UTATA NA USALITI ZAIDI NDANI YA SERIKALI PATA BILA CHENGA HAPA.......Wizara ya Maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTATA NA USALITI ZAIDI NDANI YA SERIKALI PATA BILA CHENGA HAPA.......Wizara ya Maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salas, Jul 22, 2011.

 1. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Rais kikwete anasalitiwa na watendaji wake:
  Zaidi ya asilimia 50% ya watu waishio vijijini hawana huduma ya maji, ikiwa asilimia 8O% ya watanzania ndio inakadiriwa kuwa wanaishi maeneo ya vijijini. Kwa mujibu tafiti zilizofanywa na wizara ya afya na asasi nyingine zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano ni 20,000 kwa mwaka ikiwa ni sawa na mabasi 333 yanayopata ajali kila mwaka pasipo kuwa na mtu aliyesalimika kwenye ajali. Machache kama sio hakuna yamefanywa kufikia asilimia hii ya watu wanaokosa huduma hii muhimu.

  Tumeshuhudia wabunge wakiwa kidedea kusiamamia swala la umeme katika bunge lakini nguvu hizo pia zingeelekezwa kwenye sekta ya maji zingezaa matunda ambayo yangepunguza gharama kubwa inayotumika na wizara ya afya katika ununuzi wa madawa ya magonjwa yanasababishwa na ukosefu wa maji au matumizi ya maji machafu na athari kadha wa kadha katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupoteza nguvu kazi.

  Katikahali ya kukangaynya ikiwa ni muendelezo wa usaliti kwa muheshimiwa rais wetu ni ile hali ya Tanzania kukataa kupiga kura ili kutambua swala maji kama haki ya binadamu katika uchaguzi wa umoja wa kimataifa kutambua haki Maji uliofanyika tarehe 28 july 2010. Tanzania ikiwa nimiongoni mwa nchi 41 zilizopiga kura ya absentation ikiwa ni kuficha aibu ya kukataa haki hii istambulike ikiwa imeongozwa kidedea na USA na nchi nyingine na za ulaya na makoloni ya ulaya ikiwemo kenya. Licha ya hayo nchi 122 zilipiga kura ya kutambua haki hii right to water and sanitation.

  Katika Muendelezo huu wa aibu, ukiwa unafanywa kwa lengo ama la kumdhalilisha Mheshimiwa rais au kutowajibika kwa viongozi wa idara husika Mheshimiwa rais alishapitisha sheria ya maji na usafi wa mazingira sheria namba 12 ya mwaka 2009 inayotambua kuwa maji ni haki ya binadamu. Nita quote “ 4.-(1) The objective of this act is to promote and ensure the right of every person in Tanzania to have access to efficient, effective and sustainable water supply and sanitation services for all purpose”

  Nachelea kudadavua kuwa huu ni usaliti wa makusudi ambao pia umewahi kufanywa katika kipindi cha vijiji vya ujamaa ambapo jitahada safi za Mwalimu Julius Kambarage nyerere zilipotoshwa na walarushwa wachache katika kuhujumu mawazo sahihi ya Mwalimu ili kuweza kufikisha huduma za jamii kwa watu wake ikiwemo maji na nyinginezo. Tukumbuke pia mwalimu aliweza kufanya kazi katika miongo miwili kwa kauli mbiu ya maji kwa wote. Swali ni Je kwanini hawakusaini in favor ya right to water and sanitation na wakati sheria ziko wazi ??????

  Hizi ni hujuma kama zile zinazoendelea kwenye miradi ya vijiji kumi ambapo japo wizara husika haitaki kuweka bayana kuwa vijiji sio kumi tena ila vitatu kutokana na ubadhirifu wa wataalamu washauri ambao mashirika yameundwa kiuhuni ili kuhujumu nia safi ya Rais kuwapatia huduma ya maji watu wake. Gharama za mradi zimekuwa kubwa kushinda fedha na waziri mwenye dhamana anakiri hilo kwenye hotuba yake ya wiki ya maji ili hali anajua anajua kuwa sio mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa kwenye design ya hiyo miradi ni wizi wa wataalam washauri ili makampuni ya kijanja ya ujenzi yaje kukwapua hizo hela. Huu ni ufisadi mwingine kwa ajili ya kuja kumchafua mheshimiwa rais.

  Ninasisitiza kuna haja ya kila mtu kusimama kwenye nafasi yake katika kuleta maendeleo ya hii nchi, maisha bora yatafikiwa pale tu kila mtu mmoja mmoja atakapofanya kazi kikamilifu katika nafasi yake.

  hakika kikulacho kinguoni mwako huu ni muendelezo wa usaliti dhidi ya rais wetu Mtukufu wa Jamuhuri ya Tanzania. ​
   
Loading...