Utata wa kauli ya Kagasheki kuhusu vifo vya wanafunzi wa Shauritanga

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,664
Daily News said:
The Deputy Minister for Home Affairs said all WAZAZI secondary schools, including Shauritanga, would be possessed by the government. On the number of deaths at the school, Ambassador Kagasheki said a total of 40 people, including 37 students, four of them died in hospital later and two unidentified people were buried.

He said since then, nobody had ever reported that a relative or a student from the school was still missing after the inferno 15 years ago. He advised that anyone wishing to see the Scotland Yard report regarding the Shauritanga inferno was free to contact the Ministry of Home Affairs. He said police regulations do not allow such reports to be made public.


wana jamiiforums,

..naibu waziri wa mambo ya ndani anadai kulikuwa na marehemu wawili ambao hawajatambuliwa.

..pia anadai hakuna mwananchi/mzazi aliyedai kupotelewa na ndugu/mtoto.

..nashangaa kwanini serikali imeshindwa kuwatambua hao marehemu wawili. kwa mfano kwanini hakuna taarifa za jinsia wala umri wa marehemu hao ambao hawajatambuliwa.

..pia naamini kabisa Scotland Yard wana uwezo wa kutumia Teknolojia kuweza kupata mfano wa sura za hao marehemu ambao hawajatambuliwa.

..Teknolojia ya Computer ndiyo iliyotumiwa na Milwaukee School of Engineering kuweza kutambua maiti ya msichana wa kitanzania aliyeuawa na mjomba wake.

..pia nashindwa kuelewa kwanini serikali inaficha ripoti na matokeo ya uchunguzi wa janga[vifo vya watoto 40] kubwa kama hili.

NB:

..wananchi wa Shauritanga na wilaya ya Rombo wanastahili pole zetu za dhati.

..pia lazima niwapongeze kwamba pamoja na janga hilo bado wameendeleza juhudi zao ktk elimu kwa kuwa shule 2 za sekondari kila kata.
 
Nitalisema hili hapa maana wengine wanajaribu kupaka mafuta unafiki wa serikali yetu. Hii kwa sasa inajulikana kwa mifereji ya inteligence gatherings za Tanzania kuwa shule ya shauritanga ilichomwa moto na magaidi wenye misimamo mikali ya kidini.

Ni dini gani hiyo ---- nitakutajia muda si mrefu.
 
Mwafrika,

..ninavyoelewa mimi Shauritanga ni shule ya Jumuiya ya Wazazi.

..sasa sioni sababu ya magaida wa dini yoyote ile unayoifahamu wewe kushambulia shule ile.

..serikali itoe ripoti ya uchunguzi, na zaidi watambue marehemu wote waliopatikana eneo la ajali.
 
Nitalisema hili hapa maana wengine wanajaribu kupaka mafuta unafiki wa serikali yetu. Hii kwa sasa inajulikana kwa mifereji ya inteligence gatherings za Tanzania kuwa shule ya shauritanga ilichomwa moto na magaidi wenye misimamo mikali ya kidini.

Ni dini gani hiyo ---- nitakutajia muda si mrefu.

usiwe mwongo,ile shule ni ya wazazi na wanafunzi waliokuwa wanasoma ni wa dini zote,yupo dada mmoja nilikaa nae mtaa mmoja kijitonyama alisoma pale na wakati hilo sakata linatokea yeye alikuwa yupo dar kwa ruhusa ya kuumwa.acha uzushi
 
usiwe mwongo,ile shule ni ya wazazi na wanafunzi waliokuwa wanasoma ni wa dini zote,yupo dada mmoja nilikaa nae mtaa mmoja kijitonyama alisoma pale na wakati hilo sakata linatokea yeye alikuwa yupo dar kwa ruhusa ya kuumwa.acha uzushi

Hii sio pointi. Kuna mifano mingi tu ya Magaidi kuwauwa waislamu wenzao. Bin Laden aliua wasilamu pale twin tower, Al-Zaqawi aliua waislamu wenzake kule Iraq, Abu sayaf siku zote wanasema kuwauwa wasilamu wenzao ni collateral demage. Hakuna lolote la kusumbua kwamba tukio lilikuwa limepangwa na magaidi, suala hili limewekwa kwenye jalada bila kushughulikiwa kwa maslahi ya nchi. Sio kama wakristo na waislamu wanajua kabisa kilichotokea na wote hawapendi kitendo hicho.
 
Natamani sana kujua kilichotokea hasa kwenye hii shule.Hivi hakuna aliyewahi kusoma shule ile miaka hiyo na akaandika walau simulizi lihusulo tukio hili?

Watu wapaswa kujua
 
Daaaah, hivi vifo vya watoto wa St Lucky Vincent vilivyotokea leo kwa ajali ya gari Wilayani Karatu vimenipa simanzi kubwa mno na kunifanya nikumbuke ajali ya watoto wale wa Shauritanga walioteketea kwa moto, pamoja na wale Isimani Iringa!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom