Utata: Kifo cha Wa Mutharika na Unabii wa TB Joshua.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata: Kifo cha Wa Mutharika na Unabii wa TB Joshua..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TANMO, Apr 8, 2012.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Wakuu heshima mbele na Poleni sana kwa Misiba iliyotokea na kuwagusa wengi kwa namna moja ama nyingine. Pia Heri ya Sikukuu kwa wale wanaohusika.

  Wakuu kuna hoja nimeipata kutoka kwa Rafiki yangu Mmalawi kuwa Tarehe 28/02/2012 aliyekuwa Rais wa Malawi Bwana Wa Mutharika alienda nchini Nigeria kucheki afya yake iliyokuwa inamsumbua na Madaktari waliomfanyia vipimo wakagundua kuwa kwa mujibu wa vipimo basi Wa Mutharika amebakiza siku chache (inasemekana miezi 4) sana za kuishi kutokana na ukweli kwamba ugonjwa wake usingeweza kudhibitiwa tena.

  Hivyo kutokana na kwamba miongoni mwa Madaktari waliomfanyia uchunguzi ni waumini wa Mchungaji TB Joshua basi wakamweleza Mchungaji juu ya Afya ya Bwana Wa Mutharika na kwamba ana Maximum ya miezi minne ya kuishi. Na ndiyo maana TB Joshua baada ya kutangaza "kupata maono" akawa anasisitiza watu kumuombea huyo Rais (hakutaja jina) ili kifo kimuepuke, kwamba ni miujiza pekee ingeweza kumwepusha na umauti.

  Baada ya "Utabiri" wa TB Joshua inasemekana kuwa Wa Mutharika alijaribu kuwatoa hofu wa Malawi kuwa siyo yeye anayelengwa na kwamba yuko imara kiafya huku mwenyewe akitambua wazi kuwa ndiye mlengwa wa "ule utabiri"

  Ngoja niendelee kukusanya data, nitarejea. Kama kuna yeyote mwenye taarifa kuhusu hili siyo mbaya akaongezea, aidha kwa kukubaliana na hii hoja ama kuipinga.

  Mapendo.
  TANMO.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mmmmmmhhhhhhh......
  Makubwa.......
  Kufa amekufa tayari hakuna namna.
  Kila moja atasema lake sasa.

  Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe... Amen!
   
 3. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Ebwana nakuunga mkono zaidi ya 100% basing on the fact that, baada ya YESU hakuna nabii yoyote aliyetumwa na Mungu, wote vibaka tu.
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Mkuu cha muhimu ni kutafuta ukweli ili kuujua ukweli.
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Kama hivyo ndivyo basi ni kwa nini hawa wanajiita manabii?
   
 6. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna tofauti gani kati ya Nabii na Mtume? Msaada tafadhali
   
 7. u

  utantambua JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona utabiri wa TB Joshua ulitoka kabla ya tarehe 28.2.2012? Kuna thread ilianzishwa kuhusiana na utabiri wa Joshua hapa JF tarehe 9.2.2012 hii ina maana ni siku 19 kabla ya madai yako ya Mutharika kwenda Nigeria kwenye huo uchunguzi. Jina la thread hiyo ni RAISI MMOJA WA AFRIKA ATAKUFA HIVI KARIBUNI-TB JOSHUA. Itafute ipo kwenye international forum.

  So acheni jitihada za kumdiscredit Joshua kwa sababu tu humuamini binafsi
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Ngoja niendelee kuperuzi na kudadisi juu ya mambo haya:
  Kuwa Bingu wa Mutharika alikwenda Nijeria kupima afya yake?!, kuwa ilionekana kuwa hali ya afya yake ni mbaya, kuwa ilioneana kuwa hataishi zaidi ya miezi minne?!, kuwa aliwaasa wapgakura wake kuwa utabiri wa Joshua haukuwa unamgusa yeye?!, kuwa daktari aliyemchunguza ni muumini/mshirika wa TB J. ، kuwa daktari wa Bingu alimdokeza TBJ juu ya afya ya Bingu(breach of ethics).?! Na kuwa TBJ akatangaza kiwa ni unabii alionesha na Holy spirit in Jesus christ name?!. Nikithibitisha machahche kati ya haya nitafungua tovuti maalum ya kupinga unabii wa hawa manabii wa kisasa. BTW, kwa kuwa rais wetu mtarajiwa Ndg. Edward Ngoyai Lowasa nae alienda nijeria na kuhudhuria ibada maalum katika sinagogi la TBJ naamini punde unabii utatolewa kuwa Mungu amemteua kuwa rais wa nchi hii iliyokosa mwelekeo. Na si unakimbuka kuwa baada ya ziara ya Mh. Ngoyai kule Nijeria muwakilishi wa TBJ alitoa mchango wa sh. Mil. 10 kwa waathirika wa mabomu ya gongolamboto?!, .............
   
 9. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Umedanganyika kirahisi hivyo? Kama kweli alienda Nigeria tarehe hiyo basi unabii ulitoka zaidi ya siku 18 kabla ya kifo chake.
   
