Utata: Tarehe ya Sensa ya Watu na Makazi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata: Tarehe ya Sensa ya Watu na Makazi!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bubona, May 3, 2012.

 1. B

  Bubona JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wana JF,

  Sijui ni ipi tarehe sahihi ya tukio tajwa hapo juu hasa baada ya kupata taarifa mbili tofauti kutoka serikalini!

  Wakati akiahirisha Bunge lililomalizika hivi karibuni, Waziri mkuu Mizengo Pinda alitangaza kwamba siku ya sensa ni tarehe 26/8. Vyombo vya habari mbalimbali vimekuwa vikitangaza tarehe hii pia!!
  Naye Mheshimiwa Rais wa JMT alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Mei mosi huko Tanga alitangaza kwamba siku ya sensa ni tarehe 26/12!!! Skiliza hapa dakika ya 49:30 mpaka 50:10 moja kwa moja maana hotuba ni ndefu!! Sikiliza hapa: swahilivilla: Sikiliza kwa makini Rekodi ya Audio: Hotuba ya Rais Kikwete ya "Mei Mosi" 2012 Mkoa wa Tanga

  Naomba tusaidiane kuondoa utata huu!!!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Nami niliposikia live JK akihutubia taifa nikabakia na bumbuwazi!!!!kuna mushkeri sehemu
   
 3. B

  Bubona JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuna uwezekano kwamba swala hili limechanganya wengi! Mimi naona serikali inatakiwa kutoa masahihisho katika hili na kutangaza tarehe sahihi ya tukio! Ikiachwa hivi inaweza kuathiri ufanisi wa zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya nchi!!
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata mimi nilimsikia mkuu nikashangaa nikadhani labda ameibadili. Lakini nyuma yake kulikuwa na bango linalotaja august. Hapa sasa ndipo kurugenzi ya mawasiliano Ikulu inatakiwa ije mapema kutoa ufafanuzi labda Rais aliteleza. Manake bila ufafanuzi huu watu tunachanganyikiwa.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ulimi ulimteleza
   
 6. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,859
  Likes Received: 2,782
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha ulimi kuteleza hapo! Bichwa la NAZI tena Nazi yenyewe ni koroma haliwezi kuwa na kumbukumbu sahihi na kufanya marekebisho hata kama mwandishi wa hotuba amekosea!! Kazi tunayo kwa kweli. PM yuko sahihi, wapi ulishaona sensa inafanyika mwezi wa 12? Eti tena ni siku 1 baada ya Krismasi. Poleni wanabodi kwa hasara tuliyopata kwa kuwa na Rahisi badala ya Rais!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kabisa kookolikoo lakini ujue yule ni mkuu wa nchi anachokisema kina impact kubwa kwa wananchi. Manake kama kuna matangazo yanasema sensa ni august na mtu mwingine akasikia kauli ya Rais inasema vingine basi atachanganyikiwa. Jeshini kauli ya mkubwa huwa ndio inafanyiwa kazi. kwa kufikiri kuwa ulimi ulimteleza ndio maana nikashauri Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilitolee kauli hili jambo kwa manufaa ya watanzania. Rais ni binadamu anaweza kuteleza na nakumbuka alikuwa hasomi. Alisema alikuwa na hotuba Rasmi na ambayo haikuwa rasmi ila maneno yke nadhani yote yalikuwa rasmi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...