mwishoe likaegemea mahali na kusimama, kwa bahati mbaya sana siku hiyo jenerali kombe hakutembea na walinzi wala dereva wake, yani alikuwa yeye na mke wake ROSSELEEN tu. Na ndo maana jenerali alihofia kusimamisha gari kwani alihisi labda wale majambazi wanataka lumuibia au wametumwa kumuua na ikumbukwe huyu alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa kwahiyo watu kama hawa mara nyingi ni MOST WANTED.

Huku nyuma askari wale wakaona gari limesimama na hatimaye tu walivyofika wakashuka haraka huku wote wakiwa wameshika bunduki zao [nimeshaelezea kila mtu alikuwa na aina gani ya silaha], wakati askari wanakaribia kuwafikia jenerali kombe na mkewe huku nyuma tayari jenerali alikuwa ameshatoka ndani ya gari yake.
Alipokuwa ametoka ndani ya gari alikuwa karibu kabisa na gari yake huku akitahamaki haelewi ni nini kinaendelea.

Wakati jenerali anatahamaki wale askari wakawa wameshafika eneo la tukio huku nyuma mke wa jenerali naye alikuwa ameshuka upande wa pili wa mlango wa mbele, wale askari walipomkaribia tu jenerali wakamyooshea bunduki huku wakijatambulisha sisi ni askari na kati yao kulikuwa na wngine wamevaa sare, jenerali kombe kutokana na kuwa na uzoefu na mambo ya kiusalama hakutaka kuonesha makuu kuwa yeye alikuwa ni nani katika usalama wa nchi na jeshini…

Kwa haraka kabisa jenerali kombe aliinua mikono juu kuonesha wale askari kuwa ametii agizo ingawa bado alikuwa anatahamaki ni vipi tena naoneshewa bunduku na vijana[askari] ambao walikuwa chini yangu juzi tu hapa kabla sijastaafishwa, cha kushangaza wale askari wawili kutoka DAR wakamiminia jenerali kombe risasi nne kifuani mwake bila kuwa na huruma wala kujali kuwa jenerali amesalimu amri kwa kunyoosha mikono juu.

Jenerali kombe alijeruhiwa vibaya sana na zile risasi zilizompata kifuani na hatimaye akapoteza maisha papo hapo, mkewe alizunguka mbele ya gari na kwenda pale chini alipoanguka mumewe na kuanza kumshika huku akilia sana kwa uchungu na kusema “mnajua nani mliyemuua….?” Wale askari hawakutaka kusikiliza chochote, wao walichofanya ni kuwachukua wote na kwenda kuwapeleka sehemu husika ambapo mumewe alipelekwa hospitalini na mkewe alipelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano.

Kule kituoni mke wa jenerali alitoa maelezo kuwa yeye ni nani na aliyeuwawa ni nani, baada ya maelezo hayo kamanda wa polisi Kilimanjaro akapewa taarifa kuwa Yule aliyepigwa risasi alikuwa ni jenerali kombe ndipo yeye akawasiliana na kamanda wa Dar na kumjulisha kilichojiri naye kamanda wa Dar akaongea na mkubwa wake ambaye ni mkuu wa mapolisi Tanzania[IGP]. Baada ya maelezo yake, mke wa jenerali kombe akaachiwa na kwenda hospitalini aliko mumewe na vyombo vya habari huku nyuma vya Tanzania na vya nje ya nchi vikaanza kuripoti tukio lililotokea na nchi nzima ilipatwa na simanzi kutokana na msiba huu mkubwa.
 
...Juzi ex CIA agent, aliyekuwa anakaribia kukata roho ali confess kwamba Bob Marley aliuwawa (huo uzi umo humu), kamuulize huyo mwl wako anasemaje kuhusu hili?
Namkumbuka huyo jamaa,alimpa zawadi ya VIATU Bob Marley ambavyo vimepishana namba,kile kidogo ndicho alichoweka waya uliokuwa planted CANCER,halafu akavibeba kwa madai ya kuvirudisha shop sababu ikiwa ni kukosea packing.

