Utata wa dini kongwe na jinai mbaya ya utumwa. Je, Mungu ameonyesha ishara zake kupitia Uislam?

Naamini mungu yupo lakin hivyo vitabu vya dini naona kama kilicho andikwa ni uongo mtupu
 
Ni wewe ndiye uliyeshindwa kufahamu kuwa Mungu anauwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, lakini kwa akili yako vipi utayajua mazuri ikiwa huyajui mabaya?
Sasa kwa taarifa yako hapa duniani ni sehemu ya kuyajua mazuri na mabaya ili upate kujichagulia makazi yako ya milele ni yapi, ukitaka ulimwengu wa yasiyokuwa mabaya utaupata (pepo) au ukijichagulia ulimwengu wenye mabaya utaupata (moto) hivyo usije ukajilaumu.
Ukitaka kulithamini jema lazima baya likufike.
Huwezi kuithamini afya ikiwa haujaugua.
Hujajibu swali dogo tu.

Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?
 
Uwepo wako tu unathibitisha kuwa kuna mahali ulikotoka na yupo aliyekutengeneza.
Kwanza kabisa, hujaelezea uwepo wangu unathibitisha hayo unayosema kivipi. Huo ni uzembe wa akili.

Hujajenga hoja,umebweteza maelezo.

Pili, hata kama uwepo wangu unathibitisha kuwa kuna mahali nilikotoka na yupo aliyenitengeneza, hilo halithibitishi kwamba kuna Mungu. Inawezekana kuna Klingons waliotoka Betelgeuse ndio walionitengeneza na si Mungu.

Tatu, kama kila kilichopo kina mahali kilipotoka na yupo aliyekitengeneza, basi hata huyo unayesema Mungu naye ana alipotoka na kuna aliyemtengeneza. Kwa hivyo, kamakuna aliyemtengeneza, hawezi kuwa Mungu.

Jitihada zako za kuonesha Mungu yupo,zinatupa ushahidi zaidi kwamba hayupo.
 
Soma hapo kwenye Biblia Matayo 12:22-32. Yesu na Beelizebuli. Yesu alimponya mtu bubu aliye kuwa na pepo. Cha msingi ni kuwa mapepo ni wafuasi wa shetani, sawa. Hakuna shetani atayeweza kumdhuru shetani mwenzie. Ndio maana mapepo/ majini ya kimsumbua mtu kwa wezetu nyie huyatafutia zawadi, kama dhahabu, ubani/udi wa Makka, kuchinjia kuku, njiwa, mbuzi nk kuyapa damu za makafara. Hii mistari niliyo kupa Bwana Yesu kaelezea vizuri pale mafarisayo walipo fikiria kuwaYesu Kristo alilifukuza pepo la ububu kwa kutumia nguvu za Mfalme wa mapepo, beelizebule. Miujiza isikusumbue hata shetani yuko na nguvu za miujiza. Kumbuka ile ya mfuasi wa shetani, farao mfalme wa Misri.

Baada ya Mungu kumleta mwanae npendwa wake Yesu Kristo kuja duniani ili afe kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu/mwanadamu kutoka dhambi iliyo sababisha adhabu ya kifo, shetani hakukaa kimya naye akaja na replica yake kuujibu huu mpango wa Mungu. Ndiposa unasikia Mungu hazai, hafanishwi, hana mtoto, Yesu si Mungu. Hakufa, hakufufuka, hakutundikwa msalabani, ama alitundikwa mtu mwengine sio Yesu,nk. Hii yote ni ulaghai tu washetani ili mwanadamu asiijue kweli na apate wakuungana naye motoni. Na kawapata wengi mmoja wapo ni huyu mleta huu uzi hapa. Kweli kesha ijua ila kutoka katika mnyororo alotiwa shingoni na shetani anaona taabu inabidi aanzishe maada pengine atapindisha ukweli, haaiwezeka na mbaya zaidi Issa SAW sio Bwana Yesu. Ni vitu viwili tofauti ingawa shetani alishaingiza ulaghai wake na watu wameaminishwa eti wawili hawa ni wamoja, sio kweli.
 
Hebu fafanua mabaya na mazuri ni yapi kwa ufahamu wako?
Vifo vinavyotenganisha wapendanao ni kitu kibaya.

