UTATA: Fedha za mtu aliyekufa zilizopo kwenye benki au simu hupotelea wapi?

Kasinja jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
1,034
1,792
Utasikia basi limeua wanne, pikipiki imeua sita au waliokufa Muhimbili wamefika 100 kwa mwaka jana ama meli ya Nungwi imeua 60.

Na hao ni wateja wa M-PESA, Tigo pesa na Airtel money.

Hela zao zinaendaga wapi? Kuna utaratibu upi wa kuwapatia survivorship au next of kin wao?

======

UPDATES: 29 APRIL 2019

Watu wengi nchini siku hizi wanatumia simu za mkononi si kwa kuwasiliana tu, bali pia kuweka na kutuma fedha. Ili kuzifikia fedha hizo kunahitajika namba ya siri. Je, umeshawahi kujiuliza watu wanaokufa wakiwa na fedha kwenye simu zao au kupatwa na majanga mengine, amana zao zinakwenda wapi?

Mara nyingi wasimamizi wa mirathi husahau kufuatilia salio lililomo kwenye akaunti hizo hivyo kupoteza mamilioni ya fedha.
Elizabeth George, mkazi wa jijini hapa anasema isingekuwa kufahamiana kwake na hakimu wa mahakama aliyofuatilia mirathi ya kaka yake aliyefariki ghafla mkoani Mbeya, akiba iliyokuwamo kwenye simu za marehemu ingepotea.

“Kaka alifariki ghafla. Baada ya mazishi wifi akateuliwa kusimamia mirathi. Nilimsindikiza mahakamani kwenda kusajili kwa sababu nilikuwa nafahamiana na hakimu. Huyo hakimu alituuliza kama marehemu alikuwa na simu na tumeangalia salio lililomo,” alisema Elizabeth.

Hawakuwa na wazo hilo na wifi yake hakuwa anajua namba za siri za simu zote tatu za mumewe. Waliandikisha na wifi yake akafuatilia kwenye kampuni zote tatu ambazo zilikuwa ni Mpesa, Tigopesa na Airtel Money.

Baada ya kufuatilia, anasema walikuta Sh2 milioni kwenye akaunti ya Mpesa, Sh1.5 milioni kwenye Airtel Money na Sh980,000 kwenye Tigopesa. “Tusingekumbushwa, fedha hizi zingepotea,” alisema Elizabeth.

Tangu simu za mkononi zilipoanza kutoa huduma za fedha, muongo takriban mmoja uliopita, hadi Desemba 2018, taarifa za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kulikuwa na watumiaji milioni 23.3 kati ya watumiaji milioni 43.6 wa simu za mkononi waliosajiliwa.

Wengi wa wateja hao wamekuwa wakisahau kujumuisha akiba iliyomo kwenye simu za mkononi hivyo Serikali kukusanya mapato hayo kwa kipengele cha mali isiyo na mwenyewe.

Mkurugenzi wa usimamizi wa mashauri ya Mahakama Tanzania, Eva Nkya alisema suala la kuainisha mali na madeni ya marehemu hufanywa katika kikao cha familia kabla ya kusajili mirathi husika mahakamani. Kazi kubwa ya msimamizi wa mirathi ni kufanya uchunguzi wa kutosha ili kukusanya mali zote katika akaunti za benki na simu za mkononi, hisa za kampuni, riba za mikopo aliyokopesha, pensheni na bima, kisha kulipa madeni ya marehemu na kugawa mali kwa warithi.

“Sheria inampa msimamizi wa mirathi muda wa kutosha kukusanya mali, kuzigawa na kulipa madeni kama yapo na mwisho mirathi kufungwa. Kwa mahakama za mwanzo, msimamizi hupewa miezi minne na kwingine ni miezi sita,” alisema Eva.

Akaunti ya simu

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya Tigo, William Mpinga alisema kuna sababu kadhaa za kuzingatia kabla ya kufunga akaunti iliyotelekezwa ya Tigopesa.

Sababu hizo alisema ni kutotumika kwa akaunti husika kwa walau miezi sita akisema itakufa kabisa endapo namba haitopiga simu, kutumika kwenye data, kutuma ujumbe mfupi wa maneno au kuongeza salio kwa miezi mitatu au zaidi.

Sababu nyingine ni akaunti kuhusika katika uhalifu, mteja mwenye akaunti kufariki na taarifa zake kuwasilishwa Tigo. “Hata mamlaka kama TCRA, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) au vyombo vya sheria vikitoa agizo namba na akaunti hiyo hufungwa.”

Kwa mteja ambaye akaunti haijafanya kazi kwa miezi sita na zaidi au mteja mwenye akaunti amefariki na taarifa kuwasilishwa Tigo, Mpinga alisema, “akiba iliyokuwamo hurudishwa.”

Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Vodacom, Ian Ferrao aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa akaunti ya mteja wa M-Pesa huendelea kuwa hai kwa siku 270 na baada ya hapo salio lililopo huhamishiwa BoT na akaunti kufungwa kwa mujibu wa sheria lakini mteja akijitokeza, salio lake hurudishwa.

Kampuni za simu hutunza fedha kwenye akaunti ya benki ijulikanayo kama Akaunti ya Trust na inapotokea mteja hajatumia akaunti yake ya simu kwa muda mrefu iwe kutokana na kifo, kusafiri nje ya nchi, kufungwa gerezani au kuugua, salio lake huhamishiwa BoT.

Zinapohamishiwa BoT, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bernard Dadi alisema hutunzwa kwa kuzingatia (Sheria ya Mali Isiyo na Mwenyewe) Unclaimed Property Act.

Huduma za fedha kwa simu za mkononi, zinasimamiwa na kifungu cha 31 cha Kanuni za Fedha za Miamala za mwaka 2015. Endapo mteja husika hatajitokeza kwa muda muafaka (kati ya miezi sita hadi tisa kutegemea na kampuni ya simu), fedha hizo huhamishiwa serikalini.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kigezo kikubwa kinachozingatiwa kuifanya akaunti ionekane imetelekezwa, Dadi alisema ni ukomo wa miaka mitano ya mwenye akaunti kutojitokeza.

Muda huo ukipita, BoT huzipeleka fedha husika kwa Msajili wa Hazina baada ya kuzipokea kutoka kwa watoa huduma. Lakini, endapo mteja wa akaunti atapatikana au mrithi wake kujitokeza na kukamilisha utaratibu wa mirathi, basi kampuni ya simu humsaidia kuzipata fedha za marehemu.
“Asipojitokeza kwa miaka 15 Serikali huzitumia,” alifafanua.



Akaunti za benki


Utaratibu wa kutambua na kukusanya mali isiyo na mwenyewe pia hutumika kwenye akaunti za benki ambako mteja asiyeitumia akaunti yake kwa miaka 15 mfululizo, salio lake huhamishiwa BoT.
Mteja wa akaunti au mali iliyohifadhiwa benki asipoonekana kwa muda huo, Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha inaagiza akiba iliyomo au mali husika iliyohifadhiwa kuhesabiwa kama iliyotelekezwa.



Baada ya miaka 15 ya fedha hizo kutunzwa BoT, hupelekwa serikalini na kupangiwa matumizi kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Serikali mambo yaliyokuwa na faida kwa wananchi wanayaficha na hawataki hata kuyaongea. Kwanini watu wakifa hatua ya mwanzo wenye jamaa zao wasitakiwe kufika kwenye hizi taasisi za kifedha kama hizo ulizozitaja?
 
Kuna mtalamu mmoja alisema hv kuwa iwapo mwenye simu amefariki zile pesa hukaa miaka kama Kitano hivi, mhusika au ndugu mpaka muwe na uthibisho ulio kamili usiotia shaka ikithibitika mnapewa pesa. Ila ikishindikana ndani ya hiyo miaka pesa hurudishwa bot na kuwa Mali ya bot.
 
Nakumbuka hii kitu, mume sheji ake mie aliwahi kuisemea in deeper humu jamvini mwaka 2016 kama sijasahau
 
Hugeuzwa na kuwa ' Gawiwo ' kwa Sisi ambao huwa tunabaki hai na tuliotabiriwa kuishi kwa miaka mingi ijayo.
 
Mleta Mada Big Up Sana umeleta Mada fikirishi Sana. Mitandao ya simu line ikikaa angalau miezi 6 bila kutumia kabisa huwa wanafunga line kabisa najua Hivyo kwa Baadhi ya Mitandao. Sasa let say marehemu kafariki line yake Ilikuwa na Tshs. 73500 nani huzichua? Swali zuri. Nadhani humu JF Halotel wana account yao, Mleta Mada Naomba uwa tag ili watujibu kwa upande wao. Kula like kwa Mada yako
 
Simu sio pahala pa kutunzia fedha Bali bank.
Kwa sheria na taratibu zilizopo hizo fedha zikizidi muda Fulani zinapelekwa BOT.
 
Nadhani hakuna linaloshindikana kuhusiana na mali ama fedha za marehemu zitachukuliwa vipi kama warithi watatambulika kisheria!
 
Msimamizi wa mirathi anakuwa na jukumu la kuzitambua na kukusanya mali zote za marehemu ili azigawe kwa warithi halali.

Kampuni za simu zitamlipa
Masalio yoyote katika simu za marehemu kwa mamlaka ya kimahakama ya usimamizi wa mirathi.

Hakuna lazima ya kuwa na password/ nywila - bali kuzijua namba za simu za marehemu inatosha.
 
Account ya ikikaa miezi mitatu Bila kutumika hufungwa. Hela hizo sijui makampuni ya simu huzipeleka wapi.
Ila kama una death certificate Na barua ya usimamizi wa mirathi utapata haki za marehemu wako
 
Wabongo kwa lawama, kila kitu kiko under control.....niliona jamaa yangu akipewa laki 5 za marehemu. Makampuni yote yameainishiwa taratibu za kufuata pindi mteja wao anapofariki(BOT)
 
Wafanyakazi wasio waaminifu nahisi hufaidika na hili kama kutakuwa na uzembe katika mifumo yao ya usimamizi wa akaunti zilizo lala/ domant account

Mfanyakazi akiona akaunt imelala kwa muda mrefu anaweza ivuta pesa mfano kuna jamaa yangu aliweka pesa zaid ya laki 5(2014) katika mtandaomflan ila akakaa muda sana passipo kuweka wala kutoa pesa kwakuwa maswala ya pesa yalijifunza kwakuwa alikosea password alipotaka kutoa ila line ilikuwa ikitumika cha ajabu ni kwamba siku ameenda ku_ reactivate akaunt yake pesa alikuta ipo nusu,ilichukua muda sana mpaka kuipata pesa yake yote, lakini hakuwahi kupewa jibu la kueleweka juu ya nini kilitokea katika akaunti yake mpaka akawa debited 300,000!

Huku pawaga wana msemo usemao"cha mtu huliwa na mtu"
 
Back
Top Bottom