Na alirudi tena kumuona Bob kama ameshaanza kudhohofu na akamkuta ameisha moaka DREADLOCKS amezikata.

Huku akidai ameshaua wengi bila kujutia isipokuwa kwa Bob marley tu.
1999 tulimpoteza Mzee Mchonga, aliondoka kwenda London akiwa salama salmini alirudi akiwa kwenye coffin box
 
Unapoambiwa karma ufanya revenge kwa mda wake na kamwe aliepukiki unatakiwa ukubali . Ni huyo huyo General Imran Kombe Spy Chief by then ndie alieandaa mazingira kama si njia ya kumuondoa yule mmasai kipenzi cha watu.

Malipo yote ni hapa hapa duniani huko ahera ni mengine.
Horace Kolimba anajua kila kitu maana alikuwa ndio mkuu wa msafara mchana ule Mmasai anapata ajali pale Dumila.

Bahati mbaya Kolimba amekufa na siri yake moyoni pale Kizota.
 
CIA walisema aliehusika na kifo cha Kombe ni PK na walitoa repoti yao.
There is also reason to believe that a number of people with knowledge of Kagame's plot against the presidential aircraft have been assassinated.

These possibly include Tanzania's former intelligence chief, Major General Imran Kombe, shot dead by policemen in northeastern Tanzania after he was mistaken for a notorious car thief. His wife maintains he was assassinated.

Kombe had knowledge of not only the planned assassination of the Rwandan and Burundian presidents but a plot against Kenya's President Moi and Zaire's President Mobutu, as well. There is a belief that Roman Catholic Archbishop of Bukavu, Emmanuel Kataliko, was assassinated last October in Rome by members of a Rwandan hit team acting on orders from Kagame. Other Tutsi and Hutu leaders who oppose Kagame's regime continue to flee Rwanda to the U.S. and France in fear of their lives.

Rwanda's figurehead Hutu President Pasteur Bizimungu was forced to resign last year under pressure from the only power in Rwanda, his then-Vice President, Paul Kagame. Deus Kagiraneza, a former intelligence officer in Kagame's Military Intelligence Directorate (DMI), interim Prefect of the Ruhengeri province, and member of the Parliament, is now in exile in Belgium.

He charges that Kagame's top government and military are responsible for torturing and executing their political opponents. Kagiraneza maintains that the RPF has pursued such policies since the time of the 1990 invasion of Rwanda from Uganda
Blood Money Out Of Africa
 
Laurent Kabila aliendesha Mapambano ya kumtoa Mobutu akitokea Mikocheni

Rajab Hussein na Pierre Nkurunzinza walikuwa wakiendesha Mapambano ya kuwatoa kina Pierre Buyoya kutokea Buguruni kwa Mzee wa Kibwali Mzee Mnenge

Yoweri Kaguta Museven kaongoza Vurugu Uganda akiwa Dar
Edward Mondlane kaongoza Vurugu za Msumbiji akitokea Dar

Paul Kagame kaongoza Vurugu Rwanda akitokea Uganda

Hata Prof Wamba alikuwa akiongoza Vita akiwa Dar!
Mkuu huyo Mzee mnenge si ni wakwetu kigoma?
 
Ni Vizuri kuwa Makini Kijana!

Kama Mkuu wa Usalama wa Taifa anaweza kutegewa akategeka bila ya kujua, Mimi na Wewe nani anaweza kuwa Mtaalam wa kuruka mitego hiyo?

Kunguru muoga huishi Miaka mingi japo ndio huonekana Fala kwa Makunguru wenzie
Hapa unazungumzia nini? sijaelewa ,sijawahi sikia kwenye historia ya Tanzania bosi wa intelligence kawekewa sumu, Kombe haikuwa hivyo!
 
Back
Top Bottom