Magonjwa ni kitu kibaya.

Uonevu ni kitu kibaya.

Majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi ni kitu kibaya.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna na hauwezikuwa na mabaya yote haya?
 
Watoto kuzaliwa na ulemavu ni kitu kibaya pia.
 
Sasa Mungu gani anaupendeleo, watu wengine wanazaliwa na ulemavu, wengine wanapeta?

Wakatiangeweza kufanya hakuna anayezaliwa na ulemavu.
Mungu ana ubinadamu maana binadamu siye mkamilifu anaweza akawa na upendeleo, lakini mungu wanaye dai mkamilifu hawezi kuwa hvyo kwa kuwa hayupo.
 
Vifo vinavyotenganisha wapendanao ni kitu kibaya.

Magonjwa ni kitu kibaya.

Uonevu ni kitu kibaya.

Majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi ni kitu kibaya.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna na hauwezikuwa na mabaya yote haya?
Hayo yote uliyoyataja ni matokeo ya kazi za wanadamu isipokuwa kifo na hata sababu ya kufa ni inatokana na sisi wenyewe, ulimwengu ulipoumbwa ulikuwa ni sehemu nzuri ya kuishi, binadamu wa kale walikuwa wakiishi kwa muda mrefu na afya zao zilikuwa ni imara, tatizo sisi tunaojiita GT ndiyo tuliyoharibu mazingira yetu kwa mikono yetu, kwanza utumiaji mbaya wa moto umeweza kuathiri uchafuzi wa mazingira, kwa kuwa tunapounguza baadhi ya vitu hatujui vinatengeneza sumu ya aina gani ambayo inatuathiri kiafya, na binadamu amefanya mambo mengi ambayo mengine yametusaidia na mengine yanatuangamiza, bila shaka tunafahamu jinsi gani viwanda vinachangia katika kuharibu mazingira, sumu zinazomwagwa baharini, madawa yanayotumiwa katika vyakula, ajali za barabarani au angani au majini, hivi vyote ni kazi za binadamu leo tunamsingizia Mungu kwanini?
Matetemeko ya ardhi yanatokea kwa sababu maalum, wataalamu wanasema tetemeko la ardhi alinatokea kwa sababu kuna tabaka la miamba chini ya ardhi inavunjika katika kingo zake zenye hitilafu, hivi jinsi tunavyopigana mabomu au kuchimba mafuta na gesi, uchimbaji wa dhahabu, hivi kweli hizo tabaka zitakuwa salama? Tusiwe great thinkers lakini bado tu hatujaona sisi wanadamu ndiyo wenye kusababisha matatizo yote haya halafu tunasema Mungu kashindwa kuumba ulimwengu bila ya mabaya?
Dunia ni sehemu ya mtihani kwa wanadamu ndiyo maana tunazaliwa na kufa, ukifaulu hapa duniani basi maisha ya baadaye ndiyo utakayofaidi na kama ukifeli basi hayo maisha ya milele utakuwa mwenye hasara.
Hebu kaa chini halafu jiulize kwanini mimi nimeumbwa? Na kwanini mimi ni binadamu na si mbu au inzi au mende? Hii akili ninayoitumia kufikiri ni uhodari wangu au nilizaliwa nikiwa najua kila kitu na nitajua kila kitu mpaka naaga dunia?
Naomba tutafute maarifa yenye manufaa, tujadili jinsi gani tutaweza kuleta amani kwenye nafsi zetu na kwenye majumba yetu hatimaye imani hiyo ijae ulimwenguni kote. Upendo wa kweli ni ule upendo wa kumpenda mwenzako jinsi unavyojipenda wewe, na kwa kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho basi na mapenzi yana mwanzo na mwisho, na ubora wa mwisho ni mwisho mwema.
Najua ndugu yangu Kiranga umefikia kufikiri fikra hizo kwa sababu, na hizo sababu ni wewe mwenyewe ndiye mwenye kuzijua, kwa kuwa sisi binadamu ni dhaifu na tunapitia changamoto mbalimbali katika maisha, sasa changamoto hizo zisikufanye utoke nje ya mstari wa kwamba wewe umeumbwa na kuna aliyekuumba, utakuwa hujajitendea haki, usione sasa hivi unaweza kuandika hayo unayoyataka lakini ukiondokewa na neema ya kuona (Mungu akuepushiye mbali) basi ni mtihani mkubwa huo sijui itakuwaje?
 
