Utata katika uteuzi wa majaji znz

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
CHAMA Cha Mawakili Zanzibar (ZLS) kimepinga uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu uliofanywa na Rais wa Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohammed Shein Novemba 29 mwaka huu wa 2010 na kuhoji uhalali wa uwepo wa Jaji Mkuu wa Zanzibar aliyestaafu.
Tayari ZLS kimemwandikia barua Dk Shein Novemba 30, ambayo Mwananchi ilifanikiwa kuiona nakala yake kikieleleza kuwa hakijaridhishwa na uteuzi huo kwa kuwa haukuzingatia vigezo na kwamba, umekiuka sheria kwa kuwa hakijashirikishwa. "Rais, katika uteuzi wako huo, ambao umetumia mamlaka uliyopewa na Katiba ya Zanzibar ya 1984 kifungu cha 94(2) na (3), Chama cha Mawakili hakina mashaka na uteuzi wa Abdul-hakim Ameir Issa, wala uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi, Haroub Shehe Pandu. Mashaka yetu yapo katika uteuzi wa waheshimiwa kuanzia nambari 2 mpaka 4,” Sehemu yabarua yao kwa Dk Shein ZLS inasome“Rais, sisi mawakili ambao tumetia saini barua hii tukiwa ni wadau wakubwa katika sekta hii, tuna imani kubwa nawe ..., lakini tunaamini washauri wako hawakukutendea haki walipokushauri uwateue Fatma, Mkusa na Rabia kuwa majaji wa Mahakama Kuu,” ilieleza barua ya ZLS na kuongeza:

"Rais, haitoshi tu kusema kwamba Jaji Mteule ametimiza masharti ya Katiba na hivyo anafaa kuwa Jaji wa Mahkama Kuu. Mmoja wa majaji hao wanne waliolalamikiwa (Fatma Hamid Mahmoud) ametajwa kuwa ni mtoto wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud huku mawakili hao wakieleza pia kwamba uwepo wake katika wadhifa wa jaji mkuu una mashaka kikatiba na ukiukwaji wa taratibu za kisheria.

“Mheshimiwa Rais, sisi kama chama cha mawakili, tunaamini hata uwepo wa Hamid Mahmoud kama Jaji Mkuu wa Zanzibar una mashaka tele ya kikatiba. Inaeleweka kwamba Hamid Mahmoud alistaafu kwa hiari alipotimiza miaka 60," ............SOURCE (MWANANCHI)

Wadau nadhani waliosoma gazeti la mwananchi leo wameona hii habari, Kwanza nawapongeza hawa wanasheria kwa moyo wa ujasiri and their bouldness kuandika barua hii, nikimnukuu Hayati baba wa Taifa katika kitabu chake, Uongozi wetu na hatima ya Tanzania alisema ".......Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga, si dalili ya heshima; na woga na heshima ni vitu viwili mbali mbali. Maadili mema hayatudai tuwaogope viongozi wetu.." Na tuna misemo yetu ya kiswahili kwamba kuanza upya si ujinga., Ikiwa Mkuu wa Zanzibar utaweza kuainisha mapungufu katika uteuzi wako na kwamba kulikuwa na mapungufu katika mapendezkezo kutoka kwa washauri wako muda bado unakuruhusu kufanya maamuzi ya busara! Lakini pia ni wakati muafaka wa kuwajibishana pale itakapoonekana ushauri haukubase katika vigezo vya kitaaluma, kiutalaam, kiuwezo na uzoefu

Nawasilisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom