Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,793
IMG_20180209_021612_717.jpg
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.

Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.

Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?

Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.

Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.

Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwa wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.

v1.jpg

Ibada za kutoa kafara katika satanism

Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.

Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.

Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.

Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.

Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.

Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?

Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!

Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.

Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.

Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.

Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.

Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!
 
Duh

Hii mpya kabisa kichwan mwangu

Hahaha kumbe mungu aliruhusu mke zaidi ya mmoja?! Alimuumba Adam, Eva na Lilith. Mbona siku hizi wanawake hawataki?!
Habari za Lilith hazijaandikwa popote kwenye Biblia takatifu, na huko zilikoandikwa si kwa wema bali kwa ubaya ukiachilia satanism na atheism.
 
Dunia imejaa nadharia nyingi, ukiijua hii wengine wanajua ile

Kweli dunia tajiri

Ahsante kaka mshana Jr. Ila Dini zina nichanganya.
Naona hapa kuna mahali Mungu anahusishwa na samael (malaika?) Kwamba yeye ndio alikuwa sumu ya Mungu!? Haya mafundisho ni ya kwenda nayo kwa tahadhari usiwe ukajikuta unaangukia upande mwingine
IMG_20180209_044021_233.jpg
dhana nyingine ni hii hapa ya Lilith kumhasi Samuel asiweze kuzaa... Hawa wawili Lilith ana samael naona wanatajwa sana
IMG_20180209_043950_925.jpg
 
Naona hapa kuna mahali Mungu anahusishwa na samael (malaika?) Kwamba yeye ndio alikuwa sumu ya Mungu!? Haya mafundisho ni ya kwenda nayo kwa tahadhari usiwe ukajikuta unaangukia upande mwingine View attachment 692891dhana nyingine ni hii hapa ya Lilith kumhasi Samuel asiweze kuzaa... Hawa wawili Lilith ana samael naona wanatajwa sanaView attachment 692892
Hizi tales za ajabu sana

Kuna page namsoma huyu lilith eti ni mother of all demons

Kwamba anaiba sperm from men na kujitungisha mimba then anazaa demons

Sasa kuna brother here at hamlet ana low sperms yawezekana lilith kafanya yake just jokes
 
I see! Nilikuwa sijawahi ckia hizo habari za shost ake na Hawa... ngoja nami niingie online library nimbukue kidogo!!

Sema dah, mara malkia wa giza, mara malkia wa jehanamu, mara Lilith hivi; mara Lilith vile... yaani makombora yote hayo anayopigwa kisa tu kv kamtema Adam!

Hivi huyu Adam nae si ni miongoni mwa wateule wa Mungu; au?! Kama ndivyo, huku Uswahilini si huwa tunaambiana eti mke mwema hutoka kwa Mungu; au?

Kama ndivyo, how come tena mteule wa Mungu akapata mke asiye na sifa za kutoka kwa Mungu?!

Kama mke mwema hutoka kwa Mungu; mke muovu si itakuwa hutoka kwa shetani; au?

Kama ndivyo, ina maana mteule wa Mungu aliletewa mzigo na shetani?!

Oh! Nasikia Mungu aliumba dunia kwa cku 6 na cku ya 7 akaamua kula good time! Nimepatia?!

Kama ndivyo, au inawezekana Shetani alimlia timing Mungu, na ilipofika cku nyingine Jamaa akawa anakula good time; shetani akaupenyeza mzigo kwa Mwana Mteule!!

Au hii good time alikula mara moja tu?!

Hebu ngoja, kabla sijaendelea...

Hivi ukifukunyua fukunyua mara oh, mbona kama hivi ipo vile, mara oh, kama ndivyo mbona iko hivi... hapa vipi; naweza kupata dhambi?!

Nakumbuka enzi hizo tuko Madras Hidayat Kurasini; Ustaadhi alikuwa anatuambia ukitaka kufahamu balaa la moto wa jahanamu; ziba masikio yote mawili kwa viganja vya mikono usikie moto wa jahanamu unavyounguruma!!

Basi ukitoka hapo, hata ukikutana na braza wa Std VII lazima umpe shikamoo ili usije ukakumbana na lijimoto la jahanamu ambalo umelisikia "Live!"

Mungu anakuona Ustaadhi wangu, yaani bila huruma unavilisha matango pori vitoto vidogo!
 
Habari nje ya Biblia sio habari ya kubiblia, ni simulizi za mtaani
Nje ya biblia gani.ya kikatoliki au ya kiprotestant? Maana hizo biblia walianza wakatoliki wakachambua vitabu na kuchukua vichache kati ya vingi.

hivyo kuna maandiko mengi tu ya kidini nje ya biblia yamehifafhiwa tu, wakaja waprotestant nao wakachukua bilia ya kikatoriki wakaichambua na kuchukua vitabu vichache na kuacha vingine kama 8 hivi, maana biblia ya kikatoliki ina vitabu 72 na ya kiprotestant ina vitabu 64
 
Back
Top Bottom