Asante Vumilika.
Ni kama leo, kila ukinunua bidhaa ina mannual ya mtengenezaji, ikieleza jinsi ya kuitumia na jinsi ya kutoitumia inavyopasika.
Mfano katika chombo kiitwacho Gari,
Kuna sehemu ya kutia mafuta ya aina flani, ama petroli au diseli, au oili, hapo ukitia maji gari inaharibika mara moja, uharibifu huo sio wa mtengenezaji bali umesababishwa na mtumiaji.
Hali kadharika Dunia na Miili yetu tunayoitumia.
Binadamu alikabidhiwa mwili wenye afya bora kabisa na akapewa mannual yake, ale hiki na asile kile, afanye hivi na asifanye vile ili kuutunza inavyopasika.
Dunia pia alikabidbiwa ikiwa njema kabisa na kuambiwa aitumie hivi na asitumie vile kwa manufaa yake na ya dunia anayoishi.
Hakuna mtu asiyetambua hilo hasa kwa hawa wasomi wetu wanaojitambua.
Kila mtu anaitambua mannual yake, na akiishi kinyume chake lazima atapatwa na madhara na yatamharibu.
Uharibifu tunaouona sasa haujasababishwa na mtengenezaji wetu na dunia yetu, bali sisi watu, sisi ndio wasababishaji kwani tunaikiuka mannual yetu, tuliyokabidhiwa na mtengenezaji wetu na dunia yetu hii tunayoishi.
Kwako Vumilika
 
Hayo yote uliyoyataja ni matokeo ya kazi za wanadamu isipokuwa kifo na hata sababu ya kufa ni inatokana na sisi wenyewe, ulimwengu ulipoumbwa ulikuwa ni sehemu nzuri ya kuishi, binadamu wa kale walikuwa wakiishi kwa muda mrefu na afya zao zilikuwa ni imara, tatizo sisi tunaojiita GT ndiyo tuliyoharibu mazingira yetu kwa mikono yetu, kwanza utumiaji mbaya wa moto umeweza kuathiri uchafuzi wa mazingira, kwa kuwa tunapounguza baadhi ya vitu hatujui vinatengeneza sumu ya aina gani ambayo inatuathiri kiafya, na binadamu amefanya mambo mengi ambayo mengine yametusaidia na mengine yanatuangamiza, bila shaka tunafahamu jinsi gani viwanda vinachangia katika kuharibu mazingira, sumu zinazomwagwa baharini, madawa yanayotumiwa katika vyakula, ajali za barabarani au angani au majini, hivi vyote ni kazi za binadamu leo tunamsingizia Mungu kwanini?
Matetemeko ya ardhi yanatokea kwa sababu maalum, wataalamu wanasema tetemeko la ardhi alinatokea kwa sababu kuna tabaka la miamba chini ya ardhi inavunjika katika kingo zake zenye hitilafu, hivi jinsi tunavyopigana mabomu au kuchimba mafuta na gesi, uchimbaji wa dhahabu, hivi kweli hizo tabaka zitakuwa salama? Tusiwe great thinkers lakini bado tu hatujaona sisi wanadamu ndiyo wenye kusababisha matatizo yote haya halafu tunasema Mungu kashindwa kuumba ulimwengu bila ya mabaya?
Dunia ni sehemu ya mtihani kwa wanadamu ndiyo maana tunazaliwa na kufa, ukifaulu hapa duniani basi maisha ya baadaye ndiyo utakayofaidi na kama ukifeli basi hayo maisha ya milele utakuwa mwenye hasara.
Hebu kaa chini halafu jiulize kwanini mimi nimeumbwa? Na kwanini mimi ni binadamu na si mbu au inzi au mende? Hii akili ninayoitumia kufikiri ni uhodari wangu au nilizaliwa nikiwa najua kila kitu na nitajua kila kitu mpaka naaga dunia?
Naomba tutafute maarifa yenye manufaa, tujadili jinsi gani tutaweza kuleta amani kwenye nafsi zetu na kwenye majumba yetu hatimaye imani hiyo ijae ulimwenguni kote. Upendo wa kweli ni ule upendo wa kumpenda mwenzako jinsi unavyojipenda wewe, na kwa kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho basi na mapenzi yana mwanzo na mwisho, na ubora wa mwisho ni mwisho mwema.
Najua ndugu yangu Kiranga umefikia kufikiri fikra hizo kwa sababu, na hizo sababu ni wewe mwenyewe ndiye mwenye kuzijua, kwa kuwa sisi binadamu ni dhaifu na tunapitia changamoto mbalimbali katika maisha, sasa changamoto hizo zisikufanye utoke nje ya mstari wa kwamba wewe umeumbwa na kuna aliyekuumba, utakuwa hujajitendea haki, usione sasa hivi unaweza kuandika hayo unayoyataka lakini ukiondokewa na neema ya kuona (Mungu akuepushiye mbali) basi ni mtihani mkubwa huo sijui itakuwaje?
Mungu akulipe kheri nyingi zaidi. Jumaa kariim.
 