 10. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Vitu vingine visome kwanza ndipo u post. Unadanganywa na rafiki yako halafu na wewe waja kudanganya GTs. Bingu hakuwa na saratani hatarishi mpaka apewe siku chache za kuishi. Amekufa kwa Heart Attack (Myocardial Infarction).
  Usidanganye watu bwana.
   
 11. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Mimi pia sina imani na unabii wa Nigeria maana una mahusiano ya karibu sana na pesa-money
   
 12. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nabii ni mtu anayetabiri mambo ya wakati ujao...foreteller.mfano Yohane Mbatizaji alipokuwa anawaambia watu
  yatayarisheni mapito ya Bwana...yu aja aliye mkuu kuliko mimi...sistahili hata kufungua hijamu za viatu vyake...kwa kufanya hivyo anafanya kazi ya kinabii. Kumbe mtume ni Mtu anayeleta ujumbe wa M'Mungu kwa watu wake na kuwaasa
  waenende katika mwenendo mwema. Mfano tunapoambiwa tusiibe, tusiwe mafisadi nk hapo anafanya kazi ya Kitume.
  Lakini vyote kwa vyote Unabii hausomewi wala kufundishwa tofauti na Utume.
   
 13. NOT FOUND

  NOT FOUND Senior Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  HAHAHAHAAAAAAAAA AISEE SITAKI KUTETEA UTABIRI WA TB JOSHUA KWENYE HILI LAKINI NI UONGO KWAMBA JAMAA ALIENDA NIGERIA KUFANYA CHECK UP.

  SOMA MITANDAO KIBAO YA MALAWI INADISCUSS KIFO CHA HUYU JAMAA.

  NA HATA MTANDAO NAMBA MOJA WA NIGERIA nairaland.com PIA WAMEMWAGA DATA ZOTE NA HAKUNA ALIYESEMA BINGU ASHAWAI KWENDA FANYA CHECK UP NIGERIA.

  INGEKUWA SOUTH AFRICA KWELI. MAANA NDIPO ALIPOKUWA ANAENDA KUFANYA CHECK UP NA ANA MADAKTARI WAKE KULE.

  KWA KIFUPI HUYO JAMAA YAKO KAAMUA KUKUTUNGIA UONGO ILI KUMPUNGUZIA JOSHUA COMPLIMENTS ANAZOPATA.

  BINAFSI NISHAWAHI KUSOMA UTABIRI WA JAMAA KUHUSINA NA AJALI YA NDEGE NA AKATAJA SIKU YA JUMATANO KABISA. NA KWELI JUMATANO NACHECK NEWS KWENYE HOMEPAGE YA YAHOO NAONA PLANE CRASH NA WATU 48 WAMEKUFA.

  KIFUPI TABIRI ZA JAMAA ZINAUKWELI JAPO SINA UHAKIKA KAMA NI MUNGU KWELI AU KUNA LA ZIADA.

  LAKINI TABIRI ZAKE ZINA UKWELI, SIO KAMA ZILIVYOKUWA ZA SHKH YAHYA.
   
 14. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Mkuu nashukuru nimeiona hiyo thread, ngoja nifuatilie kwa huyu Mdau kisha nitarejea..

  Mkuu Ozzie,
  nashukuru kwa angalizo, hata hivyo zingatia kuwa nimeomba yeyote mwenye data zaidi amwage hapa. Binafsi sijawahi kuwa interested kufuatilia mambo ya huyu Nabii mpaka leo hii huyu Bwana alivyonipa utata juu ya kifo cha Rais wao pamoja na Utabiri wa TB Joshua,

  nitamfuatilia kwa undani ili nimjue zaidi.


  Mkuu ngoja nipitie tabiri za huyu Nabii, huenda kuna nitakalojifunza.. Thanks
   
 15. M

  Maseto JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  To quote Prophet Joshua: 'the next Tanzanian president is Edward Lowasa...'
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Kuna watu hapa wataanza kuimba aleluyah,lol!
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Ila nafikiri kwa yale aliyopanga kuifanyia malawi, huyu bwana bora ameenda mapema. Alitaka kuigeuza nchi ile kama moja ya nyumba zake. Anajifanyia lolote anavyotaka. Mungu akasikiliza sala za watu wema kabla mambo hayaja haribika.
   
 18. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  je vipi utabiri wake wa timu ya zambia kutwaa taji la AFCON alizipata nyepesi wapi? Marefari walimwambia? Na vipi kuhusu utabiri wake kuwa drogba atakosa penalti? Sipendi tuamini sana mambo ya utabiri ila linapotokea tuangalie uhalisia wake badala ya ushabiki
   
 19. paty

  paty JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  waalizusha ni mugabe atakufa , akafa mutharika, wakakimbilia kusema oooh tulikuwa tunammaanisha Mutharika wa malawi ,
  wezi wezi wezi tu hao manabii
   
 20. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Na yule wa Mbezi Beach aliyetabiri Siyoi kumshinda Nassari Arumeru tumuite nani?
   
Loading...