Utata katika maamuzi ya mahakama zetu na uhusiano na ikulu...dawa yake ni katiba mpya.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata katika maamuzi ya mahakama zetu na uhusiano na ikulu...dawa yake ni katiba mpya....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Apr 6, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Ikulu hawawezi kupinga kuwa na influence kwenye mahakama zetu TZ.....hili linajulikana sana...sema watanzania ni wasahaulifu sana....yamewahi kufanywa maamuzi na mahakama za TZ ambayo yamewahi kuhusishwa na ikulu kabisa....mifano tunayo sana...cha kushangaza kwa hili la Lema ni kwamba this time ikulu wamejibu fasta sana....wakiashiria kuguswa moja kwa moja kwani Lema ameongea wazi kuwa ikulu imehusika...........maamuzi mengine yaliyowahi kutolewa na mahakama na kuhusishwa na ikulu hayakuwahi kujibiwa fasta na ikulu kwani wahusika hawakuwataja ikulu moja kwa moja...Labda sasa watanzania waamke wayatafakari yale maamuzi tata ya mahakama zetu TZ yaliyowahi kuhusisha ikulu....ili iwe kama reminder kwa ukulu kuwa wamewahi ku influence mahakama kwenye maamuzi yake tata.....na tunaposema ikulu hapa itambuliwe kuwa ni JK....yeye ndiye amepanga ikulu yetu...na hawa kina salva wanaongea kwa niaba yake..hata kama wanatumia lugha kali..haya yanatoka kwa JK....Kwa kujikumbusha tu moja ya maamuzi tata ya mahakama yaliyowahi kuhusishwa na ikulu ni ile amri ya hivi majuzi tu iliyotolewa na mahakama kuu ya kazi TZ dhidi ya madaktari waliokuwa kwenye mgomo...ikiwataka madaktari wasitishe mgomo na warudi kazini mara moja......kama wengi mnavyojua ile hukumu iliisha bila amri ya mahakama kutekelezwa(madaktari walirudi baada ya kuongea na JK).......na pia JK wakati akiongea na madaktari aliulizwa na madaktari kuhusu amri ya mahakama na akasema mbele yao kuwa hayo ya mahakama wayasahau.......Ninashangaaa sana ikulu inapokuja na statements hizi kwa kina Lema wakati tunajua kuwa TZ ikulu ina influence kubwa kwenye maamuzi kwenye mahakama zetu.....Watanzana wakumbuke kuwa dawa mojawapo ya tatizo hili ni kuondoa kile kipengele kwenye katiba yetu kinachoruhusu majaji kuteuliwa na rais.....yooote haya tunayaona leo kwa kuwa majaji hawa wanafanya mambo ya hovyo hovyo nchi hii kama sehemu ya kulipa fadhila kwa anayewateua..yaani rais(ikulu)...........

  ANGALIZO KWA MODS: Hii post iacheni ichangiwe(msii merge kwenye post zingine)..maana hoja hapa ni muingiliano wa maamuzi ya mahakama zetu TZ na muingiliano na muhimili mwingine yaani ikulu.......we need to discuss this issue here in the context of the new constitution to come......
   
 2. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60


  nakumbuka sana TUCTA kuna siku walikuwa wameandaa maandamano nchi nzima yalikuwa yafanyike jumatatu ya wiki ilyokuwa inafuata.Hii ni kutokana na serikali kushindikana kuishawishi TUCTA kusitisha maandamano hayo.Siku ya jumapili usiku serikari ikaweka zuio kupitia mahakama ya kazi ambalo judge alilikubali.Fikiria ni lini mtu wa kawaida anaweza kuitisha mahakama siku ya jumapili?kama si mkono wa ikulu? na pia ni judge gani anaweza kukubali zuio kubwa kama hili alifanye siku ya mapumziko?kama si mkono wa ikulu.leo kuna kesi ya kagoda wamiliki wake walikubali kurudisha pesa benki baada ya kukundulika kuwa wameiba, je kesi yao ipo mahakamani?kama si mkono wa ikulu?salva aache kufanya watanzania wahajui , au hamnazo bali watu waikulu ndo wanaojua.hayo .ianfasalva si ya ikulu bali yake.wananchi wanafahamu uozo wa kutotenganiswa mihili hii yaani serikali , mahakama na bunge vipo pamoja;ikulu ikitaka kuingilia jambo lolote inafanya.fikiria mpaka leo wasitaafu wa EAC , mbona wanababaishwa huku tayari mahakam ilishakaza hukumu?pia angalia kesi ya wakaaji wa gerezani hukumu yao ilivyokuwa.mkuu wa mkoa akaanza maandalizi ya kuvunja bado hata mahakama haijatoa maamuzi.hata waziri wa tamisemi alitoa hukumu hoyo kwa maneno kabla ya kesi kuhukumiwa.sasa kama si mkono wa ikulu ni nn?
   
 3. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Nchi hii kesi zote kubwa kubwa zinazohusu wizi wa mali za umma/ufisadi zinafunguliwa/kutofunguliwa....zinapelekwa/kutopelekwa mahakamani kwa pressure za ikulu.....hili liko wazi kabisa vinginevyo tujiulize vipi leo wale wezi wa EPA waliorudisha pesa waliachiwa na ikulu(JK)bila kufunguliwa mashtaka wakati wengine kina Manji/Rostam wa kagoda waliorudisha pesa mbona wako free wakati kuna kina Mramba na wenzake wakifunguliwa mashtaka??.......mi naona hata ucheleweshwaji wa kumaliza hizi kesi pia kuna influences za ikulu.....i mean hawa jamaa wanafikiri watanzania wajinga wasiofikiri au kuona?????
   
Loading...