Aameen, kwa sote.
Imani yangu juu yako, Mungu amekujaalia hekma sana. Kwa baraka za Mungu juu ya hekma alizokupa amfanye Kiranga ni mwenye kuelewa ulichokiandika kuhusu uwepo wa Mungu.

Aameeen.
 
ni africa tu ndo tuna danganyana binadamu wa kale alikua akiishi miaka mingi ,umetumia proof gani kutamka hivyo sababu population ya tanzania nzima miaka ya 1900 ilikua milioni 7 , watu walikua wakifa karibu sawa na wanavyozaliwa kwani vitishio vya maisha ya mwanadamu vilikua vingi tu . anza na malaria unayokimbilia dawa mara moja enzi izo ni unapelekwa kwa mganga kukuchezea dansi na kafara ya mnyama juu af bado utafariki na utasingiziwa uliwakosea mizimu.
neda kwenye mbuga,njaa na ongelea njaa kama za 1907 ambazo watu laki tatu walikwenda ,vita , na mlo usio na lishe bora ulio hathiri kukua kwa akili. una kuja kudanganya zamani waliishi kwa muda mrefu. afya iliyo imara ata wewe kama unaitaka utaipata , kuna vitu vyakuongeza na kupunguza katika lifestyle yako utakua safi, pia hii ina backing ya sayansi.

na unapoanza kwa kufikiria mambo ya kuumbwa kuumbwa tiari umeingiza fikra za ki binadamu ndani,kwamba vitu vinaumbwa , wewe nikikuuliza nini kiumbve gani hai ulichishuhudia kinaumbwa unaweza nijibu?
why uongelee kitu usichokijua kama vile ni lazima iwe hivyo,unaonyesha huwezi fikiri njee ya ulicho fundishwa kwenye dini yako.
unaongelea maisha ya baadaye ......yani kaa tungeweza kuwaamisha watu wenye kifra potofu ka wewe ningejitolea sababu asilimia kubwa ya umaskini unachangiwa na kufikiria maisha ya baadaye.

tunapodanganyana kwamba tunaweza tenda mema sijui tuende wapi tunakana asili ya uchoyo ,ubinafsi, ukabila,vita na ulafi zilizo saidia wanadamu kuweza kufika karne hii.

kwaio acha kuhubiri kwa lugha nzuri huku unachoongea ni umaskini na ukienda sehemu watu wamepevuka utaamiwa unakipeo cha uandishi wa fairytales
 
Mungu ana ubinadamu maana binadamu siye mkamilifu anaweza akawa na upendeleo, lakini mungu wanaye dai mkamilifu hawezi kuwa hvyo kwa kuwa hayupo.
Hapo ndipoutakapoona huyu Mungu hayupo, katungwa na watu tu.
 
Hayo yote uliyoyataja ni matokeo ya kazi za wanadamu isipokuwa kifo na hata sababu ya kufa ni inatokana na sisi wenyewe, ulimwengu ulipoumbwa ulikuwa ni sehemu nzuri ya kuishi, binadamu wa kale walikuwa wakiishi kwa muda mrefu na afya zao zilikuwa ni imara, tatizo sisi tunaojiita GT ndiyo tuliyoharibu mazingira yetu kwa mikono yetu, kwanza utumiaji mbaya wa moto umeweza kuathiri uchafuzi wa mazingira, kwa kuwa tunapounguza baadhi ya vitu hatujui vinatengeneza sumu ya aina gani ambayo inatuathiri kiafya, na binadamu amefanya mambo mengi ambayo mengine yametusaidia na mengine yanatuangamiza, bila shaka tunafahamu jinsi gani viwanda vinachangia katika kuharibu mazingira, sumu zinazomwagwa baharini, madawa yanayotumiwa katika vyakula, ajali za barabarani au angani au majini, hivi vyote ni kazi za binadamu leo tunamsingizia Mungu kwanini?
Matetemeko ya ardhi yanatokea kwa sababu maalum, wataalamu wanasema tetemeko la ardhi alinatokea kwa sababu kuna tabaka la miamba chini ya ardhi inavunjika katika kingo zake zenye hitilafu, hivi jinsi tunavyopigana mabomu au kuchimba mafuta na gesi, uchimbaji wa dhahabu, hivi kweli hizo tabaka zitakuwa salama? Tusiwe great thinkers lakini bado tu hatujaona sisi wanadamu ndiyo wenye kusababisha matatizo yote haya halafu tunasema Mungu kashindwa kuumba ulimwengu bila ya mabaya?
Dunia ni sehemu ya mtihani kwa wanadamu ndiyo maana tunazaliwa na kufa, ukifaulu hapa duniani basi maisha ya baadaye ndiyo utakayofaidi na kama ukifeli basi hayo maisha ya milele utakuwa mwenye hasara.
Hebu kaa chini halafu jiulize kwanini mimi nimeumbwa? Na kwanini mimi ni binadamu na si mbu au inzi au mende? Hii akili ninayoitumia kufikiri ni uhodari wangu au nilizaliwa nikiwa najua kila kitu na nitajua kila kitu mpaka naaga dunia?
Naomba tutafute maarifa yenye manufaa, tujadili jinsi gani tutaweza kuleta amani kwenye nafsi zetu na kwenye majumba yetu hatimaye imani hiyo ijae ulimwenguni kote. Upendo wa kweli ni ule upendo wa kumpenda mwenzako jinsi unavyojipenda wewe, na kwa kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho basi na mapenzi yana mwanzo na mwisho, na ubora wa mwisho ni mwisho mwema.
Najua ndugu yangu Kiranga umefikia kufikiri fikra hizo kwa sababu, na hizo sababu ni wewe mwenyewe ndiye mwenye kuzijua, kwa kuwa sisi binadamu ni dhaifu na tunapitia changamoto mbalimbali katika maisha, sasa changamoto hizo zisikufanye utoke nje ya mstari wa kwamba wewe umeumbwa na kuna aliyekuumba, utakuwa hujajitendea haki, usione sasa hivi unaweza kuandika hayo unayoyataka lakini ukiondokewa na neema ya kuona (Mungu akuepushiye mbali) basi ni mtihani mkubwa huo sijui itakuwaje?
Unapoanza kwa kusema hayo yote ni matokeo ya kaziza mwanadamu, maana yake unakubalikwamba Mungu hakuwezakuumba ulimwengu ambao hayo yote si matokeoya kazi zamwanadamu na hayapo?

Kwa mfano, ukisema mabaya ni matokeo ya uasi wa mwanadamu, au dhambi za mwanadamu, hujajibu swali la msingi, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao mwanadamu hawezi kutenda dhambi wala uasi?
 
Mungu hajatumia nidhamu uitakayo katika hii dunia, ni kama kusem kwanini kampuni ya kutengeneza meli haijaitengeneza meli iruke kama ndege. Sisi wanadamu tumepewa chaguo au hiari katika mambo yetu ndiyo maana wewe umechagua kutoamini uwepo wa Mungu wakati sisi wengine tumechuagua kuamini uwepo wa Mungu. Sasa tupo katika kushindana kwa hoja mpaka pale tutakapopata yakini ya uhalisia wenyewe.
 
Kampuni ya kutengeneza meli ina uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
 
Back
Top